Kifyatu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,382
3,196
Nasema "alitaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4, nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi, washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act).

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe.

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.


1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu.

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

J,e ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

==============================

Baada ya michango mingi iliyowekwa hapa kuna dhana niliyoigusia tu (Internal politics within CHADEMA) na wengi kuuliza kwa nini sikuifafanua. Hapa chini naiongeza ingawaje mwanzoni sikuipa kipaumbele.

Dhana ya 5.
Maadui wa ndani wa CHADEMA walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo;

1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa Uenyekiti.

2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea Urais ifikapo 2020.

3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CHADEMA mvuto na kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.
 
Last edited:
I will also go for no 2 ila kauli za mkulu dhidi ya TL zinaweza kuwa precipitating factor. Kunasehemu nimeandika kwamba very likely kuna kikundi kinachofanya huu uhalifu nje ya awareness ya serikali wakidhani wanasaidia serikali iliyopo. Kumbuka bomu ofisi za IMMA, bomu nyumbani kwa shehe, na pengine hata uvamiz clouds fm. Are they Tanzanians, Tanzanians + foreigners, imported foreigners? ??
 
Umetumwa kuja kuitetea serikali

Kwa ukumbusho tu...wakati wa mauaji ya Mwandishi Daud Mwangosi, msemaji wa Jeshi la Polisi alishawatuhumu Chadema kuhusika! Bahati mbaya kwao picha ikamuonesha polisi akimlipua huyo mwandishi na hivyo Chadema wakapona...isingekuwepo picha, hadi leo viongozi wa Chadema wangekuwa ama wanatumikia kifungo au wamepotezwa.
 
Back
Top Bottom