Mimi ni muislam wa kuzaliwa kwa baba yangu na mama yangu, kwa kifupi nauamini na naupenda uislam kwa kuwa ni dini ya haki tuliamriwa na mwenyezi mungu tuifuate, hapa naweka wazi kuwa bado siyaelewi vizuri madai yetu dhidi ya serikali, mara kwa mara nimesoma na kusikia waislam tukilalamika tunanyimwa haki zetu, lakini bila kuyataja ili tuwe tunambana kwa kudai vitu vinavyojulikana, uislam unahimiza kukumbushana bila ya kutukanana, yeyote anayeyajua haki tunazozulumiwa aziorodhesha hapa ili tuungane