Ni mwezi gani mzuri wa kuanza ujenzi?

Habarini za muda, kwa wajuzi wa kujenga ni kipindi au muda mwezi gani hali ya hewa ni nzuri kufanya ujenzi (January, February, March, April, may, June, July, August, September, October, November, December)

Karibuni kwa mtazamo wenu.

Location ni Dar es Salaam
Mwisho wa mwezi ama mwanzo wa mwezi baada ya kulipwa mshahara. Kwani wewe ulitakaje?
 
Sijaongelea utegemee mvua kunyeshea ukuta ili upate uimara.

Nimeongelea siment haiwi exposed na mwanga wa jua.

Maana mwanga wa jua unasababisha Sana nyufa na kupunguza uimara wa simenti.

Ukuta unaokauka kivulini unakua imara zaidi kuliko ukuta unaokauka juani.
Hio nakubaliana nawe kabisa. Jua kali ni baya sana kwa simenti.
 
Ansante mkuu watu wanasikia cement inahitaji kumwagilia sana basi wanaona mvua ndokiboko yani mtu ujenge nyumba halafu gharama zakunyeshea zikusumbue nafikiri kama kitu hukijui bora ukatulia ili ujifunze nikweli kunafaida wakati lakin hasara nikubwa zaidi
Binafsi nimejenga sana. Misimu yote ya mwaka. Suala la maji tunamwagilia zaidi hata ya mara nne kwa siku kwa wiki ya kwanza nzima. Baada ya hapo frequency inapungua hadi mara mbili kwa siku. Mafundi nawalipa kwa day, kwa hio mvua zikinyesha huwa inaharibu mfumo sababu mara nyingi wanasimama na kazi haiendi. Pia zege linaharibika au inabidi kifunika kila siku mara tu baada ya kulifanya. Mawe yanatoka sehemu ambazo mafuso hayawezi pita wakati wa mvua. Kwa arusha lakini. Pia matofali ya kuchoma, huwa yanapanda bei sana wakati wa mvua. Nina uzoefu sana, kwa hio usijaribu kuninyamazisha sababu mie siendani na ww.
 
Sijaongelea utegemee mvua kunyeshea ukuta ili upate uimara.

Nimeongelea siment haiwi exposed na mwanga wa jua.

Maana mwanga wa jua unasababisha Sana nyufa na kupunguza uimara wa simenti.

Ukuta unaokauka kivulini unakua imara zaidi kuliko ukuta unaokauka juani.
Lakini majengo nimejenga suala la jua tunalimudu kwa kumwagilia maji mara nyingi kwa siku. Angalia hio post hapo juu nimemjibu member mwingine.. utagundua advantage ya masika ni hilo moja tu. Suala la umwagiliaji. Ambalo linawezekana kutatulika bila shida
 
Hapana mkuu,
Wkt wa mvua Ni rahisi zaidi maana mabondeni mchanga unakua mwingi sana sababu ya kukokotwa na mvua.

Maji unatumia ya mvua.
Swali kuhusu process ya kukusanya mchanga. Wakati mvua zinanyesha za masika ndio mchanga unakusanywa kwa urahisi zaidi au baada ya mvua kuisha?
 
Ansante mkuu watu wanasikia cement inahitaji kumwagilia sana basi wanaona mvua ndokiboko yani mtu ujenge nyumba halafu gharama zakunyeshea zikusumbue nafikiri kama kitu hukijui bora ukatulia ili ujifunze nikweli kunafaida wakati lakin hasara nikubwa zaidi
Suala moja tu la kumwagilia ndio watu mmelikalia sana? Suala ambalo linatatulika kiurahisi? Na ukishapaua plasta zinamwagiliwa na mvua? HAPANA. Na INATAKIWA UMWAGIE HATA MARA NNE AU ZAIDI SIKU ZA KWANZA. Mvua haina ratiba maalum. Bado utamwagilia tu hata kama mvua inanyesha.
 
Binafsi nimejenga sana. Misimu yote ya mwaka. Suala la maji tunamwagilia zaidi hata ya mara nne kwa siku kwa wiki ya kwanza nzima. Baada ya hapo frequency inapungua hadi mara mbili kwa siku. Mafundi nawalipa kwa day, kwa hio mvua zikinyesha huwa inaharibu mfumo sababu mara nyingi wanasimama na kazi haiendi. Pia zege linaharibika au inabidi kifunika kila siku mara tu baada ya kulifanya. Mawe yanatoka sehemu ambazo mafuso hayawezi pita wakati wa mvua. Kwa arusha lakini. Pia matofali ya kuchoma, huwa yanapanda bei sana wakati wa mvua. Nina uzoefu sana, kwa hio usijaribu kuninyamazisha sababu mie siendani na ww.
Umeenda mbali mkuu humu tunaelimishana tu
 
Basi usingejibu kwa madharau ili ujifunze.
Sina sababu yakumdharau mtu yeyeto hum wala mm sio waaina hiyo sikumbuki kama nimewahi kumdharau mtu popote mm sijaelewa hii imekujaje mbona nimeanza kushukuru kwamchango wako mzuri basi ndugu nisamehe tu yaishe
 
Feb had May ni muda mzuri kujenga
1.Bei za bidhaa zinakuwa nafuu kwasababu miezi hiyo shughuli za ujenzi sio nyingi hivyo kanuni za uchumi hapa Demand and supply zitasaidia ktk kununua material kwa bei nafuu.

2.Urahisi wa kupata fundi &bei inakuwa rahisi kubargain
Coz feb to May hakunaga kazi nyingi za ufundi hivyo mafundi wengi huwa wako idle na hukubwa na matatizo ya kifedha miezi hiyo hivyo ni rahisi kupata fundi mzuri kwa bei nafuu.

3.Uhakika wa upatikanaji wa maji kwa ajili ya kujengea,maji ya mvua yatakusaidia sana kupunguza gharama ya maji ya kujengea

4.Vibarua nao huwa wengi tuu coz miezi hiyo wengi hupata vibarua kwa shida hivyo unauwezo wa kuwapata na kuamua namna ya kuwalipa(bargain power)
 
Back
Top Bottom