Lawrichie
JF-Expert Member
- Aug 27, 2013
- 753
- 2,044
Amani iwe nanyi nyote.
Ndugu zangu, hivi karibuni nilipata mchongo kutoka kwa rafiki yangu ambae yuko US kwamba kuna kampuni ambayo inawasaidia watu kutoka nchi mbalimbali, watu ambao wanatamani kufanya kazi US, kujiendeleza kielimu, kuhamia na kuwa na makazi ya jumla au kwa ajili ya utalii tu.
Huyu binti tuna kama miezi 8 hivi toka tufahamiane japo bado hatujaonana, ila yeye ndie aliyenishauri nijaribu kutuma barua pepe ya maombi kwenye kampuni ambayo amenitajia kuelezea shauku yangu ya kufanya kazi US.
Sasa basi ndugu zangu, nimeandika uzi huu ili nipate uzoefu kwa watu mbalimbali waliowahi kuandika ama wanafahamu jinsi gani barua ya aina hii huwa inaandikwa au jinsi gani inatakiwa iwe. Nimeshapekua Google nimepata mwanga wa angalau nini natakiwa nifanye lakini nafikiri JamiiForus ina watu makini zaidi karibu katika kila kitu.
Sijawahi kuandika barua ya aina hii kabla, hivyo nataka nikiandika kusiwe na kasoro. Barua natakiwa niitume kwenye kampuni kuwajulisha nia yangu ya kufanya kazi kwa Trump na jinsi gani nawaamini wao katika kufanikisha adhma yangu.
Naamini nitasaidiwa kupitia hili jukwaa huru.
Karibuni.