Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,067
HIZI SI NGOME ZA KUHIFADHI WAFUNGWA, WALA SI MABANDA YA KUHIFADHI MIFUGO, BALI NI MASKULI YA WATU KUPATA ELIMU!
AMA KWA HAKIKA DUNIA IMETUWACHA MBALI MNO!
Picha mbili za mwanzo ni skuli yangu niliosoma hadi darasa la tatu. Wote ambao nilibahatika kuwa nao darasani, hakuna aliyefaulu kuendelea na masomo ya elimu ya juu. Na wengi miongoni mwao wamekuwa wakulima au wakwea minazi na tayari wamekata tamaa kuhusu elimu!
Nilibahatika kukutana na mmoja wa wanafunzi mwenzangu ambaye tuna bahati ya kutokea kijiji kimoja. Huyu amebahatika kuwa mpishi wa wanafunzi kwenye chuo kimoja cha kiisilamu hapa kisiwani Pemba. Si kazi ambayo kaisomea kama taaluma makhsusi bali kaipata kutokana na kuwa kwake kada wa Chama Cha Mapinduzi!
Hakika mazingira mazuri mahali pa kazi, huongeza morali na ufanisi wa kazi. Jee, kama shule inashindwa kutoa mwanafunzi ata mmoja kidato cha nne kuna nini?!
Nakumbuka nilipata bahati yakusoma kwenye maskuli mengine kadhaa nje ya kisiwa cha Pemba. Hakika mazingira yalikuwa tofauti mno na yalinivutia.
Ni miaka mingi kidogo imepita lakini bado kiwango cha ufaulu na kitaaluma kwenye shule hizo vimezidi kuongezeka tofauti sana na skuli yangu niliyo na asili nayo.
Nilijaribu kufanya juhudi kadhaa ikiwemo ile yakuandika na kuchapisha vitabu ili vigaiwe bure kwenye maskuli ya Pemba na Unguja. Hata hivyo imeshindikana kutokana na mzigo huu kunielemea pekeyangu kwa kukosa wafadhili!
Niseme kwamba nimelifanya hili kwa moyo safi na msukumo wa pamoja na mwenzangu Mohammed Ghassani pamoja na wengine kadhaa lakini imetuwia vigumu. Naamini kama tukishikamana, tunaweza tukabadilisha mazingira.
Binafsi nimejitolea vitabu vyangu viwili vichapishwe na kisha vigaiwe bure kwenye skuli za Unguja na Pemba. Gharama ya uchapishaji haitozidi 2500 kwa kitabu cha kurasa zaidi ya 80. Nilipata kuchapisha kijitabu kimoja wapo na madukani kiliuzwa shilingi 5000.
Natoa wito kwa wenye kuguswa kama mimi, anitafute inbox ili nimpe namba yangu ya mawasiliano kwa lengo la kuipeleka mbele Pemba na Unguja.
Nieleze kwamba kimoja ya vitabu hivi vilishaandikiwa ripoti na wizara ya elimu Zanzibar kwamba kinafaa kusomwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
Tushikamane kwa faida ya nchi yetu na ndugu zetu wa Pemba na Unguja.