MISULI
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 7,826
- 5,451
Huwezi pata majibu zaidi ya matusi ya nguoni na kejeli.huruhusiwi kuhoji lolote lile kuhusu Lisu.Inachotakiwa we ni kuimba nyimbo za kumsifu lisu na matusi kwa jiwe. Kama unataka kueleweka Humu Anzisha uzi wa kumsifu Lisu au uzi wa kumtukana jiwe.Mwanasheria msomi nchini Tanzania ambaye alikuwa nje kwa matibabu baada ya shambulio la kupigwa na risasi ameanza ziara huko Ulaya na Marekani kwa madai kwamba anataka aieleze dunia tukio zima la yeye kushambuliwa na risasi. Na ziara hiyo imeshaanza tayari.
Sasa kwa mtu yoyote mwenye akili timamu ni lazima tu utahisi kwenye hii ziara ya Lisu huko Ulaya na Marekani kuna mtu nyuma yake anayesuka mipango na kuratibu mpango mzima.
Mtu huyu anayesimamia na kugharamikia ziara hii pengine na yeye atakuwa na malengo yake binafsi ambayo pengine sisi wapenda amani na maendeleo hatuyajui.
Sasa swali linabaki pale pale ni nani huyo anayegharamia ziara ya mtanzania mwenzetu Tundu Lisu?
Sambamba na hilo, je anategemea faida gani kutokana na sapot yake hiyo kutoka kwa Lisu?
Hivi hiyo ziara ya Lisu ina manufaa kwa nchi kweli au ina manufaa kwa lisu na watu wanaomsapoti?
Hivi ni nani wewe uliye nyuma ya ziara ya mtanzania mwenzetu?
Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu