Ni mwezi gani mzuri wa kuanza ujenzi?

abel frank

Senior Member
Apr 11, 2013
165
225
Habarini za muda, kwa wajuzi wa kujenga ni kipindi au muda mwezi gani hali ya hewa ni nzuri kufanya ujenzi (January, February, March, April, may, June, July, August, September, October, November, December)

Karibuni kwa mtazamo wenu.

Location ni Dar es Salaam
Habari waluu,
Kimsimgi ujenzi ni wakati wowote, tena masika inakuwa nzuri saana kwani hupunguza gharama na usumbufu japo baadhi ya maeneo upatikanaji wa mchanga waweza kuwa issue kwa udogo.

Wakati huu wa masika matumizi ya maji ni kifogo sana,na hupunguza gharama.

Wakati wa masika watu wengi huwa kwenye kilimo na pirikapilika nyingi na kufanya shughuli za ujenzi kupu gua, hivyo mafundi wanakuwa benchi kwa muda mrefu,hii huwafanya mafundi kuhitaji kazi ,so ukiwakuta benchi unaweza kuwapata kwa Bei kidiogo.
Kuna mtu anaweza kusema mjini nako kilimo kipo?
Miji mikubwa inalishwa na miji midogo/vijiji, wafanya biashara wa mjini hupata mazao kwa uchache kutokana na upatikani.

Ndo maana hata sisi UVIMO tumetoa ofa ya punguzo za ujenzi, finishing,kupaua, kuchimba mashimo na mifumo ya maji Safi na taka kwa kuzingatia sababu hii.
Hii ni kuepuka kukakaa muda mwing bila kazi.

Hapa chini ni kazi inayo endelea (14-Feb-21) hapa Chamazi

Mkuu, UVIMO tunaomba hiyo kazi, tutalifanyia bei rafiki kwa muda mfupi utakabidhiwa kazi yako na TUTAKUACHIA FURAHA.

Tafadhali tuwasiliane
0753961896
0629361896

.
IMG-20210110-WA0012.jpg
 
kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
1,263
2,000

. View attachment 1676973
Shukrani mkuu
 
mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
291
500
Kwaiyo mkuu mwezi wa pili naweza kuanza bila shida yeyote ya mvua kwa Dar es salaam???
Boss, karibu sana katika chama cha wababa wanaojenga. Mimi niliona nijenge miezi michache kabla mvua hazijaanza ili zinisaidie kumwagilia na kukomaza kuta na msingi.

Anza mwezi ambao unakaribia na mvua hivi mvua zitamwagilia nyumba yako itakomaa vizuri sana, kumbuka pia nyumba inabidi inywe sana maji hasa kifusi utakachoweka ndani, hivyo vizia muda niliosema.
 
kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
1,263
2,000
Boss, karibu sana katika chama cha wababa wanaojenga. Mimi niliona nijenge miezi michache kabla mvua hazijaanza ili zinisaidie kumwagilia na kukomaza kuta na msingi. Anza mwezi ambao unakaribia na mvua hivi mvua zitamwagilia nyumba yako itakomaa vizuri sana, kumbuka pia nyumba inabidi inywe sana maji hasa kifusi utakachoweka ndani, hivyo vizia muda niliosema.

Ambao ni mwezi upi mkuu???? Ebu niambie
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,634
2,000
Ambao ni mwezi upi mkuu???? Ebu niambie

Mwezi February.
Majira ya mvua kwa mikoa ya Mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi ni mwezi March -June
Kisha mwezi September-December mara chache hadi Januari

Miezi isiyo na mvua ni February, July, August.
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,634
2,000
Ujenzi wa kipindi cha mvua unaweza kukusaidia kuchukua tahadhari wakati wa ujenzi iwapo eneo husika litakuwa na changamoto ya matharani maji maji, Mkondo wa maji, bonde , n.k
Itasaidia kujua kiwango cha msingi n.k
 
Kayaula Musa

Member
Jan 2, 2020
78
125
Sababu ya kusema mvua itapunguza gharama za kunyeshea sidhani kama zinamashiko sana itategemea nimvua zipi maana cementi ikipata maji mengi kabla ya mda wake ubora unapungua
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
10,722
2,000
Hichohicho nasikiaga gharama zinakuwaga nafuu sana tofauti na miezi mingine.

Wajuzi watakupa taarifa zaidi.
Ilo Ni kweli,
1.Kipind iki material zinauzwaga Bei rahisi maana mzunguko wa biashara unakuaga mdogo.

2.Pia, mafundi wanafanya kazi kwa Bei rahisi sababu kazi za ujenz zinakua chache.

3.upatikanaji wa maji na mchanga unakua rahisi zaidi sababu ya mvua zinazonyesha.

4. Cement inashika vizur zaidi sababu ya unyevu unyevu unyevu wa kutosha.
 
DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
658
1,000
Habarini za muda, kwa wajuzi wa kujenga ni kipindi au muda mwezi gani hali ya hewa ni nzuri kufanya ujenzi (January, February, March, April, may, June, July, August, September, October, November, December)

Karibuni kwa mtazamo wenu.

Location ni Dar es Salaam
Achana na jamaa aliyekuambia eti masika. Wakati wa mvua kila kitu hasa matofali, mawe, mbao nk vinakuwa juu sababu usafirishaji wake, uaandaaji wake nk unakuwa uko juu sana. Mfano matofali yasipofunikwa yanaharibika, barabara za misituni mbao na mawe nk vinapopatikana zinakuwa mbovu. Zaidi ya hayo, hata kazi zako zinawexa haribiwa na mvua mfano zege BICHI nk. Pia mafundi hawataweza fanya kazi kwenye mvua. Na kazi itazorota sana.
Kwa hio wakati wa kiangazi ni mzuri zaidi. Japo kwa kazi za cement itabidi baada ya kukauka masaa 24 ya mwanzo, umwagilie sana sababu jua nalo linavuruga uimara wa cement. Mvua inaharibu masaa 24 ya mwanzo tokea zege limwagwe.
 
DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
658
1,000
Ilo Ni kweli,
1.Kipind iki material zinauzwaga Bei rahisi maana mzunguko wa biashara unakuaga mdogo.

2.Pia, mafundi wanafanya kazi kwa Bei rahisi sababu kazi za ujenz zinakua chache.

3.upatikanaji wa maji na mchanga unakua rahisi zaidi sababu ya mvua zinazonyesha.

4. Cement inashika vizur zaidi sababu ya unyevu unyevu unyevu wa kutosha.
Maji na mchanga ni baada ya mvua kuisham sio wakati wa hizo mvua mkuu.
 
DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
658
1,000
Ilo Ni kweli,
1.Kipind iki material zinauzwaga Bei rahisi maana mzunguko wa biashara unakuaga mdogo.

2.Pia, mafundi wanafanya kazi kwa Bei rahisi sababu kazi za ujenz zinakua chache.

3.upatikanaji wa maji na mchanga unakua rahisi zaidi sababu ya mvua zinazonyesha.

4. Cement inashika vizur zaidi sababu ya unyevu unyevu unyevu wa kutosha.
Simenti kushika si unamwagilia tu maji MENGI matotali?
 
Kayaula Musa

Member
Jan 2, 2020
78
125
Achana na jamaa aliyekuambia eti masika. Wakati wa mvua kila kitu hasa matofali, mawe, mbao nk vinakuwa juu sababu usafirishaji wake, uaandaaji wake nk unakuwa uko juu sana. Mfano matofali yasipofunikwa yanaharibika, barabara za misituni mbao na mawe nk vinapopatikana zinakuwa mbovu. Zaidi ya hayo, hata kazi zako zinawexa haribiwa na mvua mfano zege BICHI nk. Pia mafundi hawataweza fanya kazi kwenye mvua. Na kazi itazorota sana.
Kwa hio wakati wa kiangazi ni mzuri zaidi. Japo kwa kazi za cement itabidi baada ya kukauka masaa 24 ya mwanzo, umwagilie sana sababu jua nalo linavuruga uimara wa cement. Mvua inaharibu masaa 24 ya mwanzo tokea zege limwagwe.
Ansante mkuu watu wanasikia cement inahitaji kumwagilia sana basi wanaona mvua ndokiboko yani mtu ujenge nyumba halafu gharama zakunyeshea zikusumbue nafikiri kama kitu hukijui bora ukatulia ili ujifunze nikweli kunafaida wakati lakin hasara nikubwa zaidi
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
10,722
2,000
Ansante mkuu watu wanasikia cement inahitaji kumwagilia sana basi wanaona mvua ndokiboko yani mtu ujenge nyumba halafu gharama zakunyeshea zikusumbue nafikiri kama kitu hukijui bora ukatulia ili ujifunze nikweli kunafaida wakati lakin hasara nikubwa zaidi
Sijaongelea utegemee mvua kunyeshea ukuta ili upate uimara.

Nimeongelea siment haiwi exposed na mwanga wa jua.

Maana mwanga wa jua unasababisha Sana nyufa na kupunguza uimara wa simenti.

Ukuta unaokauka kivulini unakua imara zaidi kuliko ukuta unaokauka juani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom