Ni nani anapaswa kuitwa mwizi kati ya Edward Lowassa vs Mizengo Pinda?

Jahlex

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
512
604
Habari wanaJF,
Kwa kawaida wizi ni wizi hata kama ni mdogo au mkubwa kiasi gani bali ikidhibitika kama kweli kuna dalili za kutokea tu au kutendeka kwa tukio zima la wizi huo wahusika wanapaswa kuchukua hatua kabla ya kusubiri kuchukuliwa hatua dhidi yao.
Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa wastaarabu wote ulimwenguni kwa maslahi mapana ya taifa na mtuhumiwa binafsi,
Katika historia ya nchi hii yanajirudia kwa mara nyingine tena yaleyale madudu yanayohusiana na ufisadi,wizi,uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi yasiyozingatia miiko ya kiutawala na kiuongozi.
Riwaya ya namna hii si ngeni kwa watanzania,miaka michache yalitokea ya RICHMOND ambayo yalisababisa anguko la serikali na wanasiasa waliotuhumiwa wakati huo akiwemo MH: EDWARD LOWASA na mara hii tunalo hili la IPTL-ESCROW ikiwa pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali MH: MIZENGO PINDA anahusika kwa namna moja au nyingine kwa mujibu wa majukumu yake kisheria na kikatiba.
Hoja yangu ya msingi si kuonesha madudu haya mawili yalivyotutia vidonda ambavyo itatuchukua muda kupona na kusahau isipokuwa ni kujaribu kuonesha ni namana gani serikali imechukua hatua kujitetea mbele ya Bunge.
1.Katika RICHMOND;
Waziri Mkuu wa wakati huo ndg. Lowasa licha tu ya kutohojiwa na kamati ya Bunge bali pia Serikali haikuandaa utetezi kama ilivyo sasa na hivyo kuamua kuachia kiti kama alivyofanya.
2.Serikali pia haikutumia nguvu kubwa ktk Richmond kuzuia mjadala usijadilike Bungeni tofauti na wakati huu wa ESCROW ambavyo watu binafsi na taasisi zimetumia kila mbinu kuzuia mjadala usijadiliwe.
Swali la kujiuliza kwa nini haikuwa wakati ule na kwa nini sasa?
Je mkuu wa nchi halijui hili au ikulu haihusiki moja kwa moja katika hili la ESROW A/C?
Na je vp kuhusu RICHMOND Ikulu haikuhusika?
Na kama haikuhusika mbona Mh; Lowasa mara kwa mara amenukuliwa akisema hakuna alilofanya ambalo Rais hakulijua?
Na kwa kuwa tulimwajibisha Mh:Lowasa kwanini huyu abaki salama ikiwa makosa yao yanakaribia kufanana?
Nguvu inayotumika na serikali kuwalinda hawa wanaotuhumiwa ni kubwa sana na inanipa mashaka,kuna nini cha zaidi hapa?
Kwanini viongozi hawa kwa uzembe wa majukumu yao mpaka kutufikisha hapa wanalindwa na kutetewa kwa nguvu zozte?
Mwisho kabisa naona dhahiri kuwa mh; Lowasa hakutendewa haki kama hali ilipaswa kuwa hivi na huenda Mh;mizengo asingekuwa kwenye kiti hiki na kama si hivyo basi tufanye kama tulivyofanya kipindi kile.
Nawasilisha.
 
Pinda Ndo mwizi katika siku chama cha mapinduzi imeniboa katika maisha yangu yote ni leo na ccm ndiyo wanafanya upinzani kupata nguvu
 
Tunazunguka mbuyu bure! Kinara wa uozo wote ni huyu kiumbe anaitwa JAKAYA. Wengine hao tunawaonea tu.
 
Pinda aondoke tu madarakani kwanza hana vigezo vya kuwa waziri mkuu yuko pale kama bendera tu anayumbishwa na watu wa chini yake
 
watanzania tunashangaa sana eti pinda na lowasa wanataka urais upiiiiiiii? kwa maana hawana sifa wakuu wa nch kwa ufisadi na uozo walionao.
 
Ukiona Mbunge anamtetea Pinda ujue keshapewa na yeye hela Yake Kwenye mfuko wa Rambo, yani naona Aibu kusema Pinda ni waziri Mkuu, Hana personality wala hujui responsibility Yake nini, ndio shida yakuchukua viongozi wasijijua Kwa kutaka kuficha maovu yenu sasa mmechukua wezi...
 
Mwizi mwingine ni babu slaa aliiba pesa za knisa za watoto yataima huyu hasa ndiye mwizi.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya ''Kamati teule ya Bunge'' na ''Kamati ya kudumu ya BUNGE''. Katika sakata hili la Escrow waliochunguza ni TAKUKURU na CAG, WAJIBU wa kuhoji watu na kufanya uchunguzi ulikuwa mikononi mwao. PAC ilikuwa na kazi ya kutafsiri ripoti na kuandika mapendekezo kwa Bunge.
Wakati wa Richmond ''Kamati teule'' ndio ilikuwa na wajibu wa kuhoji watu kwa namna ilivyoona, kamati hiyo ilitoa fursa kwa raia yeyote kutoa taarifa au kujieleza mbele ya kamati kama anaona anazo taarifa zenye kusaidia. Hamisi Kubenea ni mfano wa watz waliojitokeza kutoa taarifa juu ya sakata hili. Kwa maana hiyo MH, L OWASA hakuitumia fursa.
Mh, Lowasa alijiingiza moja kwa moja ktk suala la Richmond kwa kuingilia maamuzi ya nani apewe zabuni kinyume na taratibu.
Mh, Pinda anaingia kwenye Escrow kwa kunyamazia mchakato huu ambao haukuwa na afya kwa taifa. Hata kama hatumkubali MH, PINDA HATUWEZA KUHITIMISHA KWA KUSEMA NI MWIZI. Kama atawajibika basi atawajibika kwa dhana ya ''collective responsibility''.
 
ukweli ni kwamba lowassa ni mjanaja na mwizi, na pinda ni goigoi ila sio mwizi.
 
Mkuu hofu kubwa sana iliyoko kwa serikali ya Jakaya ni kuwa Lowassa atalipiza kisasi ... sasa wanajaribu kwa nguvu zote kuzima mjadala kwani wanajua kuwa itamjenga Zaidi Lowassa ....
Habari wanaJF,
Kwa kawaida wizi ni wizi hata kama ni mdogo au mkubwa kiasi gani bali ikidhibitika kama kweli kuna dalili za kutokea tu au kutendeka kwa tukio zima la wizi huo wahusika wanapaswa kuchukua hatua kabla ya kusubiri kuchukuliwa hatua dhidi yao.
Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa wastaarabu wote ulimwenguni kwa maslahi mapana ya taifa na mtuhumiwa binafsi,
Katika historia ya nchi hii yanajirudia kwa mara nyingine tena yaleyale madudu yanayohusiana na ufisadi,wizi,uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi yasiyozingatia miiko ya kiutawala na kiuongozi.
Riwaya ya namna hii si ngeni kwa watanzania,miaka michache yalitokea ya RICHMOND ambayo yalisababisa anguko la serikali na wanasiasa waliotuhumiwa wakati huo akiwemo MH: EDWARD LOWASA na mara hii tunalo hili la IPTL-ESCROW ikiwa pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali MH: MIZENGO PINDA anahusika kwa namna moja au nyingine kwa mujibu wa majukumu yake kisheria na kikatiba.
Hoja yangu ya msingi si kuonesha madudu haya mawili yalivyotutia vidonda ambavyo itatuchukua muda kupona na kusahau isipokuwa ni kujaribu kuonesha ni namana gani serikali imechukua hatua kujitetea mbele ya Bunge.
1.Katika RICHMOND;
Waziri Mkuu wa wakati huo ndg. Lowasa licha tu ya kutohojiwa na kamati ya Bunge bali pia Serikali haikuandaa utetezi kama ilivyo sasa na hivyo kuamua kuachia kiti kama alivyofanya.
2.Serikali pia haikutumia nguvu kubwa ktk Richmond kuzuia mjadala usijadilike Bungeni tofauti na wakati huu wa ESCROW ambavyo watu binafsi na taasisi zimetumia kila mbinu kuzuia mjadala usijadiliwe.
Swali la kujiuliza kwa nini haikuwa wakati ule na kwa nini sasa?
Je mkuu wa nchi halijui hili au ikulu haihusiki moja kwa moja katika hili la ESROW A/C?
Na je vp kuhusu RICHMOND Ikulu haikuhusika?
Na kama haikuhusika mbona Mh; Lowasa mara kwa mara amenukuliwa akisema hakuna alilofanya ambalo Rais hakulijua?
Na kwa kuwa tulimwajibisha Mh:Lowasa kwanini huyu abaki salama ikiwa makosa yao yanakaribia kufanana?
Nguvu inayotumika na serikali kuwalinda hawa wanaotuhumiwa ni kubwa sana na inanipa mashaka,kuna nini cha zaidi hapa?
Kwanini viongozi hawa kwa uzembe wa majukumu yao mpaka kutufikisha hapa wanalindwa na kutetewa kwa nguvu zozte?
Mwisho kabisa naona dhahiri kuwa mh; Lowasa hakutendewa haki kama hali ilipaswa kuwa hivi na huenda Mh;mizengo asingekuwa kwenye kiti hiki na kama si hivyo basi tufanye kama tulivyofanya kipindi kile.
Nawasilisha.
 
Nasikitika sana kuona vijana wa nchi hii ni mambumbu kabisa hawaelewi chochote isipokuwa ni ushabiki usiokuwa na maana. Sakata hili la escrow lina mikono ya wawekezaji wa umeme kama symbion ambao wanaiuzia umeme tanesco kwa sh 55 wakati iptl inauza kwa bei ndogo hivyo serikali inataka imuondoe symbion kwa sababu anauza umeme bei kubwa hivyo amemwaga fedha kwa baadhi ya wabunge ili wadai kuifilisi iptl.
 
Back
Top Bottom