Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,735
- 40,858
Hakuna kitu kama "nidhamu ya woga" kazini. Kinachoitwa "nidhamu ya woga" ni dalili ya watu wazembe, wasio na weledi, na ambao hawana ufanisi kazini isipokuwa hadi wasimamiwe. Wafanyakazi wenye hiki kinachoitwa 'nidhamu ya woga' hawawezi kufanya kitu hadi mtu awasimamie, na ukiwaacha wenyewe hawajui pa kwenda. Wenye nidhamu ya woga hutegemea wengine kutimiza kazi zao na niwepesi 'kujishughulisha' kuliko kufanya kazi!
Ukiwaona wanavyoshughulika unaweza kuamini wanafanya kazi; ukisimama karibu yao kama wewe ni kiongozi juu yao utaona jinsi ambavyo wanashika karatasi hili, na kubonyeza hapa na pale kwenye kompyuta zao kana kwamba wanafanya kazi! Na niwepesi sana kuita "mheshimiwa" ili waonekane wako makini. Ukiwaacha kwa sekunde chache tu hawachelewi kuweka miguu juu, kushika simu zao na haraka kusahau kabisa kama walikuwa wanatakiwa kuwa wanafanya kazi. Wanadhani wanatakiwa kujishughulisha wanapokuwa kazini; wanapenda shughuli kuliko kazi!
Ukiwa mtumishi wa umma ni lazima uogope; uogope kuvunja sheria, uogope kutumia madaraka yako vibaya, uogope kukutwa unavuruga! Unatakiwa utende kazi kwa kujiamini, kwa weledi na kwa ufanisi unaotakiwa kutokana na nafasi yako. Sasa bosi wako akitokea na kukuta umekunja nne ukaruka juu na kujimwagia chai na kuanza kujifanya unafanya kazi manake ni kuwa hukuwa mwoga in the first place! Ungekuwa unaogopa ungekuwa huna wasiwasi. Hivyo, woga wa kinidhamu unahitajika na viongozi waendelee kuwashtukiza na kuwatumbua hasa kama watumishi hawawaogopi mabosi wao au viongozi wao wajuu.
Huu unaitwa woga wa kinidhamu; woga ambao inaonekana umekosekana muda mrefu kwa baadhi ya watumishi wetu. Wanaposimamiwa na kushtukizwa wanajihisi wanaonewa na kuwa mkubwa au bosi wao (mtu kama Rais au Waziri Mkuu) anasimamia hata vitu vidogo sana (micro manager). Utawasikia "kwani lazima yeye afuatilie si amuachie mtu wa chini yake" kwa maneno mengine; wanataka wasifuatiliwe kwa karibu na watu wajuu! WAnajua hawa mabosi wao wa karibu ni 'wenzao'; hawawakaripii, hawawagombezi, wakitaka kuwaonya hadi wawaite ofisini ili kutunza heshima zao! Wamezoeana nao sana!
Watendaji hawa walidekezwa; walidekezwa wakadeka na kudekeka; hawakuzoea kabisa kugombezwa (kwani wanaweza kuangusha kilio); hawakuzoea kuulizwa makali (wanajihisi wanadhalilishwa); hawakuzoea "kuambiwa hapana" kwani wanaona wanabanwa pasi ya sababu!
WAnataka waachiliwe waendelee walivyokuwa wanafanya shughuli zao (siyo kazi zao). Wanataka wawe walivyokuwa. Wengine wanataka Rais abakie ofisini tu; na akija Waziri watasema kwanini asibakie ofisini tu; na akija Mkuu wa Idara watasema kwanini asibakie ofisini tu!
Hizi ni zama mpyal; hawataachwa tena wajishughulishe tu...
]
Tulidekezwa mno hadi tukadeka na kuamini tunatakiwa kudekezwa.