Ni ngumu kuwa kiongozi imara kama unatokea kwenye umaskini mkubwa

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,697
Huu ndio ukweli kwa asilimia nyingi , ni watu wachache sana wawili kati ya kumi. Watalaamu wa masuala ya sayansi ya jamii utajiri hauna mipaka na ndiyo maana inakuwa ngumu kupata dhana halisi ya utajiri. Hakuna mpaka kwa maana kwamba hakuna kiwango halisi cha mali au fedha ambazo mtu inabidi akifikie ili aitwe tajiri. mtu mwenye baiskeli mbili ni tajiri ukimfananisha na mtu mwenye baiskeli moja, mtu mwenye gari mbili mbili ni tajiri ukimlinganisha na mtu mwenye gari moja.

Sasa ngoja tujikite kwenye mada, mtu aliyetoka kwenye familia, ukoo, eneo ambalo lina umaskini mkubwa ni ngumu sana mtu huyo kuwa kiongozi imara kwa sababu ya mazingira mtu huyo anakuwa mwoga by nature. mara nyingi humudu kazi za kawaida za utendaji ( kama ualimu, uuguzi, nk) na wanakuwa mabingwa huko kuliko kazi za uongozi zinazohusu kufanya maamuzi makubwa. mtu amaye alipokuwa mtoto alikuwa anaomba midori ya kuchezea kwa mwenzake atakuwa sio jasiri. baadaye.

Nimewahi fuatilia historia ya kiongozi mmoja aliyejitamba kwamba yeye katokea familia duni lakini kuna siku moja alikuwa anahojiwa startv akiwa kwao singida akiwa na mzazi wake huku akionyeshwa na kundi kubwa la ng'ombe alizonazo mzazi wake na yeye mwenyewe kueleza kwamba walikuwa wanatumia muda wa jioni kuchunga mifugo huku wakiwa matumbo wazi, kimsingi hao hawakuwa maskini. Hata miaka ya nyuma viongozi wengi wa nchi hii wazazi wao walikuwa walimu hii ni kwa sababu zamani ukiwa mtoto wa mwl. ulikuwa unapata heshima kwenye michezo ya watoto kwamba wewe utakuwa baba na wenzako kuwapangia wawe majogoo wawe wanawika wakati wewe umelala.

Hata ukiangalia mikoa ambayo ina uchumi mzuri inatoa viongozi wazuri kuliko ile duni , ile duni wanakuwa waoga na hawajiamini katika maamuzi.

Hata wakati jamaa yangu mmoja anachaguliwa kuwa kiongozi wa mhimili mmoja nilijua hawezi kufanya kazi hiyo akapata sifa sawa na watanguliIzi wake,

Unaweza tu kujiuliza kati ya wagombea uraisi 38 ndani ya ccm kuna kanda ilitoa wagombea 22. Unaweza pia kujiuliza katika uchaguzi mkuu katika wagombea nane kuna kanda ilitoa wagombea watano.

Mazingira yanamtengeneza mtu awe kiongozi bora, wengine hata wakipewa nafasi ya kujaribishwa tu hawadumu katika nafasi hizo kama akina Nkamia na wengine.
 
umaskini ni kikwazo, mi nashukuru sikuwahi kupangiwa kuwika nilipokuwa mtoto, nilikuwa nawapangia wenzangu
 
Back
Top Bottom