Ni nani au mtu wa aina gani anayeruhusiwa kumiliki nyara za Serikali kisheria

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Sote tuna fahamu nyara za serikali ni nini, Je kuna sheria inayo mruhusu mtu yeyote yule kumiliki nyara za serikali? achilia mbali leseni ya uindaji ili uwinde wanyama, namaanisha upewe kibali uwamiliki mfano ndege kama TAUSI uwe nao nyumbani kwako uwafuge, sijawahi sikia popote pale kuwa kuna mtanzania anaye miliki ndege kama tausi, kama wapo wanao miliki kiholela na wanaishi nao sio kwa nia ya biashara nielewesheni nijue.

Juzi ma Rais wastaafu walipewa TAUSI, je hao tausi wanaweza wakapewa watanzania wa kawaida wasio na wadhfa au umiliki ili nao wawafuge, maana hata mimi natamani ila sijui utaratibu ukoje ili niwe nao, ni sheria ipi inafuatwa ili kummilikisha mtanzania yeyote yule au imeamliwa tu hivyo maana wao wako juu hawawezi kuhojiwa wala kuulizwa.
 
Back
Top Bottom