Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,328
- 2,283
Nilikua napita pita kwenye Google Earth nimegundua miji mingi Tanzania imekaa hovyo hovyo sana.
Kuna nchi ziko jangwani kabisa lakini wamejenga kwa mpango mzuri. Hata DRC ambayo kuna migogoro kila mara bado kumepangwa vizuri. Tanzania badala ya kujenga miji mipya wanabomoa ya zamani na kujenga nyumba mpya sijui hili limekaaje.
Kwanini kila serikali ya mji isisimamie na kupima maeneo yake? Huenda labda wananchi wanaogopa kwenda kuchukua kibali cha ujenzi sababu ya gharama kwanini serikali isitoe vibali hivyo bure kama ni ujenzi wa nyumba ya kawaida kwa ajili ya makazi?
Kwanini kusiwe na sheria kali kabisa hakuna kujenga sehemu isiyopimwa? Wakati huo huo serikali ipime maeneo mengi ili kuepuka usumbufu wa ujenzi kwa wanunuzi?
Nini kifanyike ili miji inayokuwa sasa ikae kwenye mpango mzuri tofauti na mwanzoni?
Nani wa kulaumiwa kwa mipango mibovu ya miji? Serikali kuu au za manispaa?