Ni nani anapaswa kuitwa mwizi kati ya Edward Lowassa vs Mizengo Pinda?

Habari wanaJF,
Kwa kawaida wizi ni wizi hata kama ni mdogo au mkubwa kiasi gani bali ikidhibitika kama kweli kuna dalili za kutokea tu au kutendeka kwa tukio zima la wizi huo wahusika wanapaswa kuchukua hatua kabla ya kusubiri kuchukuliwa hatua dhidi yao.
Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa wastaarabu wote ulimwenguni kwa maslahi mapana ya taifa na mtuhumiwa binafsi,
Katika historia ya nchi hii yanajirudia kwa mara nyingine tena yaleyale madudu yanayohusiana na ufisadi,wizi,uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi yasiyozingatia miiko ya kiutawala na kiuongozi.
Riwaya ya namna hii si ngeni kwa watanzania,miaka michache yalitokea ya RICHMOND ambayo yalisababisa anguko la serikali na wanasiasa waliotuhumiwa wakati huo akiwemo MH: EDWARD LOWASA na mara hii tunalo hili la IPTL-ESCROW ikiwa pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali MH: MIZENGO PINDA anahusika kwa namna moja au nyingine kwa mujibu wa majukumu yake kisheria na kikatiba.
Hoja yangu ya msingi si kuonesha madudu haya mawili yalivyotutia vidonda ambavyo itatuchukua muda kupona na kusahau isipokuwa ni kujaribu kuonesha ni namana gani serikali imechukua hatua kujitetea mbele ya Bunge.
1.Katika RICHMOND;
Waziri Mkuu wa wakati huo ndg. Lowasa licha tu ya kutohojiwa na kamati ya Bunge bali pia Serikali haikuandaa utetezi kama ilivyo sasa na hivyo kuamua kuachia kiti kama alivyofanya.
2.Serikali pia haikutumia nguvu kubwa ktk Richmond kuzuia mjadala usijadilike Bungeni tofauti na wakati huu wa ESCROW ambavyo watu binafsi na taasisi zimetumia kila mbinu kuzuia mjadala usijadiliwe.
Swali la kujiuliza kwa nini haikuwa wakati ule na kwa nini sasa?
Je mkuu wa nchi halijui hili au ikulu haihusiki moja kwa moja katika hili la ESROW A/C?
Na je vp kuhusu RICHMOND Ikulu haikuhusika?
Na kama haikuhusika mbona Mh; Lowasa mara kwa mara amenukuliwa akisema hakuna alilofanya ambalo Rais hakulijua?
Na kwa kuwa tulimwajibisha Mh:Lowasa kwanini huyu abaki salama ikiwa makosa yao yanakaribia kufanana?
Nguvu inayotumika na serikali kuwalinda hawa wanaotuhumiwa ni kubwa sana na inanipa mashaka,kuna nini cha zaidi hapa?
Kwanini viongozi hawa kwa uzembe wa majukumu yao mpaka kutufikisha hapa wanalindwa na kutetewa kwa nguvu zozte?
Mwisho kabisa naona dhahiri kuwa mh; Lowasa hakutendewa haki kama hali ilipaswa kuwa hivi na huenda Mh;mizengo asingekuwa kwenye kiti hiki na kama si hivyo basi tufanye kama tulivyofanya kipindi kile.
Nawasilisha.

Hata watoto wanajua, Kuwa LOWASSA mwizi.
 
Back
Top Bottom