Ni nani anayekosoa uongozi wa awamu ya tano?

mkolosai

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,575
2,000
wanajamvi, imekuwa kasumba kwa kila mtu au jamii fulani kushabikia mtu au jamii tofauti na upande aliopo. ni nadra sana kwa upinzani kushabikia chama tawala. Lakini tujiulize upinzani ni nini?
hili linakamilishwa na usemi unaosema kuwa "by nature, every human being is selfish" na pia mwamba ngoma huvutia kwake. ni nani anakosoa uongozi wa awamu ya tano?

Tanzania ni nchi inayotakiwa kuongozwa ili kuleta usawa kwa wananchi wote takribani milioni 50. kuna maneno yalisemwa kuwa rais hawezi kuwa mchaga wala mnyakyusa wala msukuma wala mhaya hiyo ilikuwa ni ubaguzi wenye mlengo wa ukabila, na ambao katu hatuwezi kuushabikia. ni nani anakosoa uongozi wa awamu ya tano?

Kuna wakati likazuka suala la kampeni kwa kutumia dini kuwa dhehebu fulani ichukue nchi, hilo pia hatuwezi kulichekea na kulivumilia.
Miaka ya nyuma kidogo walisikika baadhi ya wanasiasa na wananchi kuwa nchi inaongozwa kiupole walau ipate dictator au iongozwe na jeshi, lakini hilo pia haliwezi kukubaliwa katika nchi inayofuata misingi ya demokrasia na utawala bora. Leo hii tunaona kelele nyi gi katika utawala wa awamu ya tano ilihali hata chembe ya udictator haijaonekana. ni nani anakosoa uongozi wa awamu ya tano?

Ndugu zangu hivi kweli mimi maskini nisiyekuwa na uhakika wa mlo wa pili na nisiye na uwezo wa kupeleka mtoto shule nitawezaje kudiriki kuhoji kuwa eti kwanini fedha za bunge zimerudishwa ili zikatengeneze madawati. Mimi ninaetembea kwa miguu umbali mrefu kutafuta maji ya kuchemshia mhogo nakurudi mchana ili nikila nilale kusubiri kesho nawezaje kuhoji fedha zinazookolewa kwa kutumbuliwa baadhi ya watendaji ili zije zinichimbie visima karibu niweze kupata maji safi na salama niondokane na adha ya kufuata maji umbali mrefu? ni nani anakosoa uongozi wa awamu ya tano?

Naombeni msicheke kwa hili nitakalolisema, inasikitisha sana. Wakati wa matokeo ya uchaguzi wa wabunge mwaka jana, mbunge mmoja wa jimbo mojawapo la dsm matokeo yalikuwa na mkanganyiko hivo kuchelewa kutangazwa. ilikuwa patashika nguo kuchanika. alitokea geye na mama yake mzazi akasikika akisema " mnataka kuninyang'anya ubunge wakati ghorofa langu halijakamilika" kweli huyu ni mwakilishi wa wananchi jimboni kwake. ni nani anakosoa uongozi wa awamu ya tano?

Rais wetu ameonyesha mfano wa kuigwa kwa kuweka wazi kiwango cha mshahara wake anachopokea, pia amefanikiwa na kuweka rekodi ya kutosafiri nje ya nchi kama tulivyozoea huko nyuma ili tu abane matumizi na kuokoa fedha ambazo haziingii kwenye mifuko yake binafsi bali ni kwaajili ya kuleta maendeleo ya nchi ambayo hata mimi maskini nitayapata. Angekuwa anabana matumizi ya fedha ili akanunue magari binafsi au kutanua nchi za wengine ningehoji juu ya utawala huu wa awamu ya tano. lakini najiuliza ni nani anakosoa uongozi wa awamu ya tano?

Ninaomba kabla hujafanya lolote jiulize
wewe ni nani?
umetoka wapi?
upo wapi na
unaenda wapi?
ukishajijibu basi endelea kukosoa uongozi wa awamu ya tano. kwa yeyote ambaye uelewa wake ni mpana atajua kuwa mimi niliye maskini inanibidi nifuate maneno matamu ya yule ambaye anachochote ilimradi tu anauwezo wa kubadilisha mboga saba kwa mlo mmoja hivyo anaweza kunilaghai niweze kumtukana au kumkashifu rais wangu kwa kuwa naweza kulipa ama kulipiwa milion 7. Ninatambua Watanzania wengi sana wanahitaji uongozi wa awamu ya tano ili kuingia katika orodha ya watu wanaokula milo mitatu na pengine kuwa na kipato cha zaidi ya dola 2 kwa siku.
Mungu mbariki Magufuli
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika.
 

Gut

JF-Expert Member
Jan 18, 2016
2,836
2,000
Maskini mwenye smartphone kweli.Unaitwa maskini na unaitika.Kaa na umaskini wako mpaka kiama.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom