NI nani huyu anayepandikiza chuki dhidi ya serikali?

Mi kwa muono wangu mdogo nadhani tatizo ni la Mkuu wa Nchi kuwafungua macho na kuwacha uhuru wa kila mjinga na mwwerevu kusema ovyo hadharani kama vichaa. leo imefikia watu wana uhuru wa kutapika maneno yeyote bila haya na adabu na wala kufikiria nini matokeo ya maneno yake baadae. Mkuu wetu ndiye aliyewaachia uhuru watu. Sijaona uhuru huu wa kuropoka kote duniani ila hapa kwetu Tz.
 
Kuna chuki imepandikizwa dhidi ya serikali yetu; chuki ambayo inawafanya watu wawe na hamu ya kuona serikali iliyoko madarrakani inaangushwa au kuanguka (collapse). Chuki hii inawafanya baadhi ya watu kufanya kila wawezalo kufichua uozo na uovu mbalimbali serikalini. Ni chuki hii inayowafanya watu hata kuamua kubadili uanachama kutoka chama tawala kwenda vyama vingine. Ni chuki ambayo inaonekana kuzidi kukua na kuongezeka kila siku ijayo.

Swali langu ni NANI HASA (mwenye wajibu wa kwanza kabisa) ANAYESABABISHA AU KUPANDIKIZA CHUKI HII?

a. Waandishi wa habari
b. Vyama vya Upinzani (wanasiasa wa upinzani)
c. Wanaharakati wa kisiasa (political activists)
d. Mitandao ya Kijamii
e. Serikali yenyewe
f. Vyote hapo juu!

Lakini swali la msingi ni jinsi gani mhusika huyo anapandikiza chuki hiyo?


Tukijua ni nani anapandikiza chuki tutatarajia hatua dhidi yake....

Hakuna hata jibu moja hapo, chuki imejipandikizia yenyewe serikali kwa kukumbatia ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma, kutetea uovu na uzembe na kisha kuwadanganya wananchi kana kwamba ni watu wasio na akili za kufirkiri na kujiona wao tu watendaji ndio wenye uelewa na wenye uamzi wa Tanzania waitakayo siyo Tanzania tuitakayo sisi wananchi. Tumewachukia kwa kuwa wao wanatibiwa nje ya nchi sisi tukienda hospitali hakuna dawa tunaelekezwa kwenye maduka ya dawa ya watumishi wa umma, tumeichukia kwa kuwa shule za serikali zimekuwa hoi, hazina walimu na vifaa hasa watoto wetu wanaosoma shule za kata wanafanyishwa mitihani hata ya masomo ambayo hawajapata kufundishwa kwa miaka yote minne huku watoto wa viongozi wakisoma shule nzuri za binafsi au nje ya nji. Tumewachukia kwa vile ardhi yetu ikichukuliwa na wawekezaji bila sisi kushirikishwa na hata tukilipwa fidia ni kupitia sheria ya miaka ya zamani siyo inayoendana na bei ya soko la saa. Tunaichukia kwa sababu wao posho zao hazikosekani lakini pensheni ya baba yangu faili halionekani na waliopoteza faili hawashughulikiwi. Tunaichukia serikali kwa sababu karibia wabunge wote wa chama tawala wamepita kwa mizengwe ya rushwa na wakipewa uwaziri wanahujma rasilimali za wananchi waliowachagua. Naendelea kuichukia zaidi serikali kwa kuwatumia vibaraka km wewe uliyeandika hapo na kutudharau sana sisi wananchi kuwa hatuwezi kuichukia serikali kwa fikra zetu mpaka tu tuwasingizie waandishi, wapinzani, wanaharakati na mitandao ya jamii!
 
hivi ukipewa swali na majibu ukapewa uchague lakini ukagundua majibu yote uliyopewa hakuna hata moja sahihi, je utafanya nini?
 
Mi kwa muono wangu mdogo nadhani tatizo ni la Mkuu wa Nchi kuwafungua macho na kuwacha uhuru wa kila mjinga na mwwerevu kusema ovyo hadharani kama vichaa. leo imefikia watu wana uhuru wa kutapika maneno yeyote bila haya na adabu na wala kufikiria nini matokeo ya maneno yake baadae. Mkuu wetu ndiye aliyewaachia uhuru watu. Sijaona uhuru huu wa kuropoka kote duniani ila hapa kwetu Tz.

Mmn! Ingekuwa hivyo then kusingekuwa na umuhimu wakuwa na msitu wa Tembo/Pande
 
MKUU Mwkjj SALUTE!
Kwa mtazamo wangu bila kumung'unya maneno ni:-
1. Serikali yenyewe - (JK kujaribu kufunika UFISADI mkubwa ulifanyika kipindi cha MKAPA, Rasilimali zetu kutonufaisha Watanzania, Itikadi ya CCM isiyojulikana! Serikali kushindwa kutoa huduma za kijamii kama;- AFYA, ELIMU, MAJI, USAFIRI NA USAFIRISHAJI, NISHATI, KUSHINDWA KUZUIA KUPANDA SANA KWA GHARAMA ZA MAISHA, MISHAHARA DUNI, GAP KUBWA SANA KATI YA MATAJIRI NA MASKINI, UONGOZI LEGELEGE HUSUSAN WAZIRI MKUU KTK KUSIMAMIA UENDESHAJI WA NCHI
2. Tume ya Uchaguzi - Walivuruga uchaguzi thanks ALLAH S.W.T Watanzania ni Wastaarabu sana, Dhulma hii inawatesa watawala kwani wanajua kuwa hawakupata ridhaa ya wananchi hivyo kupelekea kuongoza kimagumashi magumashi maslahi binafsi mbele zaidi. Wataendelea kupopolewa sana kwa mawe!
3. Shule za KATA - Elimu ya Uraia inaenea kwa kasi ya kutisha hadi kishumundu ndaniii
4. Mitandao ya Kijamii especially JF - Hapa ndo kisima cha habari then watu wanatumiana SMS na majadiliano hufuata vibarazani, pub na hata maofisini. JF wanatoa elimu nzito kwa makundi yote kuanzia wenye elimu ya ngumbaro mpaka PHD.... Nani kampa Zomba u-expert member? lol!!! only snag so far...
5.CHADEMA - Hawa Jamaa wameshinda mawimbi ya kila aina wanayopelekewa na TISS ya CCM na MAFISADI... Wanaendelea kuanika kila uozo unaofanyika ndani ya Serikali
6. Wanaharakati na Vyombo vya habari - KUDOS kila mtu anajua kazi nzuri za wanaharakati na baadhi ya vyombo vya habari ukiondoa UHUNI ya CCM, HABARI JUZI, DAILY POROJO na TBC
7. Makada wa CCM kama NAPE, MWIGULU, LUSINDE, CHENGE, SITA, MKAMA... Wanasaidia kua CCM kwa spidi ya mwanga
8. WEZI WALOWEZI aka WAWEKEZAJI - Wengi wataendelea kupoteza uhai...hawa jamaa wanalindwa kwa gharama yoyote ile! enzi zile za KAPUYA aliwaambia wawekezaji wasiwalipe watanzania rate za kimataifa kwani serikali itakosa watumishi!!!!??? grrrrrrrr Mkuu naomba niishie hapo kwanza......
 
Elimu butu ya shule za kata imechangia sana kuwaamsha waliokuwa wamelala! Hongera serikali ya ccm kutuanzishia hizi shule ambazo sasa zimekuwa mwiba kwenu!! Huko vijana wanajifunza kuichukia ccm na seikali yake!!

Kupitia shule za kata, vijana wamegundua kuwa ccm imewatapeli kwa muda mrefu!! Tusitafute mchawi, kiini cha hasira na chuki kwa serikali ni elimu ya uraia kupitia shule za kata!
 
Kuna chuki imepandikizwa dhidi ya serikali yetu; chuki ambayo inawafanya watu wawe na hamu ya kuona serikali iliyoko madarrakani inaangushwa au kuanguka (collapse). Chuki hii inawafanya baadhi ya watu kufanya kila wawezalo kufichua uozo na uovu mbalimbali serikalini. Ni chuki hii inayowafanya watu hata kuamua kubadili uanachama kutoka chama tawala kwenda vyama vingine. Ni chuki ambayo inaonekana kuzidi kukua na kuongezeka kila siku ijayo.

Swali langu ni NANI HASA (mwenye wajibu wa kwanza kabisa) ANAYESABABISHA AU KUPANDIKIZA CHUKI HII?

a. Waandishi wa habari
b. Vyama vya Upinzani (wanasiasa wa upinzani)
c. Wanaharakati wa kisiasa (political activists)
d. Mitandao ya Kijamii
e. Serikali yenyewe
f. Vyote hapo juu!

Lakini swali la msingi ni jinsi gani mhusika huyo anapandikiza chuki hiyo?


Tukijua ni nani anapandikiza chuki tutatarajia hatua dhidi yake....
In a way wote hapo juu wanahusika. lakini chanzo ni serikali:
  1. wanaharakati wa aina zote wanatakiwa kuzungumza kwa niaba ya wananchi (hata kama wana ulterior motive);
  2. wana habari hawana uchaguzi isipokuwa kuandika habari bila kificho kwani wana wajibu wa kuwahabarisha wananchi (kwa bahati mbaya wanaweza kutumiwa vibaya na wanaharakati wa kisiasa na vyama vya siasa);
  3. vyama vya upinzani vinalazimika kuikosoa serikali day in day out, na wananchi wajue kuwa wanaikosoa serikali kwa niaba yao, ndiyo namna ya kukiondoa chama madarakani (nao ni binadamu wanaoweza kutumia vyombo vya habari vibaya);
  4. Mitandao ya kijamii inawafikia watu wa chache sana na si rahisi wawe na anafasi kubwa sana ya kuongeza chuki ya wananchi dhidi ya serikali
Mimi nasema serikali ikitimiza wajibu wake vizuri kwa faida ya wananchi kwa nini serikali isemwe vibaya na wote hapo juu? Wawridhishe wananchi kwa kuwakomalia mafisadi wa EPA, TZS 315 zilizofichwa uswisi, haki za waalimu, mapolisi, madaktari, madini yetu yanayosombwa kwa fujo kwa mrahaba wa 3% while 15% is possible. Serikali iliahidi maisha bora kwa kila mtanzania lakini kila uchao mambo yanazidi kuwa magumu. Wanaharakati, wanahabari, mitandao ya kijamii na vyama vya siasa visivyo madarakani vifanyeje?

nchi ni yetu wote wanaila wachache, tumechoka na tumechukia!

The government need to shape up vinginevyo chuki itaongezeka kila siku!
 
Ni wale wanaoona kabisa kuwa kuwa mfalme yuko uchi lakini kwa unafiki wao wanamsifia alivyojisetiri...kumbe anachekwa hadi na watoto wadogo anapopita barabarani na kuonekana kama chizi!

unanikoshagaje wewe. we haya tu.
 
1) Vyombo vya habari,kupitia waandishi wenye malengo hasi kama wewe
2) Chadema
3) viongozi wa kidini

ana makinda ilipoona mawaziri wa chama chake wanazidiwa na upinzani kwa kukosa hoja alisema NI UPEPO TU UTAPITA leo hii media zinaeleza hali halisi ashindwa kuitumia kauli yake na badala yake analalama hovyo kuvishutumu vyombo vya habari.
 
Mchawi namba moja ni serikali yenyewe kwa kuongoza kufanya madudu kisha wapinzani wakayaona na kuyanadi katika majukwaa ya siasa kisha vyombo vya habari vikaandika na habari zikasaambaa kwa wananchi baada ya kujua uozo unaofanywa na serikali yao na kisha kujenga chuki na serikali yao.

Nitakupa mfano Mzee Mwanakijiji wasanii wa Bongo Flavour wao ndiyo wanaotengeneza scandal kisha magazeti ya udaku yanaandika na sisi tunawaona hawafai kama akina Wema Sepetu n.k na serikali yetu imekaa kama wasanii hao.
 
Last edited by a moderator:
Kuna chuki imepandikizwa dhidi ya serikali yetu; chuki ambayo inawafanya watu wawe na hamu ya kuona serikali iliyoko madarrakani inaangushwa au kuanguka (collapse). Chuki hii inawafanya baadhi ya watu kufanya kila wawezalo kufichua uozo na uovu mbalimbali serikalini. Ni chuki hii inayowafanya watu hata kuamua kubadili uanachama kutoka chama tawala kwenda vyama vingine. Ni chuki ambayo inaonekana kuzidi kukua na kuongezeka kila siku ijayo.

Swali langu ni NANI HASA (mwenye wajibu wa kwanza kabisa) ANAYESABABISHA AU KUPANDIKIZA CHUKI HII?

a. Waandishi wa habari
b. Vyama vya Upinzani (wanasiasa wa upinzani)
c. Wanaharakati wa kisiasa (political activists)
d. Mitandao ya Kijamii
e. Serikali yenyewe
f. Vyote hapo juu!

Lakini swali la msingi ni jinsi gani mhusika huyo anapandikiza chuki hiyo?


Tukijua ni nani anapandikiza chuki tutatarajia hatua dhidi yake....

Mzee mwanakijiji, kasoro ni moja tu, serikali kama inayo, basi itakuwa imetengeneza na kutekeleza stratergy mbovu kabisa ya propaganda. Ncho nyingi duniani huwa na mpango huu ambao mara nyingi ni wa siri na unazungumzia hata vyanzo vya habari na jinsi ya kucontrol damage. Sioni kabis ahatua zinazohusiana na haya.Na nadhani kuna watu wameipotosha serikali kwa makusudi katika mkakati huo na kuifanya iamini, njia pekee ni kuendesha propaganda za CCM nba kuwakumbusha watu kuwa ni CCM inatawala, na kuwahadaa kuwa mazuri yote yanayofanya yanafanywa na CCM, na si watu wenyewe.atokeo yake chama kimokosa mvuto so na ypte wanayoongea hata yawe mazuri vipi, yanakosa mvuto. walichokosea ni kwamba, serikali ni ya watu wote kwakuwa wote wanalipa kodi ili ijiendeshe, si ya CCM! CCM ni platform tu ya kuiweka madarakani, na kosa hili la kipropaganda linashindwa kutenganisha uozo wa CCM na uozo wa serikali.
 
Mkuu Mwanakijiji swali lako ni zuri sana.

Jibu hapo ni (f) kwamba majibu yote ni sawa.

a. Waandishi wa habari

Waandishi wa habari mahili wa magazeti mahili yasiyo ya serikali kwa mfano Raia Mwema yana waandishi ambao waliona uozo wa kuandika habari za kuibeba serikali hata kama imeshindwa. Juzi tu magazeti ya serikali yalionyesha msimamo huo wa kuisaidia serikali na maovu yake.

Katika taarifa zake kuhusu kutekwa na kuteswa kwa kiongozi wa mgomo wa madaktari Stephen Ulimboka, kichwa cha habari cha gazeti ya Habari Leo kilikuwa kikisema kwamba " Kiongozi wa mgomo hoi".

b. Vyama vya Upinzani (wanasiasa wa upinzani)

It is not about monkeying around, kazi ya chama kiku cha upinzani (ambacho ni Chadema) ni kuikosoa serikali na kuonyesha mapungufu na kushindwa kwa serikali ya CCM kusimamia uchumi wa taifa na kufuata sera zake pamoja na manifesto ambapo mpaka sasa haieleweki manifesto ya CCM ni ipi.

Pia Chadema inasema kwamba kama wananchi watakipa ridhaa ya kuongoza nchi basi inaeleza sera zake na namna itakavyotekeleza sera hizo. Hivyo basi Chadema imekosoa serikali kwenye maeneo mengi tu yakiwemo matumizi mabaya ya fedha za umma ambao ni kodi inayolipwa na umma huo. Masuala ya mikataba mibovu isiyo kichwa wala miguu na sasa ambapo imegundulika kwamba serikali kupitia mawakala wake kama TBS walikuwa wakila fedha za umma.

c. Wanaharakati wa kisiasa (political activists)

Ukiondoa Christropha Mtikila hapajakuwepo na mwanaharakati makini ambae amekuwa akileta msisimko kwenye jamii ya watanzania na wakamuelewa ipasavyo isipokuwa dada yetu wa shirika la kutetea haki za binadamu. Ila bado hana nafasi nzuri ya kufanya kazi yake na muda si mrefu itabidi NGOs zote zipigwe marufuku kujishirikisha na local politics.

d. Mitandao ya Kijamii

Hapa sina la kusema kwani ndio hasa chachu ya majadiliano, upashanaji habari, iwe kwenye JF, Twitter na Facebook imekuwa ndio tegemeo pekee. Tumeshuhudia uozo mbalimbali ukianikwa hapa kuanzia EPA na masuala ya akina Jeetu Patel mpaka mkataba ya Buzwagi. Kwahio ni ule uelewa wa wananchi watanzania ndio utazaa chuki kwani wananchi watasema alaa kumbe mambo ndivyo yanavyokwenda! Ingawa mwisho wa siku ile arrogance ya wananchi inabaki palepale. kwamba ni CCM tu sio mwingine anaweza kushika na kuongoza nchi.

e. Serikali yenyewe

Hapa siwezi kusema kwani kila kukicha serikali inajipalilia makaa ya moto. Sasa ukiangalia mheshimiwa waziri mkuu Mizengo Pinda ambae amekuwa kijadiliana na madaktari akaja na kauli kwamba "liwalo na liwe" na baadae Dr Ulimboka akachukuliwa na yule bwana wa Ikulu na baadae kuishia kujeruhiwa vibaya ni wazi serikali inakosea sana katika kutafuta suluhisho.

Mwisho, serikali iamini kuwa wanaharakati wapo tokea kabla ya nchi yetu kupata uhuru na miaka 50 sasa baada ya uhuru wanaharakati wamekuwa ni wengi na wenye uelewa wa hali ya juu.

Serikali haiwezi kushindana na wanaharakati na ni lazima ijirekebishe na kuanza kujali maslahi ya wananchi wake kwa kuangalia maeneo muhimu kama Afya, Elimu, Ubunifu na Ujasirimali.

Sasa kuhusu kupandikiza ni kwamba kuna wanaopandikiza kwania njema kabisa kama waandishi na mitandao kwa kutumia njia ya mijadala bila kuleta matatizo.

Ila upandikizaji wa chuki unaofanywa na serikali ni mbaya sana kwa sababu pia serikali hujaribu kutengeneza dawa la kupalilia mapandikizi yake.
 
1) Vyombo vya habari,kupitia waandishi wenye malengo hasi kama wewe
2) Chadema
3) viongozi wa kidini

Ngoja niwafafanulie wananchi mkuu

1. Vyombo vya habari = Kwa kuonesha LIVE mikutano ya CHADEMA ambayo sehemu kubwa Dr.Slaa hutumia kuongelea madhambi ya serikali dhidi ya wananchi wake. Mfn. EPA, RICHMOND, KAGODA, MEREMETA na KIWIRA (Mkapanized)

2. CHADEMA = Kwa kuwaambia ukweli wananchi juu ya madudu na ufisadi wa serikali. Ni imani yangu, kama nisingejua juu ya EPA, RICHMOND, KAGODA, MEREMETA na KIWIRA (Mkapanized), nisingeichukia serikali. Ningeipenda kwa mujibu wa niyasomayo kwenye UHURU

3. Viongozi wa DINI = Hawa ndio hasaaa mwisho wa yote. Njoo chini hapa:
UAMSHO = Uamsho ndio wamewafungua macho Wazanzibari kuwa kukosa kwao misaada ya tende na halua pamoja na nyama za kondoo (Eid Alhaj) ni kutokana na kiburi cha serikali kukataa kuikabidhi Zanzibar kwa matajiri wa Saudia na Qatar.
ISSA PONDA na BASALLEH = Hawa wako bize kuikwamisha serikali katika juhudi zake za kuleta maendeleo. Hivi karibuni wametoa agizo wakiwataka watu wote waliogoma kutumia akili zao, wagomee na SENSA pia. Agizo hilo limeshazua balaa hata kwenye zoezi dogo linaloendelea mitaani linalofanywa na NIDA kusajili wakazi kwa ajili ya utoaji wa vitambulisho vya TAIFA. Baadhi ya wafuasi waaminifu wa PONDA wamegoma kujisajili.

NOTE: Kwa mujibu wa tunavyoamini sisi TUNAOAMINI akili ni ndevu, mtu yeyote akigoma kwa kudai maslahi basi huyu 'KATUMWA' na CHADEMA. Kinachotusumbua ni kujua hawa wanaogomea SENSA wametumwa na nani?

You are stupidly right sir!
 
Wenye ubongo mdogo kama wewe hujaribu kuelezea failures na mapungufu yao kwa kuwabebesha wengine responsibility au kusingizia historia kama ilivyo kwa nchi zetu za Afrika. Hatushangai kusikia ukitoa sababu za kushindwa kufanya kazi reli ya kati kuwa wajerumani hawakuijenga vizuri. Nyerere aliachia ngazi miaka 28 iliyopita na hayuko duniani 14 yrs bado unaota anaongoza nchi. unafikiri kinyumenyume mkuu. Rwanda wametoka kwenye genocide only 19 yrs lakini wanaondoka. Acha mawazo mgando we dont work for the past but present and future
mbona mkali suali si limejibiwa...historia ndio inaweza kuwa sababu ya matatizo yetu...kama akili haitaki kufunguka na mpaka leo tunasema enzi za nyerere basi yeye anaweza kuwa sababu kwani ameacha watu wasiofkiri , wasio tumia bongo zao...ila wanajaribu jaribu ingekuwa nyerere ingekuwaje...na hapa ndipo kwnye mgando wetu..
hatuwezi kwenda mbele kwa fikra za zamani na za mtu aliekuwa hayupo tena....yeye sio masihi...
ila kuhusu kikwetw na umaarufu wake ..inawezekana umeshuka lakini kwa sasa hakuna mbadala wake...
 
Ni mchango wangu huu naomba mnielewe, chuki iliokuwepo juu ya serikali ni kubwa sana sababu kubwa ni serikali yenyewe,
Tatizo: Tanzania ina watu waliogawanyika katika makundi mbalimbali kwa kutumia vigezo tofauti; makabila, mikoa, dini na vigezo vinine, Hebu tafakari matukio haya:-
1. The mwembechai killing
2. Zanziba and pemba 2005 killing and last month violent.
3.NECTA double result in islamic knowledge 2012
And these miner event which have raw data
i)number of workers in different government sector
ii)number of students in Advanced schools and universities
Hapa naongelea serikali(watendaji wa serikali) na dini
TANZANIA ya leo imekuwa na upendeleo mkubwa sana wa udini sidhani kama mnalifahamu hili, na ni dini moja tu ndio inapendelewa, UKRISTO.
Mfano:- matokeo ya somo la maarifa ya uislamu katika first draft hapakuwa hata na B moja lakini baada ya wakuu wa shule za kiislamu kufatilia hatimae na A pia zimepatikana,
Waziri anasema computer imekosea, nijuavyo mimi kanuni ya computer ni "gabage in gabage out" kwa maana unacho ingiza ndicho kinacho toka, na kwanini iwe kwa somo la maarifa ya uislamu
wasiwasi ulio kuepo ni kwmba uchakachuzi huu unafanyika hata kwa masomo mengine ili mkristo aonekane ndie alie faulu.
hiki kitendo kinaidhoofisha serikali.

JAMBO LINGINE:- Inapofikia nchi ina tatizo lolote basi utaona vyombo vyote vya habari vitaripoti mapadre na maaskofu kuchangia na kuamuru serikali, kwa maana serikali inaendeshwa na kanisa, na kauli yoyote ya kanisa lazima itimizwe, HILI NI TATIZO. Chukua hii; WAISLAM wamekua muda mrefu wakiiomba serikali wajiunge na OIC lakini viongozi wa kanisa wamepiga marufuku na serikali imebana mkia na imetimiza kauli ya kanisa kw kukataa, LAKINI Wakristo wamejiunga na vatican, LAKINI PIA SERIKALI IMESAINI MKATABA WA MEMORANDUM OF UNDERSTANDING NA WAKRISTO UNAO SEMA, ELIMU NA AFYA ZA WATANZANIA ZITAKUA MIKONONI MWA KANISA, WAO (KANISA) WATAANZISHA MASHULE NA HOSPITAL HARAFU SERIKALI ITATOA FEDHA ZA KUENDESHEA, LAKINI CHA KUSHANGAZA WANANCHI WANATOZWA FEDHA WAKATI SERIKALI IMESHA CHANGIA, HILI PIA NI TATIZO.
Serikali hii imewachosha wapenda haki. kama mi mi, sma RAISI sio mbaya watendaji wake wakina NDALICHAKO NDIO HAWAFAI WAMEKALIA MFUMO KRISTO.
 
Back
Top Bottom