Ni nani aliyetoa ng'ombe kwa vijana wa Mwanza kisha ng'ombe hao wakatolewa kama zawadi kwa Rais Samia?

Ushamba wako tu Unashangaa ng'ombe mbili kwenye mikoa kama Mwanza, Simiyu Shinyanga na geita au Mara?

Kule kijana wa miaka 16 kuwa na ng'ombe 5 ni kawaida.

Acha kushangaa
Mzee ilikuwa ni zamani saivi sidhani Kama Kuna mazingira mazuri hata ya ufugaji.
Binafsi huwa napiga Vita Sana ng'ombe ndugu hazina umuhimu wowote. Zinashikilia watoto hawasomi,
Wanaibiana na kuuana,
Zinaleta queries na nahitaji Mara wamekuja kula chakula shambani kwangu,
Yaani ni vurugu tupu,ukilala haulali unawaza wataibiwa,
Watu wanawekeza in modern economy nowdays.
Binafsi Nina uwezo wa kuwekeza kwa cows Ila environment not friendly.
Miaka ya 90 kurudi nyuma ilikuwa ni cows cows basi kichwani.
Hii nimetoa uzoefu kwa wilaya yangu ya Tarime hasa so sio lazima uzoefu huu utumike simiyu shy mza kagera chato n.k
 
wangempa ndama lakini gombe lishapea kama ilivyo CCM inaonyesha ni ujumbe umetumwa kuwa CCM mshazeeka kama hao ng'ombe kaeni pembeni mwapishe vijana.
 
Achana kabisa na lile jembe tena kaa mbali🤨
westbrookswag.png
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani akabidhiwa zawadi ya Ng'ombe dume na jike. Zawadi hiyo imetolewa na vijana wa mkoa wa Mwanza ikiwa ni shukrani kwake kwa kuendelea kusikiliza mahitaji ya vijana na kuyafanyia kazi.

Bado najiuliza kwanini tunafanya siasa kwenye mambo ya msingi?
Mzee naona ulisubiri karatasi ya mchango ili wakuchangishe halafu uje utupigie kelele humu. Pole Sana
 
Hivi huu ni mkutano gani wa vijana na rais wakati mpaka sasa hakuna kijana aliyeongea lolote.?
Huu ulikuwa Mikutano wa hadhara wa Rais kuwatambulisha wateule wake wa Mikoa ya Ziwa kwa vijana na kuwahutubia kuhusu mafanikio ya Serikali katika kuwaletea wananchi wa Kanda hiyo maendeleo. Hotuba hiyo ingeweza kutolewa Ikulu Dodoma au Dar na vijana Nchi nzimà wangepata fursa ya kumsikiliza maana nao wananufaika na mafanikio ya Serikali yake. Zawadi angepata siku nyingine!
 
U
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani akabidhiwa zawadi ya Ng'ombe dume na jike. Zawadi hiyo imetolewa na vijana wa mkoa wa Mwanza ikiwa ni shukrani kwake kwa kuendelea kusikiliza mahitaji ya vijana na kuyafanyia kazi.

Bado najiuliza kwanini tunafanya siasa kwenye mambo ya msingi?
Unataka kusema wale vijana unawafahamu, hawana uwezo wa kutoa zawadi kama hiyo?
 
Kule Mbeya Mtemi Isike alipewa Kuku na Mbuzi.
Ni mwendo wa kuiga Mbowe kapita wapi na sie tuende , Mbowe kapewa Mbuzi na sie tuonyeshe Ng’ombe. lakini ajira hakuna.

Nchi ya kikum* kum* sana hii.
 
Kwa mujibu wa sheria ya maadili zawadi yoyote inayofikia 200,000 inabidi ikabidhiwe kwenye mamlaka husika hivyo rais amepotoka au amepotoshwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom