Ni nani alifanya utafiti umri wa miaka 18 ndio umri wa mtu uzima?

DsmicSound

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,622
2,000
Kuna mambo tumeyakuta na tunayafanyia kazi bila sababu za Msingi...? Mfano hata hizi sikukuu tulizokuta... Mfano sijui tarehe 14 feb sijui siku ya mama au mwanamke...

Hili suala la miaka 18 sijui ndio umri wa kuolewa au kuoa... Miaka 18 ndio umri sijui wa kufanya maamuzi binafsi...
Wakati muumba mwenyewe ndiye aliyetuambia... Mtoto akinyonya kikamilifu anyonye miaka 2...Rejea kwenye quran...


Na alisema mtu akibalehe ni ruhusa kuozeshwa... Na haki ya uyatima inamtoka... Na akibalehe na kujitambua anaanza kuhesabiwa matendo yake... Mema na mabaya...Yaani thawabu na dhambi...


Sasa hii miaka 18 imetoka wapi ili iweje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

goldcall

JF-Expert Member
Oct 20, 2017
322
500
mimi nimesoma title yako nikazani umeandika vitu vya maana, kumbe reference ni quran, acha kuuliza upupu humu!!!
 

SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
8,008
2,000
Sasa ndugu mtoa mada, ulitaka utu uzima iwe miaka 9 au zaidi ya 18?

Kuna mambo mengine ni ya kutumia akili zako tu, ukiona sawa uyafuate kama hayana maana kwako unapiga kimya tu.

Tuna mengi ya kuwaza na kufanya. Ila umeuliza swali la msingi sana na pia ni tafakuli njema kuijadili pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Gyole

JF-Expert Member
Sep 20, 2013
6,921
2,000
Kasome Mambo ya afya utaelewa, ila nikuambie zamani watu walibalehe miaka 20 na zaidi, Ila siku hizi wanabalehe miaka 10 tu, sasa upo radhi mwanao miaka 10 aolewe au aoe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
13,519
2,000
Ancient civilizations hasa Greeks, Babylonians na Romans ndio waanzilishi wa sheria mbali mbali na lengo lao ilikua kuondoa u-barbarian katika jamii.

Imagine jamii ambayo mtu anaweza kufanya kila anachotaja vile anavyoweza, ilikua ni chaos. So wanajamii walikubaliana ku set rules/regulations/laws ambazo zitawa guide katika maisha yao ya kila siku.

Kuhusu hilo la miaka 18 ni suala tu la kufikiri, kadiri watu walivyozidi kuwa civilized na kuelimika na kuwa na long term plans za ku preserve tamaduni za jamii zao moja ya njia sahihi ni ku set sheria zitakazo linda kizazi kijacho (minors). Ndio maana wakaweka sheria hizo ili kulimit vitu ambavyo anaweza kufanya mtu wa chini ya miaka flani labda 17, 18, 20, 21 e.t.c (hii sheria ya minor zinatofautiana kutegemeana na nchi na nchi).

Ku limit umri wa mtu kunywa pombe, kuingia mkataba, kuendesha gari, kuolewa n.k kunasaidia kulinda wale ambao wanaonekana bado hawajapevuka vya kutosha kuweza kufanya maamuzi sahihi (consent). Kama unavyojua kadiri mtu anavyokuwa kiumri akili yake nayo hukomaa na kuweza kuwa na judgement bora zaidi.

Ndio maana huwezi kumfuata kijana wa miaka 15 akushauri jambo la muhimu ukamuacha mzee wa miaka 50 kwasababu unajua huyu mzee atakuwa na busara zaidi kutokana na experience ya maisha na exposure.

Ni maoni yangu tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom