Ni nini dawa ya chunusi usoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini dawa ya chunusi usoni?

Discussion in 'JF Doctor' started by Tuko, Jan 19, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Wapo watu ambao wanasumbuliwa na tatizo sugu la chunusi, madoa doa na kuharibika kwa ngozi. Ingawa chunusi hizi mara nyingi hutikea usoni, wakati mwingine hutokea pia katika maeneo tofauti ya mwili.

  Kwa bahati mbaya baadhi ya waathirika wa chunusi wamejikuta wakitumia madawa mengi bila matibabu, hata mara nyingine kuharibu kabisa ngozi zao.

  Habari njema ni kwamba, imegundulika kwamba matatizo mengi ya ngozi yanayotokea usoni, hasa chunusi ni kwa sababu ya aleji (mzio) ya vyakula tunavyokula, au matatizo mengine yatokanayo na vyakula vya protini. Kwa bahati mbaya, madaktari wengi wa aleji hawawezi kugundua kama chunusi ulizo nazo ni aleji kwa sababu wanafanya allergy test kwenye ngozi, wakati aleji yenyewe iko ndani tena kwenye kiungo specific na yanayoonekana nje ni madhara tu

  Vyakula mabvyo vimetajwa kuwa huweza kusababisha allergy ni;
  - Maziwa
  - nyama
  - mayai
  - samaki
  - kuku
  - wadudu wanaoliwa kama senene, kumbikumbi nk

  Hata hivyo sio rahisi kwa mtu mmoja kuwa na allergy ya hivyo vitu hapo juu vyote, na hivyo haimaanishi kama una hilo tatizo basi ndio mwisho wako wa kupata animal protein hapana, ingawa unaweza kuwa na allergy ya kimoja au baadhi ya hivyo.

  Je, utagunduaje kama chunusi ulizo nazo zinasababishwa na allergy ya kimoja au baadhi ya vitu nilivyotaja hapo juu?
  Kumbuka, unaweza kutembelea hospitali zote wakafanya allergy tests zote na wasione tatizo, lakini allergy bado iko pale pale. Kwa maana hiyo, namna pekee ni kwa wewe mwenyewe kujifanyia test kama ifuatavyo;

  1. Acha kabisa kutumia vyakula vyote vilivyotajwa hapo juu kwa wiki 3. Ina maana kwa wiki hizo 3, utakuwa vegetarian..lol
  2. Kama hautaona mabadiliko yeyote, then utagundua kuwa tatizo lako sio allergy hivyo endelea na maisha kama kawaida, huku ukitafuta matibabu mengine.
  3. Kama utaona mabadiliko ya kupungua au kuisha kwa tatizo, then mshukuru Mungu wako, maana tatizo lako linaelekea kupata ufumbuzi. Cha kufanya hakikisha tatizo limeisha kabisa ndani ya hizo wiki tatu, au ukiona limepungua halijaisha, then subiri hadi liishe then nenda kwenye step 4 hapo chini...
  4. Tatizo likiisha, anza kurudisha kimoja kimoja, ukianza na mayai. Kula mayai 1-2 kila siku kwa siku 7-10 halafu jiangalie kama tatizo lipo. Kama limerudi, acha mara moja kutumia mayai, na subiri hadi liishe kisha ndipo uende step 5 hapa chini
  5. Tumia maziwa (kumbuka hii ni siku 10 tangu uanze kutumia mayai). Unaweza kuendelea kutumia mayai (kama hayakuleta tatizo katika step 4), kwa rate ya kawaida uliyokuwa umezoea zamani. Kunywa takribani 200ml hadi 500ml kwa siku kwa siku kumi. Hapa naongelea maziwa ya ng'ombe. Kama unatumia maziwa ya mnyama mwingine, then nayo yawe tested katika step tofauti.
  6. Endelea na vyakula vingine vilivyobaki, ukirudisha kimoja kimoja kila baada ya siku kumi, hadi utakapogundua ni kipi kati ya hivyo hapo juu kinachokusababishia tatizo

  NB; 1. Nyama ya ng'ombe, mbuzi, nguruwe nk ziwe tested tofauti. Nina rafiki yangu anaathiriwa na nyama ya ng'ombe tu sio kitimoto wala mbuzi!

  2. Kwa akina dada/mama, tofauti na chakula pia tatizo linaweza kuhusiana na proteins zilizomo kwenye semen za mwanaume/wanaume, na bahati mbaya sana ni kwamba unaweza kuathiriwa na semen ya mwanaume mmoja na sio mwingine! Kivumbi kitakuwa pale unapoathiriwa na semen za mumeo, mbaye kumwambia mtumie condom sio rahisi... Kama tatizo ni hili, hapa inabidi mpime ama kukubali kuishi nalo, au uwe unatumia anti-ellergens kila mnapokutana, lambo ambalo hakuna Dr yeyote duniani atakushauri ufanye.

  Kama hujaelewa hiyo regime hapo juu, unaweza ukauliza na kupata ufafanuzi mzuri zaidi...


  Additionally,
  matatizo ya ngozi usoni yanaweza kukupa ishara ni kiungo kipi cha mwili wako kina mataizo

  [​IMG]
   
 2. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkaa mweusi, ni ngumu sana kutoa chunusi kabisa ndani ya siku chache kama utakavyo, ninachojua mimi utapunguza tu makali ya chunusi hizo ndani ya wiki mbili kama utaconcentrate kati Tips chache zifuatazo...


  • Kwanza kama unatumia any cream usoni kwa sasa achaa
  • Nenda HS Amon nunua facial inaitwa ''Cleans up'' inauzwa 10,000
  • tafuta( asali halisi) ya nyuki isyo na chemicals,utakuwa unachanganya na kiini cha yai kila siku
  • Nunua sabuni ya ''spot removal ya nyanya, sh 3000 tu madukani
  Osha uso asubuhi na jioni kwa kutumia hiyo sabuni, then ufanye facial ya clean up, facial mara moja tu kwa siku, bandika mchanganyiko wa asali na yai usoni, acha ukauka vizuri, osha uso kwa maji ya vuguvugu, usipakae oily lotion, ukimaliza tu kukaucha uso waweza paka poda

  Nilishajaribu ikanisaidia kwa muda wa siku 10.
  Note.. huwezi kuclear madoa yote kwa muda mfupi, itaheal pole pole.
  Caution, Wapambaji ni wataalam sana, usiwe na wasiwasi wa siku yako, mpambaji ataweka make ups wala hazitaleta show mbaya siku ya harusi, usiende tu kwa mpambaji mbaya.
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Chunusi ni matatizo ya ndani ya ngozi amabyo ama husababishwa na hormones au wingi wa mafuta mwili, kwa hivyo hakuna dawa ya kupaka inayoweza kutibu chunusi. Lakini zipo dawa na njia za kuweza kupunguza ikiwemo asali. Nyengine ni utomvu wa Alaoe vera, mafuta au cream zilizotengenezwa nayo. Wakati unatumia njia yoyote, hakikisha unawacha kabisa kula vyakula vyenye mafuta pamoja na sukari kama vile chocolates na vitu vitamu vyengine isipokuwa matunda.
   
 4. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sijui umri wako lakini chunusi mara nyingi huwapata vijana wanaobalehe na hii ni kwa sababu wanakuwa na vichocheo aina ya androgens kwa wingi ambavyo kwa namna moja au nyingine husababisha chunusi. Pia kuna vimelea vya bacteria aina ya p. acnes, ambavyo baada ya matundu ya vinyweleo kuziba hukaa ndani ya matundu hayo kuzaliana na kusababisha chunusi kuvimba.

  Matibabu sana ni usafi wa ngozi ya uso, angalau mara mbili kwa siku na sabuni yenye dawa (medicated soap), acha kupaka mafuta ya mgando usoni, acha kuminya hizo chunusi kwani husababisha zipate uambukizo wa pili wa bacteria (secondary bacterial infection) ambao watasabisha usaha na makovu makubwa usoni, usishike shike uso wako kwa mikono mara kwa mara.

  Kwa upande wa dawa tafuta cream ya benzoyl peroxide (hii ni cream ya dawa ina antibacterial effect sio ya urembo), osha uso wako vizuri na ukaushe then ipake hiyo cream kwenye sehemu zote zilizoathirika na chunusi, paka mara moja au mara mbili kwa siku kutegemeana na ukubwa wa tatizo.Pamoja na hiyo cream antibiotics aina ya tetracyline hutolewa pia, zitumike kwa siku 10 mpaka wiki 2.

  Chunusi zikizidi kamuone daktari bingwa wa ngozi (dermatologist) atakusaidia vizuri zaidi.
   
 5. L

  Leornado JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Pasha asali kidogo, paka usoni usiku asbh unanawa.

  Pia maji ya limao yanasaidia kupunguza mafuta usoni, kamua limao kwenye maji kidogo nawa nayo.

  Acha kula vitu vya mafuta kama karanga, blue band nk.

  Kunya maji walau lita tano kwa siku inasaidia sana kutoa uchafu mwilini.

  Ikizidi muone mtaalamu wa ngozi.
   
 6. Uda'a

  Uda'a JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 221
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kila siku asubuhi tumua mkojo kunawa uso yaani ule mkojo wako wa kwanza kabisa ukishanawa kaa km dakika 3 kisha osha uso kwa maji kawaida ,tumia huo tu kwa muda na utaona mabadiliko.

  Mimi nina ushahidi kabisa toka kwa dada yangu yaani uso wake ulikuwa unatisha sana tena kwa miaka mingi alikuwa hivyo na kila akikutumia dawa hali ilikuwa pale pale. Aliyekuja kumkutonya ni rafiki yake ambae nae alikuwa na tatizo, mwanzoni hakuamini na aliona kinyaa ili ilimlazimu tu kwa sababu ya shida, yaani ukimuona sasa ana ngozi nzuri kabisa.

  Sasa tukija kitaalam hapo ndio sielewi mkojo unatibu ki vp.

  Kila heri....
   
 7. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kama kuna vitu vilinitesa kwenye usichana wangu ni chunusi, nakumbuka mpaka dada zangu walikuwa wananiita dudu!! au wanasema mamdogo umekuwa na sura ka ganda la fenesi!!

  Nilikuwa naona aibu hata kutoka na wenzangu ila namshukuru Mungu kwa sasa uso wangu u kama wa mtoto!!! ila nilichotumia hata sikumbuki maana makorokoro yote ya uso nilimaliza.
   
 8. U

  UNIQUE Senior Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utakesha sana hospitali. Hilo ni tatizo la mwili wako kushindwa kutoa uchafu mwilini. Kunywa maji ahai ya bio disc. Soma Amezcua na uwasiliane nami privately. unique
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Let me tell you the best natural treatments for acne. These methods are also a very good alternative for the people who don't want to go through surgical treatment or the ones who cannot afford enough money for the treatment.

  Virgin Coconut Oil: It is very efficient in curing skin ailments and also to lighten pigmentation. Usually your acne marks are hyper-pigmented, so you can replace your moisturizer with coconut oil in order to lighten your acne marks.

  Papaya: They are commonly known for its ability to lighten skin. Papaya is an important constituent in soaps and highly effective in treatment of acne marks. You can use the fruit pulp and smear it over the mark. Now leave it like this for about half an hour and allow your skin to absorb all its nutrients.

  Sandalwood Oil: It is very helpful in reducing pigmentation therefore it can be used for treating your acne marks. You could also use it as night renewal oil when you apply it over the marks and leave it overnight. It can also work as a moisturizer during the day time.

  Aloe Vera: It is the latest method used now days for treatment of acne. There are many soaps and gels made of Aloe Vera which are used to heal the skin damaged by acne.

  Mix Lime Juice and Rose-Water: What you need to do is to mix lime juice and rose-water every night in equal portions after you had thoroughly washed your face. Now keep it like this for 30 minutes. Wash your face again and let the pat dry. This is one of most effective natural treatments for acne.

  Mix Honey and Cinnamon Powder: You can just make a paste by mixing honey and cinnamon powder. Apply this paste on your face before going to sleep and wash it the next morning you get up.

  All these methods are natural treatments for acne. So they will never harm your skin or body. Plus all the ingredients you need are easily accessible and cheap.

  Natural Treatments for Acne - How To Get Rid of Acne Permanently

  http://www.kamusi.org/en/lookup/en?Word=acne
   
 10. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umri wako wako ungesaidia kujua,kama ni za ugonjwa ama ni za kiumri
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Umri umri hii ndo jamii forum watu hawakurupuki kutoa ushauri,pili hapo S.H amon umeonana na wataalamu au wafanyabiashara? sio maneno yangu nimenukuu kutoka kwa wadau juu hapo
   
 12. d

  dee dee Member

  #12
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushauri unywe maji kwa wingi sio chini ya glass nane kwa siku, mazoezi kidogo na chakula chako kiwe na mboga mboga zaid na matunda. Kila la heri
   
 13. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kama wewe ni mwanamke
  mahitaji
  1 johnsons facial scrub
  2johsons facial cleanser
  3johnsons toner
  4johnsons day cream
  5johnsons night cream utapewa na jinsi ya kutumia ukishindwa nipm
  pia kunywa maji na matunda kwa wingi epuka na red meat
   
 14. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #14
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  smile...huyu mtu anaweza akawa anabalehe....sasa hizo Jonsoni....sijui....!
   
 15. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hzi ni user friendly hata mtoto anaweza kutumia preta ndo maana sijampeleka kwa kina caro?????????????
   
 16. MKOBA2011

  MKOBA2011 Senior Member

  #16
  Nov 11, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna sabuni nzuri naifahamu nafikiri it will help you even if it is very expensive na kuna lotion yake nayo ni nzuri utaipenda nipm nikupe maelekezo
   
 17. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #17
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  punguza vyakula vya mafuta fanya mazoezi safisha uso mara kwa mara na maji ya moto kuyeyusha mafuta yaliyo usoni epuka kijipakaa mafuta ya mgando,kula matunda na mboga za majani kwa wingi.usipata nafuu nakushauri umuone daktari itakuwa ni ugonjwa.
   
 18. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  halafu hayo majonson kuna watu huwa yanawaharibu.
   
 19. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #19
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Ilikuwa mwaka 2007 nilikuwa nimemsindikiza dada yangu duka mojawapo la s.h.amon dsm kununua dawa zake, tukiwa kaunta hapo aliingia mama mmoja na kumwambia dakatari kuwa dawa aliyompa kwa ajili ya chunusi haikumsaidia sana, daktari yule alimuuliza: ''lakini MAJI unakunywa?'', yule mama akajibu; ''ndiyo nakunywa'', daktari akamuuliza tena; ''kiasi gani?, maana usiseme unakunywa kumbe unakunywa vikombe viwili tu''. Daktari akamwambia atamubadilishia dawa nyingine.

  Tulipotoka nje ya duka lile nilimuuliza dada yangu: ''umesikia maneno yale aliyosema daktari kwa yule mama?''. nilimweleza dada yangu kuwa daktari yule alipaswa kumwelekeza yule mama namna ya kunywa maji na chunusi zake zingepotea bila kupenda. Nilimwambia pia dada kuwa mahospitalini mara wanapokupa dawa wanasisitiza unywe na maji mengi ili dawa hiyo wanayokupa isikuchoshe sana. Nadhani hili watu wengi watakiri kuwahi kuambiwa hivyo.

  kwa kawaida siku utakapokuwa mahututi na unakimbizwa hospitali na ambulance, njiani madaktari watakutundikia dripu la MAJI/CHUMVI. Muda huo hawatakuandikia tena quinine!!!!. MAJI NI UHAI. bali ukilima bustani utaimwagilia maji asubuhi kabla jua halijawa kali la sivyo mimea itakufa kama utasubiri saa nane mchana jua limewaka ndo umwagilie maji. Hivyo hivyo, tunapaswa kunywa maji kabla ya kusikia kiu.

  We kunywa tu maji kwa mujibu wa maelekezo yaliyomo humu: Utangulizi | maajabu ya maji, hayo mafuta na sumu zilizozidi mwilini vitakimbia vyenyewe bila kupenda. kula vyakula vya alkalini zaidi na siyo vyenye asidi.
  Unazijuwa kazi za maji mwilini? http://maajabuyamaji2.artisteer.net/kwanini-unahitaji-maji-kila-siku/
   
 20. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  1. Chukua asali uchanganye na mdalasini ujipake usoni na shingoni uweke kwa muda wa nusu saa na baadae ukoshe kwa maji ya vuguvugu (warm water).
  2. Pia unaweza kutumia maziwa yaliyochemshwa na uyatie ndimu/limau na uyaache kwa dakika kumi, kabla ya kulala ujipake usoni shingoni na hata mikononi.
  3. Jisugue usoni na shingoni kwa kutumia kipande cha ndimu/limau na baadae changanya maji ya ndimu katika maji ya kawaida unawe uso.

   
Loading...