Ni nani aliyemtuma mkenya kumteka Dr. Ulimboka?

Pambe S

Member
Oct 3, 2011
46
10
Kuna maswali mengi nyuma ya kiinimacho kilichotangazwa na kamanda Kova juu ya utekaji wa dr Ulimboka. kati ya mengi, Maswali yafuatayo yana wafanya Tanzania wasiamini taarifa ya jeshi la polisi juu ya utekaji na utesaji aliofanyiwa dr Ulimboka.
  • Kwamba mtekaji alienda kufanya toba kanisani haiingii akilini hata kidogo.Si rahisi kiasi hicho kwanza kanisa lipo kila mahali. Toba hiyo ingeweza kufanyika Kenya, Uganda na nchi nyingine bila hatari ya mtuhumiwa kukamatwa.
  • Kwamba mtekaji alitumwa na mtu asiyemfahamu tena anafanya kazi serikalini,serikali ipi ya Kenya au hii ya JK? Kwa hiyo Watanzania walikuwa sahihi kuituhumu serikali? Mbona waziri mkuu na Rais walikanusha kwa sauti kali tena ya kuapa? Haya mwajiri wa mtekaji anafanya idara ipi? Kama mwajiri na mwajiriwa hawafahamiani mshahara baada ya kazi ulilipwa vipi? Nani alishawahi kuajiriwa bila kufahamiana kwanza na mwajiri? Kujaza mkataba wa kazi?
  • Mbona katika hili taarifa ya polisi haikuonyesha picha ya mtuhumiwa? Mbona watuhumiwa wengine huonyeshwa picha zao pindi wanapokamatwa?
  • Kwa madhehebu mengi ya Kikristo, toba haifanywi kwa kwenda kuisema dhambi kwa mchungaji isipokuwa kanisa Katoliki,Je kanisa aliloenda mtekaji lina utaratibu huo wa toba?
  • Kwamba polisi imemnasa mtuhumiwa,kwa taarifa hiyo ndo mwisho wa uchunguzi wa chaini ya kiharifu iliyo nyuma ya tukio hili?
 
Kama anahusika kweli, atakuwa ametumwa na viongozi wa hapa hapa Bongo, halafu huyo Mwanasheria wa Kenya ninayesikia ameibuka akitaka huyu Mkenya akahukumiwe Kenya, asituzingue, kama ana husika kweli, huyu Mkenya tudeal naye hapahapa, tusimpeleke kwao, tudeal naya hapa hapa kama Waarabu wanavyodeal na watu wa madawa ya kulevya ndani ya nchi zao au kama China ilivyomnyonga yule Mmbongo kwa ishu za madawa ya kulevya mwaka huu, tusimwachie, kama kweli anahusika, tumuadhibu kweli, hili tukio la Ulimboka si dogo, unafikiri angekuwa na Mmbongo mwenzetu kamdhuru Mkenya mwenzao, ingekuwaje, wangemfanyaje?!, ngoja na sisi tumuonjeshe adhabu zetu, kama wao wanavyodeal na wabongo wahalifu huko kwao
 
Embu waonyeshe picha zake kwenye vyombo vya habari, si ajabu si Mkenya, wawezakuta ni Mmbongo wa hapahapa, watu wanamjua na ndugu zake!
 
Hakuna cha mkenya wala nini mchungaji wakanisa linalodaiwa kua huyo mtuhumiwa alienda kutubu anadai polisi imepotosha uma.kwakua mt huyo alfika nakuanza kupiga waumini ndipo walipoamua kuomba msaada polisi kwakua mtuhumiwa hakua na akili .kwa mantiki hiyo mkenya kabikiziwa kesi ili kutufumba macho watanzania.janja ya mr kova na baba yake saidi mwema tumeshaigundua.
 
Embu waonyeshe picha zake kwenye vyombo vya habari, si ajabu si Mkenya, wawezakuta ni Mmbongo wa hapahapa, watu wanamjua na ndugu zake!

Umeona eeh! Hawa Polisi magamba akili zao ni pungufu mno!!! Sasa wamejiingiza kwenye mtego wenyewe. Dr Ulimboka anamfahamu aliyemteka hivyo akionyeshwa hiyo picha ya huyo aliyebambikiwa hiyo kesi atakana kabisa huyo jamaa hakuhusika. Pia kama ulivyoandika inawezekana kabisa jamaa si Mkenya bali ni Mbongo hivyo picha yake ikianikwa hadharani nduguze wanaweza kumuona na hivyo usanii wa polisi magamba kuzidi kufichuka.
 
Hakuna cha mkenya wala nini mchungaji wakanisa linalodaiwa kua huyo mtuhumiwa alienda kutubu anadai polisi imepotosha uma.kwakua mt huyo alfika nakuanza kupiga waumini ndipo walipoamua kuomba msaada polisi kwakua mtuhumiwa hakua na akili .kwa mantiki hiyo mkenya kabikiziwa kesi ili kutufumba macho watanzania.janja ya mr kova na baba yake saidi mwema tumeshaigundua.

Bahati mbaya KOVA na TISS wameingia choo cha kike.
 
Kova watakudhalilisha kwa kukushinikiza useme uongo halafu ukicheza wanakukombe.
 
kuna maswali mengi nyuma ya kiinimacho kilichotangazwa na kamanda kova juu ya utekaji wa dr ulimboka. Kati ya mengi, maswali yafuatayo yana wafanya tanzania wasiamini taarifa ya jeshi la polisi juu ya utekaji na utesaji aliofanyiwa dr ulimboka.
  • kwamba mtekaji alienda kufanya toba kanisani haiingii akilini hata kidogo.si rahisi kiasi hicho kwanza kanisa lipo kila mahali. Toba hiyo ingeweza kufanyika kenya, uganda na nchi nyingine bila hatari ya mtuhumiwa kukamatwa.
  • kwamba mtekaji alitumwa na mtu asiyemfahamu tena anafanya kazi serikalini,serikali ipi ya kenya au hii ya jk? Kwa hiyo watanzania walikuwa sahihi kuituhumu serikali? Mbona waziri mkuu na rais walikanusha kwa sauti kali tena ya kuapa? Haya mwajiri wa mtekaji anafanya idara ipi? Kama mwajiri na mwajiriwa hawafahamiani mshahara baada ya kazi ulilipwa vipi? Nani alishawahi kuajiriwa bila kufahamiana kwanza na mwajiri? Kujaza mkataba wa kazi?
  • mbona katika hili taarifa ya polisi haikuonyesha picha ya mtuhumiwa? Mbona watuhumiwa wengine huonyeshwa picha zao pindi wanapokamatwa?
  • kwa madhehebu mengi ya kikristo, toba haifanywi kwa kwenda kuisema dhambi kwa mchungaji isipokuwa kanisa katoliki,je kanisa aliloenda mtekaji lina utaratibu huo wa toba?
  • kwamba polisi imemnasa mtuhumiwa,kwa taarifa hiyo ndo mwisho wa uchunguzi wa chaini ya kiharifu iliyo nyuma ya tukio hili?
una akili sana!!
 
Halafu, kwa uelewa wangu, ni Madhehebu ya Roman tu watu ndo wanaenda kufanya confession,
Kova na TISS wamejivua nguo
 
Dk Ulimboka asingeshindwa kuitambua lafudhi ya raia wa Kenya, Mbona hawa wanatufanya wajinga sisi Watanzania tuliowaajiri wao?
 
Huyu jamaa angeenda kenya kwenye kanisa katoliki then wangetuambia amekatwa akitubu ktk kanisa katoliki huko kenya yangefanana lkn haya mmh.... bora wangeomba ushauri hata kwa Inspekta MWALA
 
Umeona eeh! Hawa Polisi magamba akili zao ni pungufu mno!!! Sasa wamejiingiza kwenye mtego wenyewe. Dr Ulimboka anamfahamu aliyemteka hivyo akionyeshwa hiyo picha ya huyo aliyebambikiwa hiyo kesi atakana kabisa huyo jamaa hakuhusika. Pia kama ulivyoandika inawezekana kabisa jamaa si Mkenya bali ni Mbongo hivyo picha yake ikianikwa hadharani nduguze wanaweza kumuona na hivyo usanii wa polisi magamba kuzidi kufichuka.
BAK, wala hakuna haja ya kupigizana kelele hapa, hakuna Mkenya wala Mbongo. Kumbuka walisema huyu alikamatwa tarehe 29/6, tangu wakati huo walikuwa wanafanya nini kabla ya kutoa taarifa hiyo hadi wameitoa jana?

Tusubiri tu tuambiwe jambazi limetoroka gerezani. Kova na wenzake wametawaza kabla ya ku.nya, sasa wanajipaka nayo!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hawa jamaa wamelewa damu ya Dr. Ulimboka sasa mpaka akili zao zimeshazima kabisa maana hata babu yangu mbaye sasa hana jino hata moja hawezi kusuka deal la kishamba kama la Kova et all!
 
huwezi ukamhukumu mtu wakati shahidi mkuu yuko hospital, hivi leo hii ulimboka akisema kua huyo mtu sio mwenyewe aliyeshtakiwa itakuaje?
 
Huyu jamaa angeenda kenya kwenye kanisa katoliki then wangetuambia amekatwa akitubu ktk kanisa katoliki huko kenya yangefanana lkn haya mmh.... bora wangeomba ushauri hata kwa Inspekta MWALA

Mkuu vngenge naona unakafuatilia sana haka kamtu kafupi!

Suala la utekaji na uteswaji wa Dr. Ulimboka limetoka kuwa la uhuzunishaji sasa ni la uchekeshaji. Najiandaa kwenda kanisani kwa Gwajima huko Kawe nikasikilize ilikuwaje Mulundi akaenda kutubu huko kwa Gwajima. Gwajima naye mmhhhh. Najua TZ na KN wanabadilishana habari za kiintelijensia kuhusu wahalifu na uhalifu. Mulundi amewaambia kwamba kiongozi wao huko Kenya anaitwa Silencer na wamekuwa wakishiriki kwenye matukio mengi ya uhalifu. Hivyo basi hapana shaka kabisa TZ imewapasha wenzao wa KN kuhusu hilo kundi na kiongozi wao na bila shaka basi muda si muda Silencer naye atakamatwa huko Kenya kwa ushahidi/taarifa za Mulundi. Vinginevyo Mulundi si Mulundi!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom