Ni nini chimbuko la fikra za mabadiliko Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini chimbuko la fikra za mabadiliko Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Jun 3, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima Kwanza!

  Kupevuka kisiasa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutafiti, kudadisi, kuhoji, kufuatilia na kushiriki kikamilifu katika maswala yote yanayohusu maisha ya kila siku. Siasa haiwahusu wanasiasa peke yao.

  Katika kipindi hiki ambapo watanzania wengi (hasa vijana) tuna shauku ya kufanya mabadiliko makubwa ya kisiasa yapo mambo mengi ya msingi ya kujadili.

  Moja ya mambo hayo ni chimbuko la fikra za mabadiliko nchini. Tukiacha Ufisadi, matumizi mabaya ya serikali, mfumo na mgawanyo wa madaraka na mfumuko wa bei unaosababisha uwepo wa maisha magumu kwa majority, Je tukienda mbele zaidi, ni nini chimbuko la fikra za mabadiliko nchini?
   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Chimbuko la mabadiliko ya fikra ni jamii yenyewe. Huwezi kuacha ufisadi. Utaupunguza tu kwa kiwango ambacho hakitaleta mapungufu ya utekelezaji wa huduma za jamii.
   
 3. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa imani na mitazamo gani? Twende mbele zaidi na tufunguke kwa kuangalia mitazamo ya kifalsafa ambayo ina mahusiano na jamii yenyewe.
   
 4. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,528
  Likes Received: 16,510
  Trophy Points: 280
  Chimbuko la madiliko ni ukosefu wa ajira na utandawazi.Pia sera mbovu za umilikishwaji wa keki ya taifa ,uongozi wa kurithishana mtoto wa mtu mwenye jina.Pia uongozi mbovu uliopo serikalini kuanzi juu mpaka chini.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wamngu kwanza umeuliza swali na ukayatoa wewe mwenyewe majibu halafu unataka twende mbele zaidi ya swali lenyewe hapa nimeshindwa kukuelewa. Kupevuka kwa siasa nchini imetokana na hayo uloyataja hakuna zaidi isipokuwa tukitaka kufikiria zaidi nje ya madai haya inakuwa kesi isokuwepo kwa sasa.

  Watu wamechoka na utawala unaolinda maslahi ya watu wachache binafsi wakati majority yao ni maskini - survivor of the fittest wakati hawana mtaji tosha kuwa Capitalist.

  Hili ni swala la kimfumo na binafsi yangu naamini hata kama Katiba itabadilishwa, vuguvugu hili litaongezeka kasi yake kwa sababu hata katiba iliyopo inapingana na maswala yote yanayotendeka leo nchini.

  Hivyo, kikubwa hapa ni kwamba tumekosa UONGOZI BORA toka chama tawala kusimamia matatizo hayo uloyataja hapo juu. Hivyo basi Wananchi wakiwezeshwa (Utajirisho) kwenda sambamba na Capitalism inawezekana.
   
 6. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwenye RED nimesema tuyaweke pembeni tujadili zaidi ya hapo, so sikujibu swali ila nimetoa mwelekeo wa swali. Nadhani tunahitaji kufikiri zaidi ya hapo, tusitoe majibu ya jumlajumla ili kupanua wigo wa mjadala.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nadhani nimekujibu vizuri tu.
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180

  To engage in philosophical discourse isn't one of my strengths. So I will try to stay in the margin. I believe that Tanzania of today is facing fundamental problems that challenged developed nations more than 60 years ago: income inequality, poor housing, poor education, and unemployment. To compound the matter, the population has skyrocketed, and the tradition means of productions aren't sustainable anymore.

  What's worse, there's huge pressure from regional and global competitors who are vying for the same resources that many Tanzanians took for granted just a decade ago. Tanzanians feel that they are being marginalized in their own country, and very little has been done to address their predicaments because people at the top are corrupt and incompetent.
   
 9. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Historia inatufundisha kuwa madiliko katika mazingira ni chanzo kikubwa cha bidadamu kuanzisha mbinu mpya kukabiliana na changamoto.

  Mazingira hapa ni kila kitu watu, viongozi, siasa, hali ya hewa n.k. kwa sasa Tanzania ina changamot nyingi huwezi kuacha ufisadi kama moja ya changamoto hizo.

  Kwa hivo watanzania wapo katika harakati za kupambana na vikwazo kadha wa kadha. Hakuna mtu mmoja anawaambia watanzania kuwa sasa tatizo lenu ni hili... tunatofautiana ingawa kuna yale yanayotuunganisha hasa yale ya siasa za Tanznia na za ulimwengu ambayo ni ya kila siku.
   
Loading...