Ni nani kama Paul Sozigwa katika viongozi wa CCM walioko sasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nani kama Paul Sozigwa katika viongozi wa CCM walioko sasa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Mar 15, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu, sifa kuu inayompambanua mzee Sozigwa katika maisha yake yote ya siasa hapa alihubiri kile alichokiamini.

  Katika miaka ya sabini, akiwa mkugenzi wa Redio Tanzania, alianzisha kipindi redioni kilichojulikana kwa jina la; "Mikingamo" katika mojawapo ya vipindi vyake, alisema kuwa ubepali ulikuwa unyama. Na kweli, mzee Sozigwa hata baada ya kusambaratika kwa siasa ya ujamaa aliendelea kuishi kama mjamaa.

  Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 1990, akiwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM alikuja Bukoba kwa shughuli za kikazi; mh. Kimiti wakati huo akiwa mkuu wa mkoa (k) alimtumia gari ya kwenda kumpokea melini; dereva alipomtafuta katika vyumba vyote vya daraja la kwanza hasimpate akarudi na kuripoti kwa bosi wake kuwa mzee hakuja; kumbe yeye alikuwa amekuja kwenye daraja ya tatu. Baadaye alimpigia mh. Kimiti kumjulisha kuwa alikuwa tayari amewasili na amefikia coffee Tree Inn.

  Baadaye wakati tukinywa chai pamoja yule dereva alikuja kuomba msamaha huku akijitetea kuwa alikuwa amepita kwenye vyumba vyote vya daraja la kwanza lakini hakumuona.

  Kitu alichomjibu mzee yule ni;"wewe nani alikwambia kuwa chama kina fedha za kupoteza kwa kusafirisha watu daraja la kwanza." Na aliyasema hayo miaka mingi baada ya azimio la Zanzibar kuiweka CCM katika njia ya ubepari.

  Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005, sekretariati ya CCM chini ya Philip Mangula iliazimia kuondoa mgombea yeyote atakakayebainika kutoa rushwa kwenye kinyanganyiro.

  Mzee Sozingwa akiwa anasimamia idara ya nidhamu katika sekretariati hiyo akalivalia njuga azimio hilo, Nakumbuka wakati rais wa sasa alipokuja Bukoba kusaka wadhamini, mzee Sozigwa alikuwepo akifuatilia nyendo zote zilizoashiria kuwepo kwa mazingira ya rushwa.

  Inasemekana wakati wa kujadili wagombea urais katika kamati kuu taarifa aliyokuwa ameiandaa ilitupwa kapuni, na hatimaye sekretarati yote ilifungiwa virago baada ya JK kuukwea wenyekiti wa CCM.

  Huyo ndiye Sozigwa, sijui maisha yake ya hivi sasa, lakini wengi tunamuheshimu kwa uzalendo wake na utumishi wake uliotukuka.
   
 2. tycoon

  tycoon JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 60
  Paul Sozigwa,great son of Tanzania!Mjamaa kwelikweli.
  Baada au baada ya rtd aliwahi kuwa mwandishi wa habari wa JKN
  Hp mnazikumbuka zile hotuba mahsusi za mwalimu hasa kipindi cha ukombozi wa bara letu.
  Nina hakika moja ya pendekezo lake kama mtu wa maadili ya ccm(ile ya kijamaa na kujitegemea)ni kutoa na kuelezea uovu wa mteule aliyekua ameshafanya maovu ya rushwa kule bukoba nk nk
  Ingekua ngumu sana kwa huyu bwana kupita 2005
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kati ya dhambi kubwa aliyoifanya JK na ambayo inakiua Chama chake ni hiyo hapo kwenye red.

  JK ni sawa na mtu anayekataa kula water melon (timu ya Mangula) na anaamua kula matango mwitu (Makamba, chiligati, mkuchika, etc)
   
 4. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kipindi cha mikingamo kilikuwa maarufu nakumbuka kipindi hiki kilianza mara tu Edward Sokoine alipoanzisha vita vya Wahujumu uchumi wakati watu wengi wakati huo walimwaga Sukari, Mafuta, Unga nk. ktk Bahari ili kukwepa kukamatwa na Polisi!!! hii ilikuwa ktk miaka ya 80 nakumbuka wakati huo niko chuoni Butimba Mwanza!

  Lakini cha kujiuliza hapa jee, Ndugu Komred Paul Sozigwa alikuwa akipanga foleni za mikate au Sukari na unga kipindi kile cha hali ngumu ya maisha au kipindi cha mgao wa vyakula kupitia RTC? kama na yeye alikuwa akiingia ktk mistari ya foleni ndefu ili kupata mlo wake na familia yake basi kweli yeye ni mjama wa vitendo! lakini kinyume chake kupanda meli daraja la 3 sio picha kamili ya Makomredi wa Siasa ya Ujamaa na kujitegemea!!!!
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  nani kwakwambia..huyo katumwa kuleta ushabiki..mzee alichota alichoweza alishindwa kula kile kinachotakiwa kuvutwa na wengi aka ufisadi ama kwa uwoga nk..lakini kula amekula kama kawa..asikwambie mtu bana kula walianza zamani..wengine wanafakamia makombo nw
   
 6. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee Paul Sozigwa, alikwisha fariki kitambo kidogo sasa (RIP) ila ni kweli alikuwa Mjamaa wa Kweli Kweli! believe it or not!

  Kwasasa ndani ya Chama (ccm) sijui kama bado wapo wa aina ya Marehemu Paul Sozigwa!
   
 7. V

  Victim Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Am so glad to read and note that there are people still alive today that can recall this great nationalist. Has anyone written an obituary of this wonderful Tanzanian,the likes of who we shall never see again.
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  That fellow (RIP) mimi alikuwa anikera sana na "Ujamaa wa Nyerere"! Mazungumzo baada ya habari zilikuwa ni "propaganda za sumu" zilizowafanya Wazee wetu "kubweteka"..
   
 9. m

  mjengwa-halifa Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hii habari wewe umesikia wapi? una huakika na unachokisema?
  Mzee Sozigwa yupo hai wala hajafa.
   
 10. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli mzee huyu alikwishafariki na kuzikwa kimya kimya itakia kuwa doa kubwa kwa uongozi wa sasa wa CCM. Katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia viongozi wakuu wakitumia raslimali za taifa kwaajili ya kuhudhuria mazishi ya viongozi wa CCM ambao hata mchango wao kwa taifa ni wa mashaka; iweje shujaa huyo azikwe kimya kimya!

  Naomba mwenye taarifa kamili athibishe habari hii ya kusitikisha.
   
 11. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Nina wasiwasi na maelezo yako haya ni ya kusimuliwa. Kwani nafikiri huyu Mzee alifariki kabla ya Mafisadi hawa kuanza mbio za kusaka urasi kwa kutumia mitandao.

   
 12. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Paul Sozigwa aliondolea kwenye Sekreterieti ya CCM enzi za Mwinyi kutokana na "KUPAUKA KIITIKADI".
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mie mwenyewe nimeshtuka maana cjawahi ckia habari za kifo cha huyu mzee.
  Kweli mzee hata mimi namfagilia
   
 14. C

  Coolhigh JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Mzee Sozigwa yupo hai ila ameshastaafu siasa na uzee umemwingia lakini.
   
 15. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,362
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kafa lini? Acha uzushi andika vitu vya uhakika, hasa jambo la uhahi wa kiongozi mstaafu aliyefuata maadili ya uongozi wakati wake.

  Huyu mzee alikuwa na uzalendo wa mwalimu Julius. Hakuwa na makuu, aliweza kupanda dala dala hali ikiruhusu etc.

  JK anawafahamu hasa hawa viongozi, na alifahamu afanye nini pindi atakaposhika hatamu za uenyekiti wa CCM. Kwa kifupi CCM imewatupa mkono waasisi wote waliokuwa waadilifu wakati wa mwalimu Julius.

  Tusubiri 25years to come wakina makamba CCM itawakumbuka vipi
   
 16. C

  Coolhigh JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Inawezekana mwandishi wa hili alitaka kumaanisha "kufa kisiasa", which is true maana hasikiki tena!!:embarassed2:
   
 17. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,540
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Huyu ndiyo Camarade Paul Sozigwa ktk clip hii:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mbona mimi sijabweteka?
   
 19. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  COMREDS PAUL SOZIGWA NA KINGUNGE NGOMBALE MWIRU ni Vigogo 2 niliokuwa nikidhani ni WAKOMUNISTI lakini hafla hiyo aliyohudhuria COMRED P:SOZIGWA imenithibitishia kuwa kumbe alikuwa muumin mzuri wa Kanisa ila alipokuwa madarakani alikuwa hana dini!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Watu wa aina ya Sozigwa ni wachache mno au hawapo kabisa serikalini kwa siku hizi.
   
Loading...