Ni nani ataibuka mshindi wa mchuano kati ya wahindi waliopo Dangote na Uhamiaji Mtwara?

masokolinda

New Member
Jan 10, 2016
2
0
NI NANI ATAIBUKA MSHINDI WA MCHUANO KATI YA WAHINDI WALIOPO DANGOTE NA UHAMIAJI MTWARA?



“Kuna Bwana mmoja mwenye Makengeza alikuwa na Kasuku wake. Na Kasuku huyo pia alikuwa na makengeza! Bwana huyo alikusudia kumuingiza Kasuku wake ndani ya tundu lakini kwa sababu ya makengeza yake akamuweka nje ya tundu akidhania amemuweka ndani. Naye Kasuku akaona hii ndiyo nafasi ya kukimbia, lakini kwa sababu ya makengeza yake, badala ya kukimbia nje na kutoweka zake, alipojaribu kuruka akaingia tunduni akidhani kuwa ametoroka”.


Mfano huu unawiana sawia na mpango unaendelea sasa kati ya baadhi ya maofisa wa idara ya uhamiaji na maofisa wa wizara ya kazi wakishilikiana na ofisi ya rasilimali watu YA DONGOTE ili kufanikisha upatikanaji wa vibali vya raia kutoka INDIA waliopo Mtwara. Na tuna imani na serikali ya awamu ya tano kwamba watakwaa kisiki.


Waswahili wanafahamu fika kuhusu jinsi gani pesa inaweza kutumika kutatua matatizo mbalimbali kama wasemavyo “penye udhia penyeza rupia” “penye amana weka rupia” hivyo juhudi kubwa inafanyika kuhakikisha wahindi wanaendelea kubaki DANGOTE hata kama hawakidhi vigezo vya kufanya kazi nchini.


Ifike wakati tuwe wazalendo wakweli, nasema hivyo kwasababu yanayojili dangote ni kutokana na tamaa za watu wachache wanaotumika kuwanyonya watanzania wanaofanya kazi katika kiwanda cha dangote. Tunajua wazi kuwa maslahi duni na unyanyasaji uliopo Dangote ni kwasababu ya wahindi.


Kuna swahiba wangu mmoja uwa napenda kumuita MZEE WA PWEZA aliwahi kunisimulia kuhusu kauli ya bw.Dangote (…BIG BOSS…..kama wahindi wanavyomuita) alisema “make sure these people are payed well” kauli hii uwa inanipa maswali mawili !!!! je BIG BOSS alimanisha walipwe kiwango wanacholipwa sasa ? ama walipwe zaidi ya hii wanayolipwa sasa ?!!!!! haya maswali yatajulikana muda ukifika…..yangu macho na masikio.


Jana nlibahatika kufika maeneo ya kiwanda na kukuta baadhi ya shughuli zikiendelea kama kawa, wakati nikijisogeza lango kuu la kuingilia, kutizama pembeni nikaona shimo la taka ikabidi nilisogelee, nilipokodoa ndani ya shimo nikakumbana na nakala yenye majina 41ya vigogo wa kihindi na wa Nigeria , na majina hayo sijui kama ndio yanakamilisha idadi ya wahindi waliopo DANGOTE au laa.


Jambo la kutia shaka ni vyeo walivyo jipachika na nina uhakika haviendani na taaluma zao (sifa). Nasema hivo nikiwa na uhakika na udhibisho utawekwa bayana pale wizara husika itakapofika kiwandani na kujionea (LIVE BILA CHENGA).


Nafasi zote nyeti wameshikilia wahindi na sitaki kukueleza juu ya idadi ya wachina na vyeo vyao. Tusubiri jipu litakapo tumbuliwa lakini ikumbukwe kuwa limeshakwiva wakichelewa linaweza kujitumbua lenyewe, watu wazima wamesha elewa.

upload_2016-1-11_22-27-16.png
 

Attachments

  • upload_2016-1-11_22-25-57.png
    upload_2016-1-11_22-25-57.png
    18.9 KB · Views: 46
Niliwahi pingana na mtu hapa kwamba idadi ya ajira inayopambwa na wanasihasa na media ni uongo waje mtwara washuhudie wenyewe kinachoendelea. Watanzania ni makuli tuu na watumwa wenyewe wanaigeria,wahindi na wachina ndio walioshika kazi zote za maana.
 
Kwa hiyo management mbongo ukipata kazi hapo lazima ukae
 
Last edited by a moderator:
Wanasiasa wanapamba kuwa kiwanda kimeajiri watanzania wengi kumbe foreigners wa bombay tena wasio na work permitt.....Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
 
Wahindi,Wachina aaaaargh
Any way labda kutakua na some changes ila kwa private sector bado kuna changamoto
 
Hivyo vyeo vyote kuna wasomi hapa nyumbani...tafadhali kila mtu achague kazi anayoiweza na wasifu wake atupe hapa jamvini tuuthibitishie ulimwengu na waziri husika na kamishna wake kwamba tupo ila tunabaaguliwa na hawa washenzi....
 
dah kweli hili si shamba la bibi bali ni shamba ambalo alina mwenyewe kwa maana hata bibi asingekubali upuuz huu
 
Back
Top Bottom