Ni mzee gani alimpa Nyerere makochi ya kukalia ambayo yapo kwenye nyumba ya Nyerere hapo magomeni?

EngutanK

Member
May 3, 2021
99
244
Hebu wanaomshughulikia Mh. Mbowe kwa kumsababishia awe na hali ngumu ya kisiasa na kiuchumi waniambie ni Mzee gani alimpa mzee Nyerere makochi ya kukalia katika nyumba yake aliyopewa iliyopo magomeni wakati wa kudai uhuru?

Nyumba hiyo ipo magomeni imekuwa kama nyumba ya mkumbusho ukienda hayo makochi utayakuta. Hawo wanaompa hali ngumu Mh Mbowe kisa tu ni mpinzani Mzee Nyerere walimpa wao makochi?

Au wazazi wao ndo walimpa Nyerere hivyo viti? Au walitaka Mzee Nyerere akae chini?

Kosa la Mbowe ni nini, kuwa mpinzani?
 
Ni Mzee MBowe baba yake Mh. Mbowe ndiye alimstili Mzee Nyerere, baada ya kupewa nyumba hapo magomeni yeye yule Mzee babayake Mh. Freeman Mbowe akampa makochi akalie mzee, ushuuda huu aliwahi kusema Mke wa Nyerer Mama Maria Nyerere,alisema Mzee Mbowe alitupa viti vya kukalia ambavyo vipo mpaka leo

Mzee Nyerere watoto wa wazee ambao alipigania nao uhuru aliwalinda na kuwapa heshima kwa kadri alivyoweza alivyoweza. Aliwapa upendeleo kuliko hata watoto wake mwenyewe wa kuwazaa.

Kuachilia Mbowe ambaye aliitumia nyumba ya msajili ya nyumba (NHC) kuwa Mbowe HOTEL au club maarufu ya Bilicanans ambayo utawala wa awamu ya tano ukaja kumnyang`anya,pia wapo mtoto wa John Lupia ambaye alikuja kuwa Katibu kiongozi, pia wapo watoto wa Hamza Mwapachu yaani Bakari Mwapachu ambaye alikuja kuwa mbunge na waziri pia Juma Mwapachu ambaye alikuja kuwa katibu mkuu wa jumuia ya africa mashariki, hao ni baadhi tu. Sasa wanzetu hawa wanaojifanya wanajua sana ndo kwanza wanawaharrass vijana hawa sijui kwa faida ya nani.
 
Duh hizi story za Familia ya Nyerere na familia ya Mbowe hizi...!. Hebu tutafutie profile picha ya Mzee Mbowe, Nyerere na Freeman, kwa ajili tuu ya kumbukumbu maana..., kumbe hadi kupeana makochi!.

Yaani mnataka kusema kama sio Mzee Mbowe, Familia ya Nyerere wangekaa chini?!.
P
Aikaeli Mbowe.jpg
Aikaeli Mbowe.jpg
Nyerere.jpg
 
Duh hizi story za Familia ya Nyerere na familia ya Mbowe hizi...!. Hebu tutafutie profile picha ya Mzee Mbowe, Nyerere na Freeman, kwa ajili tuu ya kumbukumbu maana..., kumbe hadi kupeana makochi!.

Yaani mnataka kusema kama sio Mzee Mbowe, Familia ya Nyerere wangekaa chini?!.
P

..Mzee Aikaeli Mbowe ndiye aliyepeleka posa ya Makongoro Nyerere wakati anachumbia Machame.

..Pia Mzee Aikaeli aliwahi kugombea ubunge kupitia Tanu akashindwa na Bw.Solomon Nkya Eliufoo.

..Zaidi, pale mtaa wa Samora lilipojengwa jengo la extelcoms kulikuwa na hoteli ya Mzee Aikaeli ambayo ilitaifishwa.

NB:

..Kila mahali ambapo Tanu ilibisha hodi kuna wenyeji ambao walifanya kazi ya kufungua milango. Kwa upande wa Uchagani ilikuwa watu kama Solomon Eliufoo na Aikaeli Mbowe. Kwa maeneo ya Usukumani kulikuwa na Paul Bomani "kishamapanda " ambaye alifanya kazi kubwa Tanu ikakubaliwa na Watemi wa Kisukuma.
 
Kwa upande wa Kaskazini yaani Arusha.Mzee Nyerere alisitiriwa na kufadhiliwa na familia kama tatu hivi wakati wa kudai uhuru.

Mwl Nyerere alikuwa akitafutwa na kufuatiliwa na wakoloni,familia ya Marehemu Maeda zilikuwa zikimficha Mwl Nyerere na kumuhifadhi katika nyumba zao zilizotapakaa katika miji ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara.Mpaka leo kuna mitaa/barabara zenye majina ya Mzee Maeda.Yupo Mzee mwingine jina lake Reuben Mswiya na wazee wengine wengi walijitolea sana wakati wa kudai uhuru.

Bahati mbaya watoto wao au wajukuu wao hawajapenda kuandika vitabu vya kuwaenzi wazee wao kama alivyofanya Mohamed Said wa mtaa wa Kipata.

Najaribu kufanya mawasiliano na hizi familia ikiwezekana nitaweka hadi ushahidi wa picha.
 
Duh hizi story za Familia ya Nyerere na familia ya Mbowe hizi...!. Hebu tutafutie profile picha ya Mzee Mbowe, Nyerere na Freeman, kwa ajili tuu ya kumbukumbu maana..., kumbe hadi kupeana makochi!.

Yaani mnataka kusema kama sio Mzee Mbowe, Familia ya Nyerere wangekaa chini?!.
PView attachment 1786471View attachment 1786487View attachment 1786489
Ni zawadi wakati wa dhiki, akupaye wa kwanza kumbukumbu zake hubaki milele uzuri ni kwamba aliyesimulia si mtoaji bali mpokeaji
 
Mohamed Said bingwa wa historia ya maswala ya uhuru, utakapokua na muda, tafadhali tuna kuhitaji huku uje kutupa madini kuhusu hili swala.
mzee wetu mohamed said hana interest ya kuzungumzia wazee wa imani tofauti na ile yetu ambao walisaidiana na nyerere katika harakati za kutafuta uhuru.

yeye hujikita zaidi kuzungumzia mchango wa wazee wake wa kariakoo tu. historia ya hao wazee wengine kutoka uchagani na usukumani, sio focus ya mohamed said.

kwa mantiki hiyo, usitegemee maelezo yoyote positive kutoka kwake yanayohusu familia ya mbowe na uhusiano wao na nyerere katika harakati za kutafuta uhuru.
 
Kuna watu wamekuja mjini juzi tu walitaka kujifanya nchi yao wako wapi
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom