Ni nani aliyeuharibu mfumo wetu wa elimu hadi tumefika hapa?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,783
Hebu jamani hivi kuna tofauti kubwa sana kati ya wazee wetu walioishia darasa la nane na hawa graduates wa leo wa chuo kikuu?

Graduates hawajui Kiingereza wala Kiswahili fasaha.

Uandishi wao na matamshi yao ni kichefuchefu.

Ufanisi kazini ni sawa na sifuri, hivi ni vipi mfumo wetu wa elimu umekuwa ukiharibika kila uchao? Nani mchawi wetu? Je, na kwa hili tuwasinguzie Wakenya na mabeberu?
 
Mfumo wetu wa elimu ni wa Kukariri kama kasuku!
Umejengwa katika mihemko ya kimadarka waliyojitwalia wanasiasa uchwara.Nadhani tuache kunung'unika juu ya ubovu wa elimu yetu Bali tuseme na kuleta mabadiliko ya mifumo ya elimu tuitakayo.

Tukisubiri hawa waliotuharibia mfumo wa elimu itolewayo hapa Tanzania tutaendelea kuwa walalamishi tusiokuwa na uwezo wa kufanya maamuzi.
 
Tatizo kiukweli lipo kwenye walimu, ukiachilia mbali miundo mbinu mibovu. Tuna walimu wachache Sana wenye uwezo wa kudeliver material Kwa ufasaha. Walimu wengi ni walio feli, anaenda kufundisha nini sasa wakat content ni zero, ni kwenda kufelisha wengine tu.

Na disaster kubwa Zaid inakuja mana walimu wale wazee wenye uwezo wa kufundisha darasa la chekechea mpaka la pili wanazid kuperish away, kuna hatari ya mtoto kuingia form one hajui hata kuandika au kusoma.
 
Ni kweli kabisa, yaani utakuta a graduate wa Mlimani hajuwi lugha yake Mama (Kiswahili), hapo hapo anaona sifa kuongea broken English wakati nayo pia hajuwi kuongea na hata kuandika.

Nashauri hawa wanafunzi wakamatwe na kurudishwa shule za vidudu tena wakichapwa viboko kwa kuwa wazembe, utajifanyaje kuwa hujuwi kuongea lugha yako Mama kama si ujinga?
 
Ni kweli kabisa, yaani utakuta a graduate wa Mlimani hajui lugha yake Mama (Kiswahili), hapo hapo anaona sifa kuongea broken English wakati nayo pia hajui kuongea na hata kuandika. Nashauri hawa wanafunzi wakamatwe na kurudishwa shule za vidudu tena wakichapwa viboko kwa kuwa wazembe, utajifanyaje kuwa hujuwi kuongea lugha yako Mama kama si ujinga?
🤣🙈
 
Balaa tupu,yani mtu mambo madogo tu yanamshinda mtu ni mhitimu kabisa wa chuo kikuu hajui hata tofauti ya kijiji na kata,hata shughuli kubwa nne za kiuchumi ktk nchi yake anakutajia kilimo tu pekee nyingine kama utalii,uvuvi,uchimbaji madini anakwambia kasahau,mhitimu hata kutumia kompyuta tena ktk kaz za kawaida tu hajui hata Microsoft word iko wapi kwenye kompyuta anasema haijui eti kasahau,mhitimu anamiliki smartphone lakini bado hata nchi zenye nguvu kiuchumi duniani hafahamu,mhitimu ukimuuliza nakupa wiki moja au wiki mbili za kuchagua wazo lolote la biashara unaloona linafaa anakuja anakwambia sijamaliza bado eti mtandao ulkuwa unasumbua sasa kumuuliza mtandao umekufelisha nn kwenye kazi uliyopewa anajibu nilitaka nitafute google hizo idea za biashara sasa ndo iwe wiki mbili zote hizo? ,mhitimu wa chuo kikuu anakimbia ofisi kwa kisingizio cha kwenda chooni baada ya kuja wageni wa kizungu anaogopa kutema yai anasaidiwa adi na Dada wa diploma kwenye kimombo,mhitimu wa chuo kikuu hata barua hajui kuandika vizuri....so saaaad
 
Kwa kweli mpaka naona aibu utadhani ndio mimi

Mtu amemalizaChuo ana kuja kuomba hapa jinsi ya kuandika cover letter

Yaani ukiangalia hizo walivyoandika CV mpaka unawaonea huruma

Sasa hata kama amekariri na amepata GPA kubwa, mwambie aandike technical report, hapo sasa ndio mauaji
 
Back
Top Bottom