Ni nani walikuwa wasaliti katika kudai uhuru wa Tanganyika?

Machifu wengi sana walirubuniwa na wakoloni na kujipanga nao katikakuhadaa juhudi za kupigania uhuru.

Hiini moja ya sababu Nyerere aliamuakupiga marufuku uchifu,ingawa yeye alitokea familia ya kichifu.
Umenena! Hiyo tunaweza kuifananisha kwa mbali na wanaosema " naunga mkono juhudi" kwa kujitoa kundi moja kwenda jingine ndani ya nchi moja. Hulka ya Mwafrika ni kupenda ujiko wa kufanyiwa kazi na wengine na siyo kujiendeleza mwenyewe.
 
Hata Nyerere mwenyewe alishawahi kulitaja hili katikamoja ya hotuba zake.

Waingereza wanajulikana dunianzima kwa kutawalakwa mtindo wa "divide and rule", kwa kuwa hawakuweza kuwa kila pahali, waliteua watu wao wawasaidie kuwawakilisha.

Ndiyo maana hata watoto wa machifu walipendelewa kupata elimu kidogo, kwa imani kwamba watakuja kuwasaida Waingereza kutawala.

Kuna habari moja ya Zambia, huwa naikumbuka Waafrika wanapopigania ukabila. Kuna Chifu mmoja aliulizwa, wewe kabila lako asili yake ni nini? Ulipataje kuwa Chifu? Akajibu, kabila letu liliundwa na Wingereza. Kabla ya Waingereza kuja, hili kabila halikuwepo. Waingereza walikuja wakakuta mgogoro.Kumaliza mgogoro, wakatutawanya, nyinyi nendeni huku, na nyinyinendeni kule. Wakaunda kabila jipya,na kumteua Chifu mpya. Martin Meredith aliandika habarihii katika kitabu chake "The States of Africa".

Hata Nyerere kamanakumbuka vizuri, baba yake alipata kuwa Chifu baada ya mgogoro na watu kutomkubali Chifu aliyemtangulia. Dr. Molony katika kitabu chake "Nyerere: The Early Years" aliandika.
Wadhungu mpaka sasa hivi wanafanya hiyo tabia ya ku divide and rule, ndio Maana yanajifanya kutetea wapinzani uchwara wa nchi, Maana kama ni ukweli wana uchungu na nchi kwa nini wasifanye kama wachina?
Wadhungu ni kutaka kuuza silaha zao na wapate cheap labor nchini mwao kama milibya ilivyo turn up kuwa maslave baada ya kufanya irrational decision walahi!
Ehhh Mola wangu tuokoe na mijitu yenye tamaa kuu walahi!
 
Back
Top Bottom