Ni nani anayesimamia gharama ya ziara za Lissu huko Ulaya na Marekani na anategemea faida gani?

Jibu swali gharama za Lisu huko Ulaya zinalipiwa na nani?

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
Maantiki ya kutaka kujua mlipaji wa gharama ni nini? Hujanionyesha kwamba TL mwenyewe hawezi kujigharamia so why nianze kutafuta mtu wa pili kama wa kwanza yaani mhusika hajathibitishwa kwamba hawezi kujigharamia? Pia ni kuwaza kimaskini kwamba kila msaada una masharti mabaya
 
Mwanasheria msomi nchini Tanzania ambaye alikuwa nje kwa matibabu baada ya shambulio la kupigwa na risasi ameanza ziara huko Ulaya na Marekani kwa madai kwamba anataka aieleze dunia tukio zima la yeye kushambuliwa na risasi. Na ziara hiyo imeshaanza tayari.

Sasa kwa mtu yoyote mwenye akili timamu ni lazima tu utahisi kwenye hii ziara ya Lisu huko Ulaya na Marekani kuna mtu nyuma yake anayesuka mipango na kuratibu mpango mzima.

Mtu huyu anayesimamia na kugharamikia ziara hii pengine na yeye atakuwa na malengo yake binafsi ambayo pengine sisi wapenda amani na maendeleo hatuyajui.

Sasa swali linabaki pale pale ni nani huyo anayegharamia ziara ya mtanzania mwenzetu Tundu Lisu?

Sambamba na hilo, je anategemea faida gani kutokana na sapot yake hiyo kutoka kwa Lisu?

Hivi hiyo ziara ya Lisu ina manufaa kwa nchi kweli au ina manufaa kwa lisu na watu wanaomsapoti?

Hivi ni nani wewe uliye nyuma ya ziara ya mtanzania mwenzetu?
Nazani ww utakuwa mtz wa kununua sio mualisia hata mwalimu jk alifanyiwa ukarim na duwa kubwa hawakutaka kingine wazee wetu ni ukombozi kwahiyo anaemsaidia lisu nimpenda haki ambae hata wewe ukipata matatizo kamayale haswa yakuonewa utasaidiwa mategemeo ya mfadhili hyu ni ukombozi wa Tanganyika na Zanzibar kuwa safi zenyewatu wenyekuhurumiana na kupendana hilo ndiofuraha na mategemeo kwake
 
Unashangaa gharama za ziara siku ya pili tuu, lakini hujashangaa gharama za matibabu yale ya zaidi ya siku 400. Ama kweli akili za kuku ni za kuku sio za bata
 
Hizi tabia kama ya huyu mtoa mada ikiachwa ndo tunazalisha mapunga mtaani!

Mbona hukuhoji ndugai kuzuia stahiki zake za matibabu
 
Unafanya kazi wizara ya mambo ya ndani hadi kujua kwamba jalada halijafunguliwa?

Je kwa nini dereva wa lissu hataki kutokea kueleza kilichojiri ili jalada lisonge mbele?

Kwa nini chadema mnatumia nguvu kubwa sana kumficha dereva wa lissu.?
Hadi mnaingia gharama ya kile mnachoita masomo yake ughaibuni.?

Yajayo yana nafuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanze na wewe kwanza, hebu rudisha camera ulizong'oa pale eneo la tukio.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Wewe unayekosa huruma kwa mtu aliyemiminiwa risasi zaidi ya 30 kweki utakuwa na huruma na nchi...!?

Endelea kula tu usidanganye watu... Ni muda wako.

Huruma gani ulitaka niwe nayo? Ulitaka nisimame kuzikinga risasi? Wewe na wenzako ndo mnaodanganya watu hapa kwamba mnampenda na kumjali Tundu Lisu klk hata Familia yake ambayo iko kimya na haijionyeshi, Btw ni lini ulienda kumtembelea Mbowe Gerezani kama ni kweli una huruma kama unavyojinasibu?
 
Mwanasheria msomi nchini Tanzania ambaye alikuwa nje kwa matibabu baada ya shambulio la kupigwa na risasi ameanza ziara huko Ulaya na Marekani kwa madai kwamba anataka aieleze dunia tukio zima la yeye kushambuliwa na risasi. Na ziara hiyo imeshaanza tayari.

Sasa kwa mtu yoyote mwenye akili timamu ni lazima tu utahisi kwenye hii ziara ya Lisu huko Ulaya na Marekani kuna mtu nyuma yake anayesuka mipango na kuratibu mpango mzima.

Mtu huyu anayesimamia na kugharamikia ziara hii pengine na yeye atakuwa na malengo yake binafsi ambayo pengine sisi wapenda amani na maendeleo hatuyajui.

Sasa swali linabaki pale pale ni nani huyo anayegharamia ziara ya mtanzania mwenzetu Tundu Lisu?

Sambamba na hilo, je anategemea faida gani kutokana na sapot yake hiyo kutoka kwa Lisu?

Hivi hiyo ziara ya Lisu ina manufaa kwa nchi kweli au ina manufaa kwa lisu na watu wanaomsapoti?

Hivi ni nani wewe uliye nyuma ya ziara ya mtanzania mwenzetu?

Kwani shida yako ni nini ?

Mambo ya mtu binafsi unayahoji ili iweje ndugu? Tan

Hivi kwa akili yako rafiki yangu unadhani ni jambo dogo mtu kunusurika kifo cha risasi za bunduki za kivita zaidi ya 40 halafu unyamaze tu kimya bila kuutangaza utukufu wa Mungu duniani kote?

Ni jambo kubwa sana aisee na kwa hilo tu ni muhimu mno kutembea dunia nzima kuutangaza ukuu wa Mungu!!

Shida ninayoona mimi ni moja.

Serikali inatuhumiwa kwenye jaribio la mauaji ya mtu huyu......

Serikali imesusia matibabu ya mtu huyu ambaye ni kiongozi wa umma (mbunge wa wananchi) kwa sababu inazojua yenyewe.....

Serikali haifanyi uchunguzi wowote wa tukio hili la kinyama kuwahi kutokea tangu uhuru wa Tanganyika 1961 kwa kiongozi (mbunge) kushambuliwa akiwa kwenye utekelezaji wa shughuli zake za kibunge mchana wa saa saba ndani ya eneo la makazi ya viongozi lenye ulinzi wa CCTV cameras na polisi masaa 24 kila siku ya wiki na mwaka mzima!!

Sasa walio serikali na wafuasi wa Chama kinachoongoza serikali (likely na wewe ukiwemo) wakiona mtu huyu anazunguka dunia nzima kuelezea scenario ya tukio zima huku akiituhumu serikali, wanahisi ni kuichafua serikali na ni kukosa huo mnaouita "uzalendo"...

Yaani nyie kuua watu (raia) wakosoaji wa serikali kwa risasi, kuteka watu na kuwapoteza kwa tafsiri yenu HUO NDIYO UZALENDO lakini mtu awaye yeyote mliyepania kumuua akinusurika kifo na yeye kwa nafsi yake kuuamua kuzunguka dunia nzima kutangaza SIFA na UTUKUFU wa Mungu wake, si mzalendo na kanunuliwa na mabeberu...!!

Aisee, if that's the case, mimi uzalendo wa kishetani wa namna hii hakika siutaki na sitaki hata kuusikia milele...!!!
 
Mwanasheria msomi nchini Tanzania ambaye alikuwa nje kwa matibabu baada ya shambulio la kupigwa na risasi ameanza ziara huko Ulaya na Marekani kwa madai kwamba anataka aieleze dunia tukio zima la yeye kushambuliwa na risasi. Na ziara hiyo imeshaanza tayari.

Sasa kwa mtu yoyote mwenye akili timamu ni lazima tu utahisi kwenye hii ziara ya Lisu huko Ulaya na Marekani kuna mtu nyuma yake anayesuka mipango na kuratibu mpango mzima.

Mtu huyu anayesimamia na kugharamikia ziara hii pengine na yeye atakuwa na malengo yake binafsi ambayo pengine sisi wapenda amani na maendeleo hatuyajui.

Sasa swali linabaki pale pale ni nani huyo anayegharamia ziara ya mtanzania mwenzetu Tundu Lisu?

Sambamba na hilo, je anategemea faida gani kutokana na sapot yake hiyo kutoka kwa Lisu?

Hivi hiyo ziara ya Lisu ina manufaa kwa nchi kweli au ina manufaa kwa lisu na watu wanaomsapoti?

Hivi ni nani wewe uliye nyuma ya ziara ya mtanzania mwenzetu?
Yaani mtu we mbunge kwa zaidi ya awamu mbili, awe mwanasheria tena wakili maarufu kwa miaka zaidi ya 10 na atibiwe nje ya nchi kwa mamia ya mamilioni akose pesa ya tiketi ya ndege na malipo ya hoteli ya siku chache?
Mawazo gani haya???
 
Kama isingelikua kupigwa risasi, haya yote usinge hoji mkuu. Tuanzie kwanza mwanzo wa tatizo

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Hela zetu za ruzuku ndiko zinakoishia, ndo maana wanapinga Mswada mpya, hawa jamaa chadema ni wezi na wala hawana huruma na hii nchi.
Kama serikali ilikataa kumtibu, sisi na wasamaria wema tuliamua kumchangia matibabu yake na tuliweka wazi. Na sasa tunaweka wazi zira zake na usiulize nia yetu. Kaa kimya kama ulivyokaa kimya baada ya kummiminia risasi na hujatuambia nani alikuwa nyuma ya shambulizi hilo na nia yake ilkuwa nini.
 
Back
Top Bottom