Ni nani hasa alihusika na Kifo cha Sokoine?

Mimi nimependa sana habari hii ya kiuchunguzi tatizo la watu humu wanakosoa bila kuleta altenative nyingine ni bora uwe na constractive critisism badala ya ubishi
 
Acha blaa blaa! Unatakiwa kuuliza Kaka zako Mwinyi aliipokea Nchi hii ikiwa katika hatua ipi kiuchumi na Kijamii?

Hakuna Chakula ulichokuwa unaweza kununua bila ya kibali cha Mjumbe wa a Nyumba kumi ( Balozi)

Kila Sector ilikuwa Mbovu sana.

Mzee Ally Hassan Mwinyi aliweza kuvusha Taifa kutoka kwny Mfumo mmoja kwenda Mwingine bila ya Mtikisiko Mkubwa na hili ni Jambo kubwa sana sema tu lilifanywa na Mtu asieamini kwny Mbwembwe na misifa
Pamoja na madhaifu yake kwa sisi watu wazima tuliyoziona awamu zote 5 za serikali, hatutamsahau mzee Mwinyi na sera zake za TRADE LIBERALIZATION zilizopelekea mageuzi makubwa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hata nchi ikaona neema toka ktk hali tete ya kufunga mkanda baada ya vita vya Kagera. Hapa ndio watanzania wengi kwa mara ya kwanza tuliijua TV nakuanza kutumia colgete.
 
Nashauri mwenyw uzi huu pia pitia kitabu cha Mwl. Julius K. Nyerere cha Uongozi Wetu na Hatima Ya Tanzania utaona siri hizo Mwalimu yeye mwenyewe alivo ziweka hadharani. Pia soma kitabu cha Pan- Africanism or Pragmatism? Lesson of Tanganyika- Zanzibar Union cha Issa G. Shivji.

Ni sehemu gani alipoelezea hizo siri kwenye hiko kitabu mkuu?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Huyo wakati mwinyi Ana kuwa rais alikuwa hajazaliwa inaonekana amekuwa amekuta mwinyi kasharuhusu kila kitu hajapanga foleni RTC kununua sukari na dona
Duh we unanikumbusha mbali sana, hawa watoto wa smartphones watajulia wapi hayo uwaambiayo, watu walikuwa wanavaa viatu vilivyotengezwa kutokana na matairi ya gari.
 
Mara Nyingi Mimi Badala ya Kusoma Riwaya napenda sana Kutafuta habari za Masahibu yenye Utata ili angalau nipate clue ni nini kilitokea hasa.

Muda Mwingi Nimekuwa Nikitatizwa na Matukio ya Afrika ya Kuuana kwa Kugombania Madaraka. Nchini Kenya Miaka ya Nyuma, Kila ikikaribia Uchaguzi ambao Rais anayemaliza Muda wake hagombei tena Basi Kunatokea Mauaji ya Ajabu ajabu sana.

Kenyatta alipoashiria Uzee sana basi kulikuwa na Mauaji ya kutisha ya Kisiasa Kenya. Moi alipotangaza nia ya Kutogombea Tena Miaka y 90 hali Kadhalika. Kibaki alipomaliza Muda wake hali ikawa hiyo hiyo.

Nilidhani Tanzania hali ni Tofauti Lakini sivyo. Mwalimu Nyerere Tangu kumalizika kwa Vita vya Uganda, alishakuwa na Mpango wa Kujiuzulu Urais au Kutogombea Tena. Shadowy forces za Dunia zilishanusa Ni nani Nyerere alimpanga Kumrithi. Waliandika Katika Ripoti yao Maalumu, " Nyerere kwa kupenda Elimu na umahiri aliamua Kumpeleka Dokoine Yugoslavian ili akamalizie Masters yake na Pia ajifunze First hand jinsi Wayugoslavia walivyoendesha Ukomunist kwa Mafanikio.

Hawa walikuwa wakiweza kumvumilia Nyerere lakini walijua Sokoine wasingeweza Kudeal Naye kwani Misimamo yake haikuwa Balanced Kama Mwalimu. Wakamuua Sokoine, Nyerere alilia sana, Lakini hakuna aliyekuwa na Uhakika Ni kina nani hasa walihusika ingawa Sponsors Nyerere aliwajua. " Hawa walijigama Kwenye Chapisho lao moja wakati Fulani Kuwa kwenye Kila Serikali ya Mlengo wa Kushoto ie communist, nusu ya Wajendaji wa serikali, wana usalama nk wapo pia kwenye pay roll yao" Wakimaanisha Kuwa utakuta waziri wa Tanzani lakini Pia Kila Mwezi anavuta Mshahara kwenye coffers za Worlds strongest shadowy forces!

Kadhalika Katika Chapisho lingine walidai, Silaha yao Kubwa ilikuwa Ni kuchapisha Fedha Fake za nchi husika, wanawapa baadhi ya stooges wao,Wanazitumia Kunulia Bidhaa na kuzirundika kwenye Magodown ili zioze na zipotee kuwatia wananchi hasira juu ya regime! Kwa mwenye shaka na hili rejeeni miaka ya 80 jinsi Mwalimu Nyerere alivyokuwa akibadilisha fedha kwa ghafla. Na pia Rejeeni ni Nani alianzisha Vita dhidi ya wahujumu uchumi 1983-84 (Sokoine) Ikimbukwe Mhujumu uchumi sio Mlanguzi, Mlanguzi ananunua Bidhaa kwa lengo za Kuziuza kwa Bei ya faida Kubwa Mhujumu uchumi au Sabotage ananunua Bidhaa kuziharibu na Kuzipoteza ili aweke mazingira magumu ya kitawala nchi.

Sasa, Baada ya Sokoine Kufa Bado Kulikuwa na Vuta Nikuvute ya Kumpata Mrithi wa Nyerere, Mzozo ulikuwa kati ya awe Kawawa au awe Salim, Nyerere akamteua Mwinyi kama suluhisho. Lakini Pia sio hao wawili tu, Shadowy Forces zilikiwa na watu wao, na Mwishoni, wakati wa utawala wa Mwanzo wa Mwinyi Makicha yakaonekana Wazi. Katika Dossier ya Hawa Shadowy forces walionyesha Makundi Mawili Moja Lililolalia Upande waCommunism na Lingine Upande wa Soko huria, Ambao wasingemlenda Sokoine au yeyote anayependekezwa na Nyerere!

Kundi walillsema ni La Ki Socialist

1) Rashid Kawawa
2) Kingunge Ngombale Mwiru
3) Joseph Warioba
4) David Mwakawago
5) Joseph Butiku
7) David Msuguri
8) Kighoma Malima
9) Pius Msekwa
10) Charles Nyirabu


Kwenye Kundi walilodhani ni La Wingu la Mabadiliko waliwaweka

1) Ali H. Mwinyi
2) Salim A. Salim
3) Cleopa D. Msuya
4) Mustafa Nyang'anyi
5) Seif Sherif Hamad
6) Imran Kombe
7) Paul Bomani
8) Gilbet Rutihinda
9) Idris A. Wakil
10) Alnur Kassum


Katika hiyo Short List ya Shadowy Forces Jina Lililonishitua ni La Imran Kombe, Na Baadaye Nikaona Mahali ambapo Imran Kombe Rip. Amehusishwa moja kwa moja na Makundi yaliyojengeka Kinyang'anyiro cha Primary ya CCM 1995. Hapo ndipo hasa Makundi haya yalianza kusalitiana na Kuvurugana na Nadhani Ndipo Mboga na Ugali wa Uhujumu Uchumi na Kifo cha Sokoine 1983-84 Zikamwagwa! Kuna Madai kwamba Bodyguard wa Sokoine aliamriwa aende Monduli huku Sokoine akielekea Dar kwa Gari badala ya Ndege!

Kilichofikia Imran Kombe hasa Kunyanyuliwa Nafikiri ni 1996 Sijajua hasa Ni nini, Lakini Inawezekana Kulikuwa na Hofu Kubwa Mkapa kama mtu wa Karibu wa Nyerere angerudisha Usocialist, Katika Matoleo yao Pia walionekana Mahali wakisema (1986-87) Nyerere angeweza " Kumshinikiza Mwinyi aachie Ngazi, Ili Awaweke wengine, Wakaonyesha Short List ya Ambao Nyerere angewaweka Moja wao Badala ya Mwinyi Kuwa Ni,
1) Waziri Mkuu Joseph Warioba, au
2) Balozi wa Canada Benjamin Mkapa au
3) Salim au
4) Kingunge Ngombale Mwiru,
5) Rashid Kawawa.
Asante kwa kuelezea kidogo maana kifo chake kina utata sana yule dereva aliuehusika na kifo sijui yupo wap
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mwinyi Alikuwa Ni Mtu Mwenye Uwezo Mkubwa wa Administration, Lakini sio Kuongoza, Pia alikuwa ni Mtu Mwenye Roho njema sana na asiye na Makuu, Muugwana sana. Nyerere alipoachia Madaraka 1985 Alikuwa hana Uhakika Mambo yatakwendaje, Hivyo alimweka Mwinyi Kwa Kipindi cha Majaribio akijua wazi endapo yakizuka Matatizo Makubwa, as a result ya yeye, Nyerere, kuondoka, Basi Mwinyi asingeona Kinyongo kama ingemlazimu Nyerere Kumwambia aondoke, Kisha au Arudi yeye Mwenyewe Madarakani na Msimamo Mpya au Amweke Mwingine. Ikumbukwe huko Nyuma Nyerere alishafanya hivyo Kwa Kumwachia Kawawa Uwaziri Mkuu! Na Kisha akarudi tena. Hiyo sio Tathmini yangu bali ni Tathmini ya hao Warefu! Je Mnakumbuka Miaka ya 1994 Nyerere alisema wazi Kuwa Mwinyi hakuwa Chaguo Langu!
Mkuu unamaanisha nn kusem ana uwez mkubw kwenye adminstration bt co kwenye uongoz????
 
Bila shaka Tanzania ilipoteza dira rasmi tarehe 12/4/1984...Yote yaliobakia ni kujaribu kurudi kwenye mstari tu tena kwa kubabaisha tu....Waliomuua Sokoine ni weusi wanaotumika kama toilet paper na usishangae ndio waliotake over...Hakuna jambo ambalo naliona ni mistake kubwa kama kumuua Moringe tena kwa makusudi mazima ya kumkomesha.Great mistake.Alikuwa yeye na alijiamini na aliuamini ujamaa...Kama hatima mbaya isingemfika ama kwa hakika kungekuwepo na nchi moja ya mfano katika Africa.
 
Haya ma mtu ya usalama yamevurugwa, mnatoa toa siri. hahahahahahahahahhahaha
 
Mahali Fulani walisema, Iwapo Nyerere atakufa kwa Ugojwa au Kuuwawa, Ni most likely Viongozi wa Kiraia Akiwepo, Msuya, Malechela, Bomani, etc Wangeshindwa Kuchukua Nchi. Na kwa Njia Hiyo watakaoweza Kuchukua Madaraka watakua ni 1) Imran Kombe au Muhidin Kimario. Lakini walionyesha Kombe ndiye waliyemhusudisha sana hata Kuweka Picha yake kwenye andishi la riport hiyo.

File la Pili Uk. no 16

Wakasema sehemu Nyingine Pia, Iwapo "Successor wa Nyerere akaondoka Ghafla Kutoka Kwenye uwepo" Basi ambao wangeweza Kuingia Madarakani Bila kuingizwa kwa Ushawishi wa Nyerere ni 1) David Msuya 2)Paulo Bomani au Mkapa wangekuwa na Nafasi ya Kuchaguliwa.
File la kwanza Uk. No 10

Kwa aliefanikiwa kufungua hizo file msaada tafadhali kwa format nyingine kama word au pdf
 
Back
Top Bottom