Tangu sakata la Jerry Muro liibuke mjadala umeelekea kwenye ' nadharia ya njama'.
Jeshi la Polisi ndilo linaloonekana kutupiwa lawama zaidi. Nahofia hatulitendei haki. Mimi najaribu kuvaa ' miwani ya giza'. Nina kiu ya kutaka kujua ukweli mzima wa sakata hili. Maana kuna wenye kuujua ukweli mzima, na ukweli ni mzigo mzito. Haubebwi na mtu mmoja, husambazwa, watu wakafahamu. Bila shaka tuko wengi wenye kiu hii. Na huu si wakati wa kutoa hukumu ' kishabiki'. Tuache sheria ichukue mkondo wake.
Na kuhusu Jerry Muro. Binafsi nimebahatika kukutana na hata kufanya kazi na wanahabari wengi wa Tanzania. Nasikitika sijapata kukutana na Jerry Muro. Nimemfahamu Jerry Muro kupitia runinga tu, haijapita zaidi ya miaka miwili tangu nianze kusikia jina lake na kumwona kwenye televisheni. Kuna mliosoma naye, kuna mliefanya kazi naye. Na mtusaidie kumwelezea Jerry Muro ili nasi tumfahamu alikotokea, tujue hapo alipo sasa, na itusaidie kupata picha ya wapi anakokwenda.