Ni nani anajali hatima ya tanzania?

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,991
1,194
Nani anaijali hatima ya Tanzania?Ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu makini kuweza kuishi. Ni nchi inayoshangaza sana, ingawa raia wake hawaonyeshi kushangazwa na matukio kadhaa yanayotokea.Naizungumzia Tanzania nchi niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu,magonjwa na kila aina ya shida ambayo mwanadamu wa kawaida anapitia, jawabu kubwa linapatika kwa swali; nani anajali?Ndio, nani anajali? Hili ni swali ambalo kila Mtanzania anapaswa kuulizwa.Ni kwa kiasi gani, mwananchi wa kawaida, kiongozi au muhusika yeyote wa nchi hiianajali matatizo ya nchi yetu.Nimejaribu kwa kiasi kikubwakutazama sura za viongozi wetu, mawaziri, wabunge, Wakurugenzi, Mameneja na kila kiongozi. Sioni anayejali.Wengi wanaongea wasichofikiria kukifanya kwa dhati na nchi imezidi kuoza. Akili zao ziko katika wizi kwa sababu na wananchi wenyewe wala viongozi wengine hawajali.Nchi inatafunwa kila jua linapochomoza na kuzama. Hakuna anayejali na kila mtu anaangalia maisha yake.Msukuma mkokoteni haoni ni kwa namna gani anahusika naWaziri mwizi wala Mkurugenzi wa Manispaa mla rushwa.Atajihusisha vipi? Kwa nini atumie muda wake mwingi kujali? Kama watuwanaomzunguka hawajali kula yakekwa nini na yeye awe anajali maisha ya wengine.Siwezi kusema nilifaidi matunda ya utawala wa Mwalimu Nyerere.Sijui mengi yaliyotokea wakatiwa Utawala wake, lakini tangu nilipopata akili timamu sijawahi kusikia Rais wa nchi yangu akimfukuza kazi Waziri wake kwa rushwa wala wizi.Je ni kweli kwamba marais wangu hawawaoni Mawaziri wezi na wala rushwa? Kama wangekuwawatiifu na waadilifu basi nchi yetu ingekuwa mbali. Lakini naamini wanawaona, kikubwa ni kwa vile hawajali kinachotokea.Hawajali kwa sababu hawana sababu ya kujali. Kwa kuwa wananchi hawajali basi na wao hawajali kama ambavyo wananchi hawajali. Wanaendelea kutojali na daima tunaendelea kupata vizazi vya Watanzania wasiojali.Kwani tukifungua mikataba ya ajabuya Madini hatuwaoni walioweka saini hizo? Tunawaona,lakini nani anajali?Nchi inasonga mbele na maisha yanaendelea.Huyu anajaribu kuandika gazetini kwa uchungu na yule anatamka lilekatika kipindi cha redio kwa uchungu, lakini nani anajali? Kina mama na watoto wanafungulia michezo ya maigizo ITV na kwingineko. Nani atawalaumu wakati watu makini wenyewe hawajali? Si afadhali nao wasijali!Kwani yuko wapi yule Waziri aliyesema yuko tayari kuona wananchi wanakula majani ili ndege ya Rais inunuliwe? Ndege ambayo ni mbovu!. Si amechaguliwa tena kuwa Waziri?Nani anajali kama Rais wa sasa hakujali? Mimi nitajali nini?Ni mwananchi gani anajali? Walio wengi wanafanya maaandamano katika mikasa ya kidini au ile ya kumpongeza Raisaliyefutiwa madeni ambayo fedha zake zilitumiwa kununua mashangingi.Kuna anayejali kwenda katika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya umeme? Kuna anayejali kuandamana baada ya kusikia Nesi amesababisha kichanga kufa sekunde chache baada ya mama mjamzito kujifungua?Hakuna anayejali kwa sababu hata akiandamana kwauchungu mkubwa, Rais hawezi kumwajibisha Waziri wa Afya!. Ndivyo nchi ilivyo na watu wengi wamekwenda jela baada ya kutoa taarifa njema kwa jeshi la Polisi.Lakini nani anajalikuwepo kwao jela? Ukitoa taarifakuhusiana na mkubwa fulani anayepokea rushwa, kesho yake Kamanda waPolisi wa Mkoa anakuonya na kukwambia uachane naye.Kwa nini niendelee kujali kwa watu ambao hawajali? Watu wangapi walishikwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es salaam lakini wapo nje kwa madai kwamba uchunguzi unaendelea?Uchunguzi upi wakati madawa yalitolewa tumboni na tukaonyeshwa katika taarifa za habari za Televisheni mbalimbali? Kwa nini niendelee kujali kuwepo nje kwa mtuhumiwa wakati Kamanda wa Polisi wa mkoa haonyeshi kujali?Yuko wapi dada machachari Mbunge wa kike aliyedai kwamba ana majina ya wauza madawa wa kulevya? Ni kweli kwamba alizungumza jambo jipya katikajamii yetu ya watuwasiojali?Tunao watu wengiwanaouza madawa na kwa bahati wanajulikana, lakini nani anajali?Dada yule ?alionyesha? kujali,lakini baada ya hapo nani amejali? Mbona hatujasikia mtu amekwenda ndanikutokana na mdomo wake?Tangu baada ya ?mauaji? ya basi ya Buffalo,magari yanazidi kwenda kasi barabarani. Nani anajali? Si mpaka watu wengine wafe ndio tusikie tamko jingine la kinafiki?Kuna melingapi mbovu paleZiwa Victoria na sehemu nyingine zenye vyombo vya usafiri wa majini? Kwa sababu hakuna anayekufa kwa sasa wahusika nawananchi hawajali mpaka litokee janga.Ili mradi asubuhi inafika, mchana unapita na jioni inawadia basi hakuna anayejali mpaka litokee janga. Nani anajali?Mchele mbovu unahalalishwa, watu wanatengeza majiya ?kufoji? na kuuza, nani anajali? Nikienda kusema Polisi wananitazama kwa jicho la chuki lakini tayari nimeshawaachia mianya ya rushwa.Keshokutwa nakutana na mkubwa wa Polisiniliyemshtua akiwa pamoja na mkuu wa Kiwandanilichokishtaki. Wanakula ?kitimoto? pamoja na wanacheka vilivyo, nani anajali?Kuna watuwachache walikiweka mikononi Chama cha soka nchini FAT,enzi hizo. Nani alijali? Kama si kuvurugana wenyewe kwa wenyewe wangeweza kuwepo mpaka leo.Ndio, Rais wa nchi alikuwepo, lakini hakuwa na muda wa kujali. Kipaza sauti kilikuwa kinamwambia asijali mambo hayo ila aelekeze macho katika Utandawazi.Ndio, utandawazi ambao unaruhusutupeleke makontena ya mchanga uliochanganyika na dhahabu nje yamipaka yetu. Nanianajali?Wachachewanajaribu kujali lakini nani anawasikia? Wenyewe wanakutana Golden Tulip wakila firigisi na kupeana ruhusa hizo. Mimi na wewe tujali nini wakati hatuna uhakika wa kesho?Tukipata watoto nao wanaingia katika mkumbo huo huo wa kutojali. Kizazi hikiambacho watoto wengi wamegeukia hisiaza kimagharibi ni yupi kati yao anaweza kujali?Wa kiume anakazania kusuka, wa kike anatamani kuvaa kama Beyonce. Hakuna hata mmoja mwenye hisia na nchi. Hawezi kujali kwa sababu hajafundishwa kujali.Ukisikiliza maoni ya wengi kuhusiana na kesiya Justine Kasusura, wengi wanamlaumu kwanini hakutoweka nje ya nchi. Hakuna anayesikitika kwa kitendo chake chakuiba fedha. Kwa nini?Watu hawajali alichokifanya. Yeye alifanya hadharani lakini kuna wanaoiba kwa karatasi? Hawa akina ?Kasusura? wa mezani nani anawazuia? Nani anawajali?Iko wapi Kampuni ya Richmond? Mbona kimya? Nani anajali? Kwa sasa umeme upo na watu hawajali tena. Wanataka ije?Richmond? nyingine ya Maji au huduma za Afya. Nani anajali?Ndio, sijawahi na wala sitaki kupiga kura. Yupo atakayesema napoteza haki yangu ya msingi. Simuoni wa kunijali na hata kama akiamua kunijali basi mfumo hauwezi kumsapoti anijali.Wakati wananchi wengine wakipigakura mimi naangalia vipindi vya soka katika Televisheni, kwa nini uniambie sijali wakati atakayechaguliwahatanijali?Katika kituo cha wapiga kura chenye wakazi 1000 lakini mshindi ameshinda kwa kura 1200, kwa nini nijali kusumbuka juani huku FFU wakinighasi wakati waliopanga matokeo hawaijalikura yangu?Nijali nini hasa kwa kutompigia kura mtu atakayekwenda bungeni kupitishasheria ya Takrima? Acha nifuatilie Ligi kuu ya England na utamu wake.Soma magazeti yetu ya leo. Watu wameamua kuandika mambo laini ambayo si sehemu ya mapambano yetu.Makala za leo ni zile zile zinazoelezea kwa undani Habari za Theolojia, Ulokole,na mambo mengine. Mwananchi asiye na uhakika na machweo ataelewa nini na kupata tumaini jema katika makala hizi? Wanaoziandika hawajali kinachotokea kwasasa.Kwetu, kiongozi kutajwa anamiliki hiki na kile kwa jina la mwanae, si kashfa. Kwetu, mtoto wa mkubwa au mkubwa mwenyewe kuua si jambo la ajabu sana. Nani anajali? Wao na Kamanda wa Polisi wanakutanaKilimanjaro Kempsky katika dhifa mbalimbali, unajua wanaongea nini? Kwa nini ujitie kimbelembele chakujali? Ili mradi unapumua, iangalie siku yako ya kesho.Tanzania ya leo imejaa watu wanaozijali familia zao.Nani atawalaumu watu hawa? Kwani viongozi wetu wanawajali kina nani? Si wanajali elimu za watoto wao pale Oxford, Havard na kwingineko?Kamaunabisha, mbona sasa hivi ndio wanatuongoza? Nani anajali? Tunauhakika gani kama baadaye wajukuu hawataongoza? Sindio wanapewa ukamanda wa vijana wakijiandaakumtawala mwanangu ambaye ni mnyonge wa baadaye? Nani anajali?Sina hasira na mtu.Nina furaha na maisha yangu kwa sababu napata ninachokitaka kwa uhalali. Kamamaisha
 
Dah hii kitu inaumiza kwa kweli......nimesoma mpk najisikia uchungu

Hakika umeongea kwa hisia kali kabisa yenye ukweli usiopingika.Ni nchi pekee ninadhani ambayo watu wake hawajali chochote kile ni bora kuna kucha na kuendelea na shughuli za kibinadamu haijalishi anamatatizo yoyote ili mladi kuna kauli moja rahisi sana na mwachia mungu au hata tukibadilishi uongozi ni walewale tu hivyo inampelekea kutokujali kabisa.Matukio mazito kabisa yaliyotikisa nchi kama Escrow lakini watanzania hawajali viongozi walewale wamewarudisha bungeni watanzania hawajali,wanatukanwa nakudhalilishwa hawajali wanatokea watu wakutaka kuwakwamua na unyonge walio nao watanzania hawajali kwa kweli inauma sana.
 
Mbaya zaidi ni vijana wetu.,ni nini tufanye tunusuru taifa?Tuishi kama kuku tuwaachie vibaka waendelee kupora? Nasema hapana ,tunoe bongo zetu...
 
Back
Top Bottom