NI NANI AFISA MWAJIBIKAJI SERIKALINI (Accounting Officer) ?


B

Byendangwero

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Messages
872
Likes
5
Points
0
B

Byendangwero

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2010
872 5 0
Katika Gazeti la MwanaHalisi la wiki iliyopita kulikuwepo stori iliyohusu namna wakubwa waliokuwemo katika serikali iliyomaliza kipindi chake hivi karibuni, walivyo jinemesha wakati wa kulipana mafao yao. Mbali na kuguswa na mmomonyoka wa maadili uliopelekea Mawaziri na Manaibu wao kulipwa mara mbili; kwanza kama mawazili na baadaye kama wabunge, nilishutushwa na barua iliyoandikwa na Sitta kwa JK ikimtaka kuidhinisha malipo ya kamishna wa bunge(hata sijui hawa ni wakina nani!). Mimi nilidhani ya kuwa Afisa Mwajibikaji serikalini ni Katibu Mkuu wa wizara husika, na wala siyo wanasiasa. Kitendo cha kumwona rais mzima anakubali kujiingiza katika masuala ambayo kwangu mimi ni ya jikoni kimenidhihirishia kuwa fedha zetu haziko salama. Hii inatokana na ukweli kwamba katika hali halisi usimamizi wa mambo ya fedha unakuwa mikononi mwa watendaji, wanasiasa kazi yao ni kuwadhibiti watendaji hao ili wasije wakatumia fedha hizo kinyume na kanuni zilizowekwa. Sasa kama wanasiasa wanaweza kwenda moja kwa moja jikoni, nani atakuwa na uwezo wa kuwadhibiti.
 
K

kayumba

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
654
Likes
5
Points
35
K

kayumba

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
654 5 35
Ndiyo maana tunataka katiba mpya ili tuangalie na madaraka ya mkuu wa kaya. Hukumbuki jinsi alivyaamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe kwenye EPA!
 
G

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
2,641
Likes
8
Points
135
G

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
2,641 8 135
Katiba mpyaaaaaaaaaaaa.
 

Forum statistics

Threads 1,238,314
Members 475,877
Posts 29,315,867