Ni nani mwenye hati miliki ya jina la "Nyerere." | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nani mwenye hati miliki ya jina la "Nyerere."

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Mar 10, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mara kwa mara tumekuwa tukisikia kauli kutoka kwa baadhi ya watu na asasi mbali mbali hapa nchini zinazo ashiria kwamba ni wao tu wenye hati miliki ya jina la 'Nyerere." Itakumbukwa wakati wa uchagizi mkuu uliopita, mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara,ambaye ni mtoto wake marehemu Nyerere, alifunga safari kwenda wilaya fulani mkoani Mwanza, kwenda kumfunda shemeji yake aliyekuwa anagombea ubunge kwa tiketi ya CDM, kuacha mara moja kutumia jina la Nyerere, eti kwakuwa alikwisha achika. Na hivi leo kuna stori katika gazeti ya sirikali ya Habari Leo, inayomnukuu mmoja wawana familia akiwahasa CDM kuacha kupandia kwa mgongo wa Nyerere. Vile vile CCM na jumuiya zake imekuwa ikitoa kauli zinazo ashiria kwamba kwa maoni yake chama hicho kina hati miliki ya jina la Nyerere. Kwa maoni yangu Nyerere ni baba wa taifa la watanzania/ Tanganyika, hivyo wananchi wote katika ujumla wao ndiyo wenye hati miliki ya jina lake.
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :A S 13:

  Ni watanzania wote wenye uchungu na nchi hii........

  .Nyerere (kama Baba wa Taifa) is not just a family figure au ya CCM tu, ile ni figure ya kitaifa hasa kwa wale wenye uwezo, ujasiri na uthubutu wa kukemea kukengeuka kwa nchi yetu....ndio maana mkulu hamtambui kama Baba wa Taifa zaidi ya "Mzee"
   
 3. m

  mtimbwafs Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni sisi watanzania wote basi.
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Leo nimesikia tena chama kimoja kinasema eti vyama vya siasa visifanye kaburi la mwalimu ni mtaji wao, jamani tunaenda wapi? kaburi la mwalimu lini likawa mali ya mtu, chama au serikali? mahali alipolala baba wa taifa ni pa kila mtanzania wake kwa waume, vijana na watoto.

  Kweli imenisikitisha sana hii habari, hawa wenzetu sasa wanafika mbali mno kwa hili.
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bila kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa suala hili, kadri nchi yetu inavyoendelea kumeguka katika vipande vipande unaweza ukashutukia watu wanauana kwaajili ya jambo hilo. Tatizo lililopo hatuna mahali maalum palipotengwa kwaajili ya maziko ya viongozi wa kitaifa. Hivyo kwa huu mtindo wa kuzika viongozi hao mahali watokako, kwa kiasi fulani kunaifanya jamii ijenge hisia ya kuwa familia za viongozi hao, na wana ukoo, ndio wenye hati miliki yy viongozi hao. Hivi kuna ugumu gani kuandaa eneo maalum kwaajili ya maziko ya viongozi wa kitaifa! Bila ya kufanya hivyo hata gharama zenyewe za kulinda makaburi yao yaliyotapakaa nchi nzima utakuwa mzigo mkubwa.
   
Loading...