NI MWISHO WA DEMOKRASIA NA VYAMA VINGI TANZANIA?

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Baada ya nguvu kubwa kutumika kuzuwia kuonesha bunge live na kamati ya Maadili kutumia meno yake kunyamazisha baadhi wabunge mahiri wenye hoja kinzani kwa kuwafukuza bungeni.

Siku chache zilizopita jeshi la polisi Tanzania lilitoa tamko la kuzuwia Mikutano ya Hadhara na Maandamano kwa vyama vya siasa wakisema kwamba taarifa za kiintelijensia zimewalazimisha kufanya hivyo.

Viongozi wa vyama vya siasa walisikia na kuamua kutii amri hiyo na kuamua kupinga amri hiyo ya Polisi kwa kufungua kesi ya kupinga amri hiyo katika mahakama kuu ya Mwanza mwishoni mwa wiki hii.

Kutokana na mikutano ya hadhara na maandamano kuzuiwa vyama na wananchi wameamua kufanya mijadala yao kwa njia nyingine ambazo hazijazuiwa na jeshi la polisi ikiwemo makongamano ya ndani ya kumbi kujadili masuala mbalimbali.

Na mwishoni mwa wiki hii tulipata fursa ya kuona tangazo la chama cha ACT Wazalendo likiwaalika watanzania kushiriki mjadala wa kuchambua Bajeti ya mwaka 2816/2017 katika ukumbi wa LAPF Millenium Towers leo tarehe 12/06/2016 lakini katika Hali lisiyotarajiwa Afisa habari wa chama cha ACT Wazalendo Ndugu Abdallah Khamis anatujulisha kuwa Polisi wamezuwia Kongamano hilo na wameonekana kuzingira eneo la ukumbi tangu saa 12 asubuhi.

Polisi kuzuwia tukio hili muhimu ambalo halikuwemo kwenye katazo Lao la msingi hii linaleta tafsiri gani kwa wapenda demokrasia?
 

Attachments

  • 1465728546209.jpg
    1465728546209.jpg
    58.2 KB · Views: 37
Back
Top Bottom