Ni namna gani ya kushangaza uliweza kujua kwamba rafiki yako ni tajiri

Mm wala si shule ni kitaa cha kukutaniana tu jamaa lilikuwa bonge chafu chafu tu , anakibanda cha chips tulikuwa tunapenda kukaa tu nae kupiga story na nini muda uende aiseee kumbe bhana mshikaji ni anahela balaaa migorofa kkoo yani pale kwenye chips za jioni ni kupenda tu kuishi maisha ya kawaida sana, kuna watu hela kwao ni kitu cha kawaida mnoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha bilionea mmoja alikua anaitwa Paul Allen (mwanzilishi mwenza wa Microsoft pamoja na Bill Gates), mwezi wa sita mwaka 2018 nilibahatika kukutana nae Serengeti alikuwa yupo na wamasai anapiga nao soga. They had no clue who he was, and how much loaded he was.

Hakuna kitu kizuri kama kujichanganya na watu halafu hawajui kama una mfuko mpana au la (stealth wealth). Inakuepusha vitu vingi sana kuanzia marafiki bandia mpaka business proposals kila mtu anataka uweke pesa ktk mipango yake.

Always avoid being flashy (kama upo mjini endesha magari madogo madogo, mf IST au Carina), don't splash your lifestyle on social media.
 
Kuna mmoja yupo group la WhatsApp ni tajiri na wote hatukujua,
Siku tunabadilishana mawazo akatukaribisha Kwake ni Arusha bwana weee kwenda kwenda kwa Maelekezo tukajikuta tumasimama mbele ya boonge ya mgorofaaaa.....

Kilichofata ni historia, kumbe ule mjengo ni wa kwake na yeye ndo anaishi hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana we jamaa unashoboka Sana,ukifika Kwa MTU unaanza kumuuliza uliza hiki cha Nani,unashngaa magari etc,mpaka huyo jamaa kakujibu shombo nimeuza X3 sasa hvi Nina X5,hqta mm ukinikuta mahali nakunyoosha Tu ili uache kutafuta hela uwaze kupost ujinga kama huu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni rahisi kuficha kama wewe kwenu kuna uwezo kwenye level hiyo ya elimu ila kwa level ya chuo ngumu sana hata ufanyaje hata uwe sio wakuvimba na kuShow off ila watu watajua kama wewe kwenu kuna kitu.

Portfolio | 2020
Watajuaje? Kama mtu ameamua kukaa hostel na wenzie, anapokea boom kama wenzie na anakula canteen kama wenzie tutajuaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watajuaje? Kama mtu ameamua kukaa hostel na wenzie, anapokea boom kama wenzie na anakula canteen kama wenzie tutajuaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Pressure za kusubili boom utakuwa huna, vile vipindi vya pasi ndefu boom limekata utakuwa havikupati, kukopakopa kawaida kwa mwanachuo wewe hutakopa na kukopwakopwa kawaida 100K nk kioindi watu wanasota...kuna life huwezi kuliigiza au ku-fit hapo ndipo some questions mark zitakuja kwa jamaa huyu vipi mbona hayaface tunayo yaface.

Mshikaji wangu kwao maDon anaishi kawaida ila pressure kama hizo hatawai zi face.

We umewasema watu wenye uchumi wa kati mtoa mada amewasema madon.
Haya mambo ya kutokopa wala kutokuwa na hekaheka za boom hata mimi nayaweza sana wakati njaa kali home.
Kuna jamaa naishi nae ghetto mzee wake ana mashine za kukamua dhahabu, vitalu, gesti, ekari kibao, bajaj, gereji na miradi kibao. Huyu jamaa binafsi ana nyumba yake ya kuishi kaijenga mwenyewe kutokana na mishe alizokuwa anamfanyia mzee wake na ana kiwanja pia.
Sasa huyu mtu kwa kukopa ndo hatari, anakopa vibaya mno wakati kwao ana hela. Ukimtazama hivi utaona ni mtu wa chini lakini siku akiamua kuonesha makali watamtambua.
 
Ni rahisi kuficha kama wewe kwenu kuna uwezo kwenye level hiyo ya elimu ila kwa level ya chuo ngumu sana hata ufanyaje hata uwe sio wakuvimba na kuShow off ila watu watajua kama wewe kwenu kuna kitu.

Portfolio | 2020
Hata chuo wapo mkuu
 
Kuna kabinti fulani hivi nilikutana nako fb,nilkua nakaa nako mji mmoja siku naonana nako nilikaona ka kawaida mno ndo kalikua kamemalza form 4..aisee siku kamenipeleka kwao nilbaki natoa macho tu mjengo niliokutana nao ni laana zmepaki ndinga 3 za maana,moja bonge la V8 jeupe..akanigusia tu baba ake anafanya kazi Canada..hyo V8 baba ake alipewa zawadi siku ya birthday yake na kaka ake anaeishi ujerumani..nikahoji kaka ako na dada ako je wako wapi,kaka ake ansoma sweden na dada ake anasoma australia sikuendelea kuhoji,ule msemo ukanijia kichwani, usi mdharau usie mjua binti mwenyewe ukimkuta mtaani unaweza sema kwao maisha magumu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom