Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

Hakika bajeti ina mapungufu fulani ya kiufundi,linapokuja suala la kumukwamua mlalahoi kutokana na bajeti hapa kuna tatizo la msingi maana mara nyingi Mtazamo wa serikali ni kuongeza mapato yake ya kila mwaka angalau kwa asilimia 6-10% kulingana na hali ya uchumi.

Tatizo kubwa nimefanya utafiti katika uandaaji wa bajeti na kugundua kimsingi unaanza October yaani miezi 2 baada ya kupitisha bajeti hii ni katika ngazi ya wilaya na December ngazi ya mkoa na April ngazi ya taifa. kwa mfano huu bajeti haiendani na hali halisi na mara nyingi kila hatua inachukua siku 21-28, watendaji wanaenda ku-copy na ku-paste kwa kuongeza 6-10% kwa ile ya awali.

Hata vyanzo vyetu vya mapato vimebadilika mno lakini haya hayapatikani kwenye bajeti yetu.

Napendekeza MODS waweke jukwaa la bajeti ili tupate muda wa kuchanganua na kutoa mawazo yetu katika kuboresha kama ilivyo ya katiba na chaguzi.
Bajeti ndo inatoa taswira halisi ya muelekeo wa uchumi wa nchi.
 
Rutashubanyuma. Its the time now we decide to make changes that shall redeem the theft of these politicians ..we have to decide for our own future..this is our country...

Rogi you are right it is the only country we can ever call home sweet home
 
Last edited by a moderator:
Hakika bajeti ina mapungufu fulani ya kiufundi,linapokuja suala la kumukwamua mlalahoi kutokana na bajeti hapa kuna tatizo la msingi maana mara nyingi Mtazamo wa serikali ni kuongeza mapato yake ya kila mwaka angalau kwa asilimia 6-10% kulingana na hali ya uchumi.

Tatizo kubwa nimefanya utafiti katika uandaaji wa bajeti na kugundua kimsingi unaanza October yaani miezi 2 baada ya kupitisha bajeti hii ni katika ngazi ya wilaya na December ngazi ya mkoa na April ngazi ya taifa. kwa mfano huu bajeti haiendani na hali halisi na mara nyingi kila hatua inachukua siku 21-28, watendaji wanaenda ku-copy na ku-paste kwa kuongeza 6-10% kwa ile ya awali.

Hata vyanzo vyetu vya mapato vimebadilika mno lakini haya hayapatikani kwenye bajeti yetu.

Napendekeza MODS waweke jukwaa la bajeti ili tupate muda wa kuchanganua na kutoa mawazo yetu katika kuboresha kama ilivyo ya katiba na chaguzi.
Bajeti ndo inatoa taswira halisi ya muelekeo wa uchumi wa nchi.
[MENTION]
peter tumaini[/MENTION] tatizo jingine hii bajeti inayoongelewa kwa vishindo siyo bajeti ambayo serikali inataka kuitekeleza.........................bajeti wanayoipenda wao itakuja Desemba na huiita mini bajeti na la ajabu hutumia khoja zako hizihizi katika kuhalalisha kupitishwa matumizi wayatakayo wao wenyewe
 
Hii ni nchi ya kufikirika ndugu zangu. Ila siku inakuja na kila mtu atajua nini ni nini hakuna atakayebaki waacheni watende yaliyo mioyoni mwao kwani siku watashangaa. uwezi kujinufaisha wewe na kuja hapa na Bajeti ya kutaka kututia moyo tu wakati tunaona mambo yana zidi kuharibika kwetu. WATANZANIA sasa tuseme basi inatosha
 
Dr. Mgimwa ni mradi wa Pinda na Makinda na binafsi sina tatizo na hilo maana what matters is the content.

Sijui Zitto atakuwa na mapendekezo gani kwenye alternative budget yake lakini kama atakuwa na mazuri basi ningeshauri wabunge wa CCM wamuunge mkono. Nasema hivyo kwa sababu hii budget ya Mgimwa itawaletea balaa. Kwa mfano anasema watakuza uchumi kutoka 6.4% to 6.8%. Tafsiri yake ni kwamba kwa miezi 12 watakuza uchumi kwa 0.4%! Shida kubwa hapa, kama wananachi hawaoni unafuu wa maisha under 6.4% ukikiza uchumi by 0.4% itatoa tofauti gani?

Na mbaya zaidi budget haionekani kuweka kipaumbele kwa sector ambayo inagusa 80% ya watanzania yaani kilimo, ufugaji na uvuvi. Hakuna kilimo cha umwagiliaji popote kwenye budget. Lakini lililonistua ni kusoma kuwa Serikali bado inapanga kuingiza vyakula (importation)! Badala ya kujikita kuzalisha wao wanazungumzia kuagiza vyakula nje ya nchi!

Now, twende kwenye kodi. Waziri ametoa viwango vya kodo kama una "kumbukumbu" na pia kiwango tofauti kama "hauna kumbukumbu". Implementation ya hii itakuwa vigumu na most likely itaongeza rushwa.

Mwisho, Budget ina msukumo mkubwa sana wa EAC na wafanyabiashara wakubwa. Misamaha ya kodi ni sawa kama hakuna kilichofanyika. No wonder wanasema uchumi utaongezeka by 0.4%!
 
shegaboy tuko wote....................it is time to tell them enough is just enough.......mizigo wanayotubebesha wao hawako tayari kuinua hata kwa kidole kimoja..........................mateso ni makubwa.
 
Last edited by a moderator:
Ruta,
Unaweza kuwa na point kidogo kwenye hoja zako. Lakini ni vema ukajizuia kwa kuweka nguvu nyingi kumsema waziri kama mtu binafsi, kama vile anatengeneza bajeti hii chumbani kwake na mkewe.

Utatusaidia sana watu kama mimi kama utakuwa unakosoa na kuweka wazo mbadala. Mambo mengine umeweka sana emotions zako bila kutafuta ukweli halisi.

Mfano, unapoweka magari yanayozidi miaka nane pamoja na mitambo ya barabara, uko sahihi? Hata trekta tu linatifautiana sana na gari na hivyo kodi ni tofauti.

Weka arguments, na siyo kuuliza waziri ni mradi wa nani. Ni waziri gani wa fedha alikufurahisha wewe na kwa bajeti ipi?
 
Dr. Mgimwa ni mradi wa Pinda na Makinda na binafsi sina tatizo na hilo maana what matters is the content.

Sijui Zitto atakuwa na mapendekezo gani kwenye alternative budget yake lakini kama atakuwa na mazuri basi ningeshauri wabunge wa CCM wamuunge mkono. Nasema hivyo kwa sababu hii budget ya Mgimwa itawaletea balaa. Kwa mfano anasema watakuza uchumi kutoka 6.4% to 6.8%. Tafsiri yake ni kwamba kwa miezi 12 watakuza uchumi kwa 0.4%! Shida kubwa hapa, kama wananachi hawaoni unafuu wa maisha under 6.4% ukikiza uchumi by 0.4% itatoa tofauti gani?

Na mbaya zaidi budget haionekani kuweka kipaumbele kwa sector ambayo inagusa 80% ya watanzania yaani kilimo, ufugaji na uvuvi. Hakuna kilimo cha umwagiliaji popote kwenye budget. Lakini lililonistua ni kusoma kuwa Serikali bado inapanga kuingiza vyakula (importation)! Badala ya kujikita kuzalisha wao wanazungumzia kuagiza vyakula nje ya nchi!

Now, twende kwenye kodi. Waziri ametoa viwango vya kodo kama una "kumbukumbu" na pia kiwango tofauti kama "hauna kumbukumbu". Implementation ya hii itakuwa vigumu na most likely itaongeza rushwa.

Mwisho, Budget ina msukumo mkubwa sana wa EAC na wafanyabiashara wakubwa. Misamaha ya kodi ni sawa kama hakuna kilichofanyika. No wonder wanasema uchumi utaongezeka by 0.4%!

[MENTION]
FJM[/MENTION] ninaafiki nawe ya kuwa kumpigia mtu debe hakuna shida kama content yake ni kuboresha lakini hapa ina shida kwa sababu waziri wa fedha ni mbumbumbu kabisa wa matatizo yetu na huyu kama wale waliomtangulia atakachoweza ni kutuongezea dhiki na maumivu tu huku akilinda kitumbua chake kwa kuelekeza miradi ya maendeleo kwa Pinda na Makinda, Anne.................
 
tatizo la TANZANIA ni MOja tu...hata kije chama gani...hata labour au Democrats toka marekani waje kushika nchi hapa..ni Utendaji..sisi ni mafundi sana wa kupanga na kuongea lakini utendaji ni SIFURI.....watu wanapiga kelele kuhusu ubora wa katiba, ingawa nakubali kuwa ina mapungufu yake yaliyo wazi ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho lakini katiba yetu sio mbaya maana imegusa maeneo yote muhimu, mambo yote ya msingi yameguswa..n ayapo katika katiba, tatizo ni UTENDAJI...kuna sheria kibao na nzuri sana...zipo kwenye karatasi tu lakini hazijawahi simamiwa for ages...So hata Wakija hao chadema uoza utakua ule ule tu...udhaifu wa utendaji upo damuni na akilini...unless EA community itushape tutakuwa hivi hivi daima dumu...ni mara chache sana kukuta mtanzania mchapa kazi na mkweli...sahau ...wengi ni ujanja ujanja tu na porojo...hata mseme nini Watz MANENO MINGI........VITENDO HAKUNA...unless we change sahauni kuhusu maendeleo..
 
Ruta,
Unaweza kuwa na point kidogo kwenye hoja zako. Lakini ni vema ukajizuia kwa kuweka nguvu nyingi kumsema waziri kama mtu binafsi, kama vile anatengeneza bajeti hii chumbani kwake na mkewe.

Utatusaidia sana watu kama mimi kama utakuwa unakosoa na kuweka wazo mbadala. Mambo mengine umeweka sana emotions zako bila kutafuta ukweli halisi.

Mfano, unapoweka magari yanayozidi miaka nane pamoja na mitambo ya barabara, uko sahihi? Hata trekta tu linatifautiana sana na gari na hivyo kodi ni tofauti.

Weka arguments, na siyo kuuliza waziri ni mradi wa nani. Ni waziri gani wa fedha alikufurahisha wewe na kwa bajeti ipi?

Mbalamwezi tangia ni na uwezo wa kufahamu kinachoendelea hakuna......wote ni bomu tu na ndiy maana nchi ni masikini na adha zetu zinaongezeka
 
Last edited by a moderator:
Kyaiyembe tatizo siyo ni chama gani kipo madarakani bali ni matatizo ya kimfumo ya upatikanaji wa viongozi bora...............tuzame kubadili mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi na hawa wababaishaji watakuwa ni historia......
Hapa siyo mfumo bwana, unaweza ukawekwa na mfumo mbovu lakini ukwa kiongozi bora maana hawa wanajua ni nini wanatakiwa wafanye lakini wanapuuza tu makusudi kwani Wa-Tz ni wapole na hawana tabia ya kuhoji.
Deni kukua kama uyoga ni mfumo, ktoa misamaha ya kodi ovyo ni mfumo.
Hii ni Chukua Chako Mapema sio mfumo.
Si katai mfumo una matatizo lakini watu wanatumia nafasi vibaya, mfumo hauwezi kutufanyia kila kitu.
 
tatizo la TANZANIA ni MOja tu...hata kije chama gani...hata labour au Democrats toka marekani waje kushika nchi hapa..ni Utendaji..sisi ni mafundi sana wa kupanga na kuongea lakini utendaji ni SIFURI.....watu wanapiga kelele kuhusu ubora wa katiba, ingawa nakubali kuwa ina mapungufu yake yaliyo wazi ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho lakini katiba yetu sio mbaya maana imegusa maeneo yote muhimu, mambo yote ya msingi yameguswa..n ayapo katika katiba, tatizo ni UTENDAJI...kuna sheria kibao na nzuri sana...zipo kwenye karatasi tu lakini hazijawahi simamiwa for ages...So hata Wakija hao chadema uoza utakua ule ule tu...udhaifu wa utendaji upo damuni na akilini...unless EA community itushape tutakuwa hivi hivi daima dumu...ni mara chache sana kukuta mtanzania mchapa kazi na mkweli...sahau ...wengi ni ujanja ujanja tu na porojo...hata mseme nini Watz MANENO MINGI........VITENDO HAKUNA...unless we change sahauni kuhusu maendeleo..

[MENTION]mkaliwakitaa[/MENTION] bila ya kujenga mifumo ya kuhamasisha tija a badala yake kila mmoja wetu akawa na njozi n\ya kuwa mbunge au waziri nchi hiyo lazima ikwame hadi pale tutakapoacha kuwatukuza wanasiasa...........
 
Hapa siyo mfumo bwana, unaweza ukawekwa na mfumo mbovu lakini ukwa kiongozi bora maana hawa wanajua ni nini wanatakiwa wafanye lakini wanapuuza tu makusudi kwani Wa-Tz ni wapole na hawana tabia ya kuhoji.
Deni kukua kama uyoga ni mfumo, ktoa misamaha ya kodi ovyo ni mfumo.
Hii ni Chukua Chako Mapema sio mfumo.
Si katai mfumo una matatizo lakini watu wanatumia nafasi vibaya, mfumo hauwezi kutufanyia kila kitu.

Kyaiyembe ubora wa kiongozi siyo kufanya kazi zote mwenyewe bali kujenga miundo mbinu ya kimfumo ambayo itawashirikisha wenzie kusukuma gurudumu la maendeleo yetu.........na hivyo hata kama hayupo hiyo mifumo itaendelea kufanya kazi............
 
Last edited by a moderator:
Jana nilijaribu kumsikiliza waziri wa fedha Dr. Mgimwa na swali lililokuwa likijirudia mara kwa mara kichwani mwangu ni hivi huyu Mheshimiwa ni mradi wa nani?

Baada ya JK kudhalilishwa na mawaziri wake wawili wa fedha kwa maana ya utendaji duni wa Meghji na Mkullo ni dhahiri alitafuta ushauri wa nani anafaa kumsaidia kwenye wadhifa tajwa................ni nani ushauri wake JK aliuzingatia katika uteuzi tajwa?

Wakati serikali ya JK ikikumbwa na kashfa ya CAG ya matumizi mabaya ya fedha ulikuwepo uvumi kuwa hata PM alikuwa anafikiria kujing'atua na kumwacha JK azame na merikebu yake ya TITANIC...................lakini hakufanya hivyo ni kwa sababu zipi?

Jingine ni kuwa wakati makabrasha ya wizara ya fedha ya bajeti yalipocheleweshwa alikuwa ni Pinda aliyemkingia kifua Dr. Mgimwa kuwa Dr. Mgimwa alikuwa na kibali cha Raisi ayapitie upya makadirio tajwa ili na yeye kwenye wadhifa wake mpya aweze kuweka michango yake.................baada ya kupitia bajeti husika sioni kama kuna jipya ukiondoa misamaha ya kodi kwa walalahoi wanaopata chini ya milioni tatu na hata hapo naona bado kuna uonevu umefanyika na nitafafanua baadaye..........

Jingine, jipya ni kuamsha ari za usajili magari kwa majina binafsi na kuyalipia milioni 5 kila baada ya miaka 3...............hili ni kuiga marekani ambako utaratibu huu umeshamiri.................

Mengineyo yote yaliyomo kwenye bajeti, hata Mkullo au Meghji wangelisoma hayohayo kwa hiyo sioni khoja ya Pinda ya ucheleweshwaji wa bajeti kama ina mashiko.......................

Kwa hiyo, kama Pinda alilidanganya Bunge kwa minajili ya kumlinda Dr. Mgimwa alifanya hivyo kwa masilahi ya nani? Kwa maoni yangu binafsi, Pinda na wala siyo JK ndiye mhimili na mfadhili wa huyu waziri mpya wa fedha na Pinda anaona kavuna dume kwa sababu amekuwa akitafuta mianya ya hazina kusukuma kwa kasi maendeleo ya mkoa wa Rukwa hususani jimbo lake la uchaguzi........na Mkullo hakuwa akimsikiliza sana kwa sababu ana uhusiano wa moja kwa moja na JK uhusiano wa miaka mingi tangia akiwa NPF na JK akiwa kwenye baraza la Mwinyi........

Bajeti hii ina sifa za kulinda masilahi ya viongozi na wala siyo ya walalahoi na maeneo haya ndiyo maangalizo 10 ambayo yananifanya nije na misimamo tajwa:-

1) Viongozi wote serikalini wanakiri kuwa makali ya maisha yameongezeka lakini ufumbuzi wao ni kulinda walichonacho au hata kujiongezea bila ya kujua kwa kufanya hivyo walikuwa wanapunguza huduma za kijamii na hivyo kumwongezea makali mlalahoi. Mishahara ya viongozi na sheria ya pensheni ya viongozi vilitakiwa vifanyiwe marekebisho makubwa ili kuondoa ubaguzi ambao unafanywa na viongozi kwenye nyanja hiyo kinyume na sheria..................haya hayakufanyika na kamwe hayatafanyika katika kipindi cha JK akiwa madarakani kwa sababu yeye mwenyewe ni matunda ya mfumo mbovu wa upatikanaji wa viongozi kwa hiyo hawezi kuwa na hisia kali ya kurekebisha mapungufu yaliyopo na hata hisia tajwa angelikuwa nazo bado hana ujuzi wa kufanya hivyo....................kwa lugha nyingine JK ni matunda ya kunukuu staili ya utendaji mbovu ya wale aliyewarithi.

2) Kumpunguzia makali mlipa kodi mwenye kipato cha chini ya milioni 3 ni unafiki wa kupindukia. Mtumishi wa serikalini mwenye kipato kama hicho hana
capital costs kwenye mapato yake jambo ambalo anayejiajiri anazo. Tumchukulie mama ntilie mwenye kipato cha milioni 3 kwa mwaka utakuta gharama zake za kuendesha mradi ni asilimia 70 hadi 90 ya mapato tajwa sasa ukimtoza kodi katika kiwango hicho cha chini ni dhahiri unatoza mtaji na hivyo kumwongezea adha za kufukarika. Serikali iliyo makini ingeweka wazi apataye mapato chini ya Tshs 20 millioni kwa mwaka hapaswi kulipa kodi kwa sababu hicho kiwango ni cha kumwezesha kujiajiri na kumudu gharama za maisha...............hivyo pamoja na porojo za Dr. Mgimwa bado hana hisia kali za adha ya umasikini na vyanzo vyake hapa nchini..

3) Kodi za magari chakavu kupandishiwa umri kutoka miaka 10 hadi zaidi ya miaka 8 ni panga linalokata pande mbili: sababu za kulinda mazingira ni lazima zilinganishwe na sababu za kukuza uchumi. Dr. Mgimwa alipaswa atofautishe aina ya vyombo husika.... magari ya anasa na vifaa vyovyote vile vya anasa ni sahihi kuvitoza kodi tajwa lakini vyombo vya uzalishaji kama vya barabara, ujenzi na viwandani vilipaswa kubaki umri uleule wa miaka 10 kutokana na mchango wake katika kuinua kipato cha nchi na kuwapatia ajira raia wake. Utashangaa kufahamu zaidi ya asilimia 90 ya mitambo ya barabara inayojenga barabara zetu in umri wa zaidi ya miaka 10. Sasa ukianza kutoza kodi ya asilimia 20 kwa yule anayeagiza mitambo hiyo ambayo bado kabisa ina khali nzuri sana huo ufukara unamletea nani kama siyo mlalahoi anayetegemea kujipatia kipato kutokana na vyanzo hivyo vya uzalishaji.

4) Bajeti kama zile zilizoitangulia bajeti hii, imeshindwa kuainisha kwa kushirikiana na CAG mianya ya kuporomoka uwajibikaji katika matumizi ya serikali. Haitoshi kwa Dr. Mgimwa kudai usimamizi wa bajeti hii utakuwa tofauti na zile zilizotanguliwa bila ya kuonyesha kwa namna zipi. mfano serikali za mitaa inabidi zimilikishwe halmashauri kwa madiwani wawe na mamlaka ya kuajiri watumishi wa ngazi zote badala ya kutegemea serikali kuu kupandikiza mamluki wao ambao ni viwavi jeshi na madiwani kubakia ni wapiga tarumbeta za hamelini. Kwenye mashirika ya umma kuna uhaja wa kubadilisha mfumo mzima wa uteuzi wa bodi na bodi kuwa na mamlaka ya mwisho ya uteuzi wa watendaji wote wakiwemo CEOs kwenye taasisi zao badala ya Ikulu kuona ni kivuno cha kupanga safu za viwavi jeshi. Bodi za wakurugenzi zinapaswa zitokane na wadau wa sekta husika ambao watapatikana kwa kupigiwa kura na washiriki wa nyanja husika hivyo kuondoa mmomonyoko wa uwajibikaji. Wenyeviti wa Bodi kuchaguliwa moja kwa moja na wajumbe wa bodi badala ya Ikulu kuwabandikia mtu ambaye hushukuriwa kwa sababu za kumlinda kisiasa bila ya kujali kama ana mchango wowote wa taasisi ambayo amekabidhiwa kuisimamia....

5) Kusahau nafasi ya michezo katika kuleta ajira na kukuza uchumi. Timu zote za daraja la juu (Premier league) la mpira wa miguu zilitakiwa zitengewe fungu la kuanzisha timu za watoto ili kuibua vipaji kama sehemu ya awali ya kuanzia. La ajabu viongozi wetu kila siku huimba soka huendelezwa na timu siyo timu ya taifa lakini ni wagumu kwenye mioyo yao kutoa fedha za shughuli hiyo nyeti katika kukuza vipaji vya michezo, kufufua uchumi na kuwapatia ajira vijana wetu. Kwa kuanzia kila timu iliyoko kwenye Premier league ingelitengewa shilingi milioni 200 kwa mwaka kwa kazi hiyo ya kukuza vipaji vya vijana na fedha hizo CAG lazima akague matumizi yake.
Haya, huyu Dr. Mgimwa hawezi kuyafikiria kwa sababu ni kizazi kilichopitwa na wakati.

6) (a) Upendeleo wa misamaha ya kodi zote kutofutwa kwa vigezo ambayo vinakinzana na katiba yetu ya kuondoa aina zote za ubaguzi. Katika hukumu ya KTM {Karibu Textiles Mills} mahakama zote za juu zilisema ni ukiukwaji wa katiba kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya makampuni tu tena yapo kwenye sekta moja khalafu wengine mkawabagua eti kwa sababu wana mikataba yao na wengineo hawana. Mbali ya ukweli kuwa ubaguzi tajwa unatibua nguvu ya soko lakini la kuzingatiwa ni kuwa katiba iko juu ya mikataba tajwa.
Nilidhani kama Dr. Mgimwa is the real deal angeliifuta mikataba tajwa kwa kuongozwa na hukumu za KTM ya EAC na ya CAT (TZ COURT OF APPEAL) katika kutenda haki. Lakini kwa vile, Dr. Mgimwa hakuwekwa pale kwa dhamira safi ya kulisaidia taifa bali ni kujibu tu kiu ya aliyemweka ambaye ninaamini ni Peter Mizengo Pinda basi upeo wa kuyaona haya hana na hivyo hana sifa hata moja ya kuwa Waziri kwenye nyadhifa yoyote ile kwenye baraza la mawaziri achilia mbali Wizara ya fedha.

b) Misamaha ya kodi kwenye mahoteli ya kitalii kanda ya kaskazini haijafutwa ambayo inaigharimu nchi zaidi ya dola 20-70 milioni kwa mwaka. Sasa Dr. Mgimwa alichelewesha bajeti hii kwa nini kama...........it is business as usual, na hata huyo Pinda aliyekuwa akimtetea hivi haoni hata haya?

What a shame!

7) Eneo ambalo humgusa mlalahoi moja kwa moja ni eneo la kodi. Kodi ya VAT ya asilimia 18 imesaidia sana katika kufifilisha soko la ajira. Hawa wakubwa wakisha kulamba hela yetu pale hazina hukimbilia kudai haya ni makusanyo ya serikali na kusahau hata siye ambao hatujaajiriwa serikalini nao ni sehemu hiyo hiyo ya serikali. Serikali yoyote ambayo haisikilizi kukua kwa gharama za maisha na uhaba wa vyanzo vya uzalishaji hiyo serikali siyo sikivu hata kama ikidai vinginevyo.

a) Kwa kuanzia VAT ilipaswa kupunguzwa kutoka asilimia 18 hadi 15 ili kuhamasisha waajiri wakuze soko la ajira na kuongeza ushindani wa bidhaa zetu kwenye soko la dunia. Mapato ya serikali kuyaongeza siyo kuongeza viwango vya kodi tu bali kuwa na kiwango cha kodi ambacho kitahamasisha tija na uzalishaji. Hili tuendelee kulidai kwani ni haki yetu kukataa kuburutwa bila ya siye kutaka katika ufukara wa kujitakia.

b) VAT ya EWURA na REA, kwenye umeme ni ya kuondoa tena kinatakiwa kiwe kitendo cha haraka sana. Hivi huo umeme wa vijijini hata ukipelekwa ni nani kule atakayeweza kuumudu gharama zake kama hata wakaazi wengi wa mijini naona wamerudishwa kwenye vibatali tu? Kiujumla wakaazi wa mijini wana uwezo wa kumudu gharama za maisha zaidi ya wale wa vijijini na kama mfupa umemshinda mzee fisi je nani atauweza?

Hivi huyu Dr. Mgimwa anaelewa nchi hii inatoka wapi, iko wapi na yaelekea wapi? Kama siyo mbabaishaji tu?

8) Kukwepa kufuta road tolls za magari makubwa. Kila mahali alipokuwa akihalalisha kupanda kwa kodi, Dr. Mgimwa alikuwa anajificha kwenye kichaka cha EAC na sheria zake. Bajeti ya jana ya Kenya wamefuta vizuizi vyote vya barabarani vikiwemo vya tozo za magari makubwa, usafirishaji wa vyakula n.k .......................sasa hayo maigizo ya EAC mbona hayakufika kwenye kufuta road tolls ambazo zinatajirisha watu wachache badala ya kulitajirisha taifa?????????????..........Kuhusu uzito wa magari ni udhibiti wa idadi ya matairi ya nyuma la gari au load axles unatosha kabisa kuhakikisha magari yetu hayazidi tani stahiki. Kenya wao lori lenye axles 3 tu ndizo zinaruhusiwa kwenye barabara zao. Sasa ukiisha kulisimamia hilo huu uchafu wa road tolls ambazo zinaongeza mrundikano wa bidhaa na kuchelewesha huduma kwa jamii huku zikimwongezea mlaji gharama zisizorejesheka ni wa nini kama siyo kulinda ajira na ufisadi wa watoto wa vigogo ambao ndiyo wamerundikwa kwenye vituo vya matozo tajwa?

9) Ukuaji wa deni la taifa Dr. Mgimwa aliuchukulia kimzahamzaha tu na hakuna maelezo ya kutosha kuelezea ni kwa sababu zipi taifa limebebeshwa mzigo wa deni la trilioni 5 tu wakati Mkapa anamkabidhi Jk nchi na khalafu deni hilo lipande khadi trilioni 8 mwaka 2009 na leo lifikie trilioni 22 (Kwa fedha za kitanzania)? Tathmini ya nani alikopa na kwa idhini ya nani inabidi ijulikane sasa na hata CAG sijui yuko wapi kutathmini hilo na badala yake anatumia muda mwingi kuwabana halmashauri ambao mapato yao ni kiduchu. Dr. Mgimwa kama angelikuwa makini angelianzisha sheria ya kuhakikisha bunge ndilo lenye mamlaka ya kupitisha mikopo yote ya serikalini. Hatukumchagua Raisi aende Ikulu kufanya atakavyo bila ya kuwajibika kwa yeyote. Haya madeni yatalipwa na wajukuu zetu na vilembwekazi hata hatujui hizo fedha zilifanya nini na aliyekuwa aziidhinisha alifanya hivyo kwa mashinikizo ya akina nani...........

10) BOT imekuwa haitazamwi juu ya vyanzo vyake vya mapato na matumizi na imekuwa kinara wa ufisadi ambao hata CAG huwa anaufumbia macho. Wakati umefika mapato na matumizi ya BOT yakawekwa wazi na ile sheria ya kulizuia bunge kudhibiti BOT ikafutwa na kurejesha BOT mikononi mwa udhibiti wa Bunge......................

Kwa haraka haraka, Dr. Mgimwa ni bomu na tusitishike na kauli zake za kujiamini..mara nyingi matapeli ndivyo walivyo.............na nimpa D minus kwenye maandalizi ya bajeti inayomjali mnyonge...............................have your say too.

Naomba kukuuliza mheshimiwa yafuatayo:
i. Kwani Mh. Waziri kaandaa hiyo bajeti peke yake?
ii. Wataalamu wa wizara ya Fedha, BOT, Mashirika ya Fedha nk hawakuhusika?
iii. Je ana muda gani hapo HAZINA hata tumtoe makosa kupitia bajeti aliyokuta imeandaliwa?.
iv. Mwisho usisahau ni mara ya kwanza yeye kusimama Bungeni na kupewa jukumu kubwa kama hili. It is obvious anaweza kuwa ametetereka ktk kuongea na kuwasilisha mada. Hilo lisitufanye tuendelee kumuona hafai.
v. Watanzania wenzangu safari ya ukombozi wa Mtanzania bado ni ndefu hivyo nasisitiza tumpe muda anaweza kuwa Daudi aliyemuua Goliati. Tupunguze negativity kubwa tuliyonayo inayosababisha upofu hata yaliyo mazuri hatuyaoni wala hatutayaona tukiendelea hivi. Tumuombee yeye na viongozi wengine watuongoze vizuri na kwa uadilifu, pia na tuiombee Tanzania yetu, nani ajuae Daudi amepatikana?
Queen Esther
 
[MENTION]Queen Esther [/MENTION]

hoja hizi zinakuja baada ya waziri mkuu kudai ya kuwa makabrasha ya bajeti yalichelewesha la kumpa waziri mpya wa fedha muda aliomwomba Raisi ili aifumue na kuisuka upya kulingana na matakwa yake...............kwa hiyo upende usipende bajeti hii ni ya Dr. Mgimwa na wala siyo ya hao wengineo...............wao kazi yao ni kumshauri tu lakini mafanikio na maanguko ya bajeti tajwa yapo mikononi mwake.........................tumpe muda wa kutosha wa nini kama dalili za siku mbaya huanza tangia asubuhi?

katika huu ubabaishaji wafikiri tunaletu hapo?
 
Kimsingi nakubaliana na wewe, tatizo lililopo hapa ni serikali kuongozwa na watu wenye akili za mgando. Hakuna jipya katika hii bajeti. Imekosa kapisa ubunifu zaidi ya kuweka bold kwenye font na kuongeza font size.
Bajeti inaposomwa inakosa msisimko kuisikiliza maana utakuta yale yale yalionzishwa na Mkapa ndo yanawekewa bold. Pombe, sigallah, na vinavyofanana navyo.
Tunachoweza Tanzania siyo kubuni vyanzo vipya vya mapato, bali kubuni vyanzo vipya vya misamaha ya kodi.

What a shame.
 
Naomba kukuuliza mheshimiwa yafuatayo:
i. Kwani Mh. Waziri kaandaa hiyo bajeti peke yake?
ii. Wataalamu wa wizara ya Fedha, BOT, Mashirika ya Fedha nk hawakuhusika?
iii. Je ana muda gani hapo HAZINA hata tumtoe makosa kupitia bajeti aliyokuta imeandaliwa?.
iv. Mwisho usisahau ni mara ya kwanza yeye kusimama Bungeni na kupewa jukumu kubwa kama hili. It is obvious anaweza kuwa ametetereka ktk kuongea na kuwasilisha mada. Hilo lisitufanye tuendelee kumuona hafai.
v. Watanzania wenzangu safari ya ukombozi wa Mtanzania bado ni ndefu hivyo nasisitiza tumpe muda anaweza kuwa Daudi aliyemuua Goliati. Tupunguze negativity kubwa tuliyonayo inayosababisha upofu hata yaliyo mazuri hatuyaoni wala hatutayaona tukiendelea hivi. Tumuombee yeye na viongozi wengine watuongoze vizuri na kwa uadilifu, pia na tuiombee Tanzania yetu, nani ajuae Daudi amepatikana?
Queen Esther

[MENTION]Queen Esther [/MENTION]

hoja hizi zinakuja baada ya waziri mkuu kudai ya kuwa makabrasha ya bajeti yalichelewesha la kumpa waziri mpya wa fedha muda aliomwomba Raisi ili aifumue na kuisuka upya kulingana na matakwa yake...............kwa hiyo upende usipende bajeti hii ni ya Dr. Mgimwa na wala siyo ya hao wengineo...............wao kazi yao ni kumshauri tu lakini mafanikio na maanguko ya bajeti tajwa yapo mikononi mwake.........................tumpe muda wa kutosha wa nini kama dalili za siku mbaya huanza tangia asubuhi?

katika huu ubabaishaji wafikiri tunaletu hapo?
 
tatizo lingine TANZANIA NI USHIRIKINA...ukiwa mchapakazi na mweli ...siku zako ni chache hapa Duniani..nimeshaona kwa wengi..na ndo kisa kimenitoa kwenye ajira ya serikali na kujiajiri...wewe jifanye ni mchapa kazi , ukaanza kupata viji safari vya hapa na pale na marupu rupu..utaona jinsi watu wanavyokutazama kwa macho makali...watu wafanyi kazi lakini chuki na wivu vimewatawala..bora kujiajiri kuliko kufa kwenye ajira za serikali...huku nako kwenye kujiajiri taabu tupu..ukianza kufanikiwa mara ooo jamaa anauza unga...mara oo free masons...ina maana ni Tanzania pekee mbapo mafanikio huja kwa kuuza unga na ufreemasons pekee.. naipenda sana nchi yangu...lakini tabia za wakazi wake ni za ajabu sana....Mungu ibariki Tanzania...labda vizazi vijavyo na si hiki wataishi kwa amani na kuifaidi hii nchi bila ushirikina , majungu na wivu...
 
Back
Top Bottom