Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,491
- 26,978
Ndugu zangu!
Tujilazimishe tu kusamehe na kuachilia. Sio kitu rahisi, lakini faida zake ni kwa maslahi ya kesho yako. Kwenye mapenzi unakutana na mtu ambaye humjui, unajifariji eti utamfahamu kupitia maelezo yake! Hii ni kujitekenya pakubwa.
Wengi wana yao mioyoni na hutoweza kuyajua, wenye majuto na hofu ya kuumizwa wapo. Wenye visasi vya kulipiza wapo, wale waliokata tamaa na kuona 'itakavyokuwa' tu nao ni wengi tu.
Kwa namna hizi na nyingine, iwe ni wewe au yeye. Ukiingia kwenye mahusiano mapya na kumbukizi mbovu au machale machale huwezi kufaidi mema walahi.
Tujifunze kusamehe na kujitakasa, waliokuumiza ni wengine sio huyu mwingine. Anza upya, na ufurahie maisha.
Ncha Kali.