Ni nani aliyependekeza uteuzi wa Blandina Nyoni katika awamu hii ya Rais Magufuli?

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Hili ni swali muhimu sana na pia ni kipimo cha kujua kama mfumo umebadilika au la?

Tulishuhudia kelele nyingi humu JF,wizarani n.k juu ya utendaji mbovu na ama ufisadi na unadhirifu wa mama huyu hasa kuanzia miaka ya 2012.

Nikategemea kuwa mama huyu asingeweza kamwe kupewa fursa katika Serikali ya Magufuli lakini kwa mshangao akapewa Uwenyekiti wa bodi ya shirika la Nyumba.

Sisi wasema mbovu wa JF tukashshuliwa na mamlaka za uteuzi ...mafisadi yakachekelea huku wapinzani ambao walishajinajisi na ufisadi wakabaki kimya wasijue la kufanya.

Leo hii mama huyu katumbuliwa kabla hakujakucha vizuri ...tunashangilia sana ila kwa sisi wengine tunajiuliza swali muhimu sana kwani hatuna uhakika kama huu ndio mtumbuo wake wa mwisho au atapata fursa nyingine ya uteuzi ?

Je ni nani aliyempendekeza mama huyu kuteuliwa kipindi hiki cha Magufuli ilihali alishachafuka vilivyo hadi waziri mkuu Pinda akampiga chini?

Je ni nguvu ya Chama cha mapinduzi?

Je ni nguvu ya key players wa ufisadi nchini?

Nilimsikia mheshimiwa Rais akijiuliza kuwa inawezekana na yeye ajiangalie katika uteuzi kama anakuwa sahihi...mimi nashauri AANGALIE ZAIDI KWENYE UTEUZI WA ANAYEMPELEKEA MAPENDEKEZO YA UTEUZI!!
 
Jiongezeni,
Hiyo nafasi kuna mtu kanda ya Ziwa(Kabila sitaji) alikuwa masomoni ya shahada ya Udaktari illikuwa inamsubiri, Sasa amehitimi juzi huko Marekani na ndiye kaletwa sasa.

Thats all
Haya mambo hayajawahi kuisha na hayataisha , tuombe mwisho mwema tu , unless otherwise , kuna moshi unafukuta!
 
Jiongezeni,
Hiyo nafasi kuna mtu kanda ya Ziwa(Kabila sitaji) alikuwa masomoni ya shahada ya Udaktari illikuwa inamsubiri, Sasa amehitimi juzi huko Marekani na ndiye kaletwa sasa.

Thats all
Heee kwa hiyo kumbe mama Nyoni alikuwa kamshikia huyo aliyekuwa masomoni pale US. Dooh sasa mwenye nafasi yake karudi na ni mtu wa kanda ya ziwa mwenzetu..

Mama pishaaa..
 
Hili ni swali muhimu sana na pia ni kipimo cha kujua kama mfumo umebadilika au la?

Tulishuhudia kelele nyingi humu JF,wizarani n.k juu ya utendaji mbovu na ama ufisadi na unadhirifu wa mama huyu hasa kuanzia miaka ya 2012.

Nikategemea kuwa mama huyu asingeweza kamwe kupewa fursa katika Serikali ya Magufuli lakini kwa mshangao akapewa Uwenyekiti wa bodi ya shirika la Nyumba.

Sisi wasema mbovu wa JF tukashshuliwa na mamlaka za uteuzi ...mafisadi yakachekelea huku wapinzani ambao walishajinajisi na ufisadi wakabaki kimya wasijue la kufanya.

Leo hii mama huyu katumbuliwa kabla hakujakucha vizuri ...tunashangilia sana ila kwa sisi wengine tunajiuliza swali muhimu sana kwani hatuna uhakika kama huu ndio mtumbuo wake wa mwisho au atapata fursa nyingine ya uteuzi ?

Je ni nani aliyempendekeza mama huyu kuteuliwa kipindi hiki cha Magufuli ilihali alishachafuka vilivyo hadi waziri mkuu Pinda akampiga chini?

Je ni nguvu ya Chama cha mapinduzi?

Je ni nguvu ya key players wa ufisadi nchini?

Nilimsikia mheshimiwa Rais akijiuliza kuwa inawezekana na yeye ajiangalie katika uteuzi kama anakuwa sahihi...mimi nashauri AANGALIE ZAIDI KWENYE UTEUZI WA ANAYEMPELEKEA MAPENDEKEZO YA UTEUZI!!

hahahaha..Mkuu naona umeamua kula na huyu mama sahani moja since 2010!

Ila naona arobaini zake zimefika. Hakuna marefu yasiyo na mwisho.
 
Back
Top Bottom