Tetesi: Ni nini faida za CWT Kwa wanachama wake ambao ni walimu

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,798
21,395
Kama Uzi unavyojieleza. Chama Cha walimu Tanzania (CWT), kimeanzishwa zaidi ya miaka 40 iliyopita. Ninaomba wanachama wa CWT waeleze faida za CWT Kwa wanachama wao ambao ni walimu
Pili ninaomba kujua asilimia 2% inayokatwa kutoka Kwa mwalimu ambaye ni mwanachama zinamfaidisha nini mwalimu au mwanachama ambaye ni mwalimu?
Tatu, ni nini hatima ya wanachama wa CWT iwapo wanachama wataamua kujiondoa uanachama?
Mwisho makusanyo ya mabilioni kutoka kwenye mishahara ya walimu kwenda CWT kwanini hayatumiki kusomesha walimu walioko vyuoni ili wakija kuajiriwa wawe wanachama wao.
 
Nijuavyo mimi CWT ni stepping stone ya viongozi wakuu wa chama hicho kuwa viongozi wakuu wa kisiasa
mfano ni mama sitaa,na waziri mkuu na wengine unaweza ongezea.Kwa wanachama wa kawaida kunufaika
sijui kama lipo wazi ndo maana ndo karibia kada inayoongoza kudharauliwa japo ni muhimu sana.
Natangaliza samahani kama nimewakwaza wenzangu kwa kusema ukweli
 
Chama feki sana hiki. Pamoja Na mikiki yote ya walimu lakini wameshindwa kukikataa hiki chama!
 
Hichi chama cha CWT kitakua kinaubia na serikali, kwani jinsi walimu wanavyo nyonywa! Ingesha wasaidia walimu!
kwan nichama cha lazima na kuna walimu walijikuta wanakatwa bila hata kujaza fom ya kujiunga na chama! Na kuishia kupewa t-shirt na bando za bati za kujengea banda la sungura watatu.
 
HAKINA faida yoyote.

Yapaswa Waalimu waungane kisha wawapeleke Hawa viongozi wa CWT mahakamani kwasababu wanawaunga kwenye chama automatically bila ridhaa yao.
 
True! Sab walimu wengi walijikuta wanakatwa, hasa enzi zile salary slip zinapatkana halmashaur, ingawa had sasa mchezo huo unafanyika hasa kupitia viongoz wa CWT ngaz ya shule, yani mwalim ana mchomesha mwalim mwenzake, inauma sana.
 
Utaratibu wa kukata ada ya uanachama kwa kuangalia basic salary ya mtu ni wa kijima kwani walimu wote wanahudumiwa na hako kachama kwa kiwango sawa licha ya kwamba siku hizi wamekalia kukata hiyo asilimia mbili na si kutetea maslahi ya walimu .Inasikitisha walimu wengine wanachangia zaidi ya tsh 25000 kwa mwezi wengine si zaidi ya tsh 10600 .Kutokana na idadi ya walimu tz isiyopungua 285000 ilitakiwa wakate flat rate tsh 5000 na bado wangekusanya mamilioni ya fedha ambazo zingewawezesha kuishi maisha mazuri tu.Enyi cwt sikilizeni manung'uniko ya wanachama wenu kuhusu hayo makato yasiyo ya haki
 
2% ya mshahara NDIYO wanayokata. Kuna walimu wanafyekwa zaidi ya 48,000/-kila mwezi. Yaani zaidi ya 570,000/-kila mwaka. Huu ni wizi /ujambazi!!!!!!!!!
 
Kuchangia chama, maana ukijidai kuhoji Tu mambo yanayogusa vyama ambavyo ni matawi ya fisiemu, utatafutiwa kesi za ugaidi na uhujumu
 
Utaratibu wa kukata ada ya uanachama kwa kuangalia basic salary ya mtu ni wa kijima kwani walimu wote wanahudumiwa na hako kachama kwa kiwango sawa licha ya kwamba siku hizi wamekalia kukata hiyo asilimia mbili na si kutetea maslahi ya walimu .Inasikitisha walimu wengine wanachangia zaidi ya tsh 25000 kwa mwezi wengine si zaidi ya tsh 10600 .Kutokana na idadi ya walimu tz isiyopungua 285000 ilitakiwa wakate flat rate tsh 5000 na bado wangekusanya mamilioni ya fedha ambazo zingewawezesha kuishi maisha mazuri tu.Enyi cwt sikilizeni manung'uniko ya wanachama wenu kuhusu hayo makato yasiyo ya haki
CWT walishaweka pamba masikioni! Sjui nani wa kupiga kopo la kombolela, sab kunatetes hata mwendazake alichota mabilion CWT, so kama ni kweli, then CWT inaidai serikali kama mifuko ya hifadhi kama PSSSF, so, wakuwaokoa walimu sijui atatokea ktk dunia hii au mbinguni.
 
Kazi ya vyama vya wafanyakazi Tanzania ni kudhibiti wafanyakazi. Hata CWT ndio kazi yao.

Walimu ni jeshi kubwa. Bank ya walimu mpaka sasa hivi iko hoi, wakati ingeweza kubeba walimu wote na kuwa bank kubwa.
 
Cwt ni taasisi ya wakubwa,wanakula kwa mgongo wa jasho la mwalimu. Pamoja na kupigiwa kelele,kushauri hata na marais waliopita juu ya utendaji na makato yao lakini hawabadiliki and nobody cares,na walimu wanahisi ipo siku cwt itabadikika bila wao kuchukua hatua. Walimu amkeni,wa kuikataa cwt ni nyie,hakuna mwanasiasa atakayewatetea.
 
Back
Top Bottom