Mimi nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu hii dhana ya Baba wa Taifa na hasa kwa nchi yetu ya Tanzania. Ninavyofahamu mimi mtu anayepewa heshima ya kuwa Baba wa Taifa ni yule muasisi wa mwanzo ambaye alifanikisha kuzaliwa kwa hilo Taifa lenyewe.Hapa kwetu Tanzania tunaambiwa kuwa Mwalimu Nyerere ndiye Baba wa Taifa (officially).
Mimi nimekuwa nikisita kidogo kukubali kumwita Nyerere Baba.Si kwa utovu wa adabu au ukorofi lakini naona haingii akilini kabisa.Naweza kukubali shingo upande kuwa ni Baba wa Taifa la Tanganyika(ambalo liliundwa baada ya uhuru wa 1961). Nasema shingo upande kwa sababu naelewa kuwa walikuwepo watu waliomtangulia kupigania uhuru wa Tanganyika ambao waliongoza mapambano kabla ya yeye hajatoka kijijini kwao na kuja Dar na baadae kukabidhiwa usukani. Nyerere hakuanzisha na wala hakuwa mwenyekiti wa mwanzo wa TAA.
Kwa upande wa Tanzania mimi nashindwa kunyanyua ulimi wangu kumwita Baba. Kwa kauli zake mwenyewe Nyerere ametamka mara nyingi kuwa alikuwa ni Karume ndiye aliyemfuata Dar-es-Salaam na kumshauri waungane.Hili Nyerere amelisema mara nyingi kila alipokuwa akisakamwa na Wazanzibari kuhusu mashaka ya Muungano. Sasa ikiwa ni Karume aliyekuja kumtaka Nyerere wafunge ndoa na nyerere akakubali, mbona leo tunaambiwa Nyerere ndiye baba?
Kwa mila na desturi zetu za kiafrika ni mume ndiye anayetoka kwenda kuposa mke na si vyenginevyo. Na kwa kauli za Nyerere mwenyewe, ni Karume ndiye aliyetoka kwenda kupeleka posa Dar na kwa bahati posa zikapokelewa na harusi ikafungwa haraka haraka na Taifa la Tanzania likazaliwa.
Kwa mtizamo wangu hapa naona karume ndiye mume (mposaji na muowaji) na mume ndiye kwa mila na desturi zetu huitwa BABA. Nitakubali ikiwa tutaambiwa Nyerere tumwite MAMA wa Taifa.
Dalali