Ni nini faida, changamoto na hasara za kazi za nje ya nchi, hasa Mashariki ya Kati?

The Hebrew

JF-Expert Member
Feb 7, 2015
348
442
Wapendwa natafuta ufahamu, ujuzi na uzoefu kwenu, kama maelezo hapo juu.

Mazingira ya ajira katika nchi nyingi za kiafrika ni ngumu na si kwetu Tanzania pekee. Kumetokea vijana wengi wanatoka Tanzania kwenda kufanya kazi nje (Kazi za kawaida) na hasa bara la Asia.

Nimekua nawasiliana na baadhi wakiwa huko, kwa maelezo yao mishahara yao ni mizuri ambayo kwetu huku ni pesa nzuri tu sawa na mishahara ya wasomi wetu hapa nyumbani japo kazi hizo huko kwa wenzetu zinahitaji sana ujuzi na uzoefu kuliko shule.

Naomba kufahamishwa, ni nini basi faida, changamoto na hasara za ajira hizi?
 
Mkuu umekuwa ukiwasiliana na baadhi yao ila haujabahatika kujadili nao juu ya changamoto, faida na hasara!?
Nimefanya hivyo, ila si kila kitu waweza ambiwa, pengine upo ugumu flani ila mtu kwakua anakaa na kufanya kazi huko ni anataka kukuonesha kila kitu kipo sawa. Nimeuliza hili kwakua nimeona naambiwa vitu positive ni kama hakuna changamoto vile.
 
Wabongo acheni hizo bana,Ukiambiwa mazuri unataka mabaya,ukiambiwa mabaya unata mazuri.Usipoambiwa unanua.Mabaya huwa yapo ila nategemea na mtazamo wako.Cha muhimu ni uwe tayari kupigika na kupiga kazi.
 
Nimefanya hivyo, ila si kila kitu waweza ambiwa, pengine upo ugumu flani ila mtu kwakua anakaa na kufanya kazi huko ni anataka kukuonesha kila kitu kipo sawa. Nimeuliza hili kwakua nimeona naambiwa vitu positive ni kama hakuna changamoto vile.
Mi ningekushauri ujikite ktk kuuliza namna nzuri ya kufika huko ukasake maisha, mambo mengine utayajua ukifika huko.
 
Upo sawa Mkuu. Ila nauliza lililo na changamoto kwangu, sioni kama namna ya kufika ni tatizo ila nashukuru kwa maoni yako.
 
Mkuu kwanza, ridhika na ugali-dagaa wa nchini kwako. Mambo ya kutaman kwenda kuwa kibarua ugenini utakuwa mtumwa ambaye utapata mateso bila msaada kwa jiran kwa sababu kila jiran kule sio ndugu yako.

Pili, ogopa sana waAsia ni miongon mwa jamii za watu katili sana duniani. Usisahau pia tuhuma zao za kupenda 0713.

Tatu, usidanganyike na mshahara mzuri wa nchi za Asia kwa kuulinganisha na maisha ya hapa Bongo. Nchi za kule gharama za maisha nazo ziko juu kiasi kwamba hyo hela wanayokutajia kwa maisha ya kule huenda itakusaidia kula na kukodi kachumba cha kulala.

Tafakari kisha chukua hatua.
Hapa kwenye 0712 hujadanganya kabisa maana kuna vijana wengi sana nimeshuhudia waliokuwa wameschukuliwa kwenda kufanya kazi nchi flani hivi uarabuni hakika waliporudi huwezi kuamini ni wao kwa jinsi walivyoharibiwa na kuathirika kisaikolojia mioyoni mwao.

Sent from my ONEPLUS A3010 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwanza, ridhika na ugali-dagaa wa nchini kwako. Mambo ya kutaman kwenda kuwa kibarua ugenini utakuwa mtumwa ambaye utapata mateso bila msaada kwa jiran kwa sababu kila jiran kule sio ndugu yako.

Pili, ogopa sana waAsia ni miongon mwa jamii za watu katili sana duniani. Usisahau pia tuhuma zao za kupenda 0713.

Tatu, usidanganyike na mshahara mzuri wa nchi za Asia kwa kuulinganisha na maisha ya hapa Bongo. Nchi za kule gharama za maisha nazo ziko juu kiasi kwamba hyo hela wanayokutajia kwa maisha ya kule huenda itakusaidia kula na kukodi kachumba cha kulala.

Tafakari kisha chukua hatua.
Mpe kidokezo hiki ( kwa kuwa hakutaja nchi)

✓ Kwanini raia kutoka India wakija kwetu hawatamani kuondoka....kama Asia maisha ni mazuri? Yaani nilikuwa nafanya kazi kwenye Kampuni moja hivi Mikocheni kwa - Mwalimu walikuwepo Wahindi wakutosha pale..basi siku moja, mmoja akaambiwa kazi zimepungua hivyo unapaswa kurejea kwao India .. huwezi amini alilia sana yule raia wa India.

✓ Kwanini Kariakoo wamejaa Wachina ili hali kwao Asia maisha ni mazuri?
 
Basi pengine nitoe baadhi ya nchi, maana hiyo unazungumza ni mashariki ya mbali si mashariki ya kati.

Kama yupo anayeweza zungumzia sehemu kama Dubai na Abu Dhabi.
 
Nimepitia michango ya baadhi ya wadau wanaoponda kufanyia kazi huko mashariki ya kati...nilichoelewa ni kuwa wengi wao hawana exposure. Wanaongea vitu kwa mihemuko.

Mtu anakupigia mfano eti wahindi na wachina wapo wametulia hapa Tanzania kungekuwa kuzuri huko mashariki (ya kati) si wangeenda huko kufanya kazi?

Huyo anaetoa sababu hiyo hajawahi kufika huko mashariki ya kati akaona kama wahindi na wachina wapo au hawapo huko...basi si angejaribu hata kusearch information kwenye google kujua idadi ya wahindi/wachina waliopo mashariki ya kati wanapiga job.
 
Kweli nimeamini penye miti hkn wa kwezi!!! wewe si mjilipuaji!! ila una tu iga iga tu!!!! uko nyorornyoro sana!! inaonekana huko baba hapa kufai!!

tulitishwa ooh! Dar maisha magumu kaeni hapahapa kwa baba yenu! maweee! nani? Tata nyarusare au!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom