Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Kwa Kutumia akili za kawaida tu inaeleweka kwamba vijana waliichoka CCM ya JK kwa kuona matarajio Yao ya maisha bora kwa kila Mtanzania hayakufikiwa. Huu ni ukweli hata CCM wanajua. Ni ukweli pia kwamba Lowassa lengo lake lilikuwa kwenda Ikulu kwa namna yoyote hata kwa kufanya mikataba na Shetani! Ukweli huu wenye akili wanaju!
Ni ukweli pia kwamba 2015 wananchi walihitaji mabadiliko ya kweli siyo ya kubadilisha Chama au kumchagua mtu aliyepania kwenda Ikulu kwa gharama yoyote, ukweli huu wenye akili wanaujua isipokuwa wafuata upepo na wasiojua kuchambua mambo.
Hata hivyo, CHADEMA walifanya kosa kubwa kwa walichokiita Gia ya Angani. Walitaka kumtumia Lowassa kwenda Ikulu wakiwa hawana agenda yoyote Baada ya kuitupa Ajenda ya Ufisadi kwa kumsimamisha mtu waliyetuhubiria kwa miaka 8 kwamba ni fisadi na ni heshima kubwa kwa Mungu kumzomea.
Hapa ndipo ilipodhihirika kwamba kumbe CDM hawana nia ya kuleta mabadiliko bali wanafanya mzaha tu. Hii itawagharimu sana maana wananchi wameshawashtukia Hawa kwa ulaghai wao!
Mabadiliko sio kudeki barabara, kuigiza kuzimia na wala kuzungusha mikono! Kidumu Chama cha Mapinduzi! HAPA KAZI TU!!!!