Ni mwandishi gani wa Maisha, Mahusiano na Fasheni anayekuvutia

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Kwa miaka kadhaa sasa tumekuwa na magazeri na majarida mbalimbali ya mambo ya maisha. Wapo waandishi wa magazeti yale ya zamani na hata kwenye mitandao. Najaribu kutaka kuwasoma baadhi ya waandishi maarufu wa mambo haya wkani wale wa kisiasa wengi wanafahamika. Je kwenye masuala ya maishe (lifestyle), mahusiano (relationship) na hata mitindo (fashion) ni wachache wanafahamika au wanafahamika kwa kundi la watu wachache.

Naomba kwa wale wanaowasoma hawa watu (nazungumzia waandishi wa Kitanzania) tushirikishane:

a. Ni kina nani?
b. Wanaandika eneo gani
c. Wanaandikia kwenye magazeti gani?
d. Kwanini wanakuvutia?
e. Ni gazeti gani la mambo haya linalokuvutia zaidi na kwanini?
f. Na wanaandika kwa lugha gani zaidi - Ningependa wale ambao pia wako very fluent katika Kiingereza au hata Kifaransa!

MMM
 
kuna Mwandishi anajiita Mabala wa Mabalaa, ana page yake Gazeti la Raia Mwema(kila wiki J5) inaitwa Aya za Ayah Binti Hidaya. sina uhakika kama ni yule Richard Mabala. But ni kind ya hadithi flani hivi za kufikirika za maisha ya kila siku zinasisimua kusoma.
 
Jamani nataka tuweze kuwatambua dada zetu na hasa wanaondika kuhusu maisha yetu. Hata kama yuko nje ya Tanzania lakini ni Mtanzania.. Yawezekana kuwa labda ni kuwa kina dada zetu hawapati nafasi zaidi? Au labda niulize pia labda kuna dada ambaye anapenda sauti yake isikike katika mambo kama haya na hajapata nafasi?
 
Kuna huyu jamaa anaitwa Dismas Lyassa. Uwa anajitahidi kuandika kuhusu mahusiano katika magazeti ya Mwananchi na Mwanaspoti.

Kuna Maimuna Kubegeya, uwa anaandika juu ya mitindo katika gazeti la Mwananchi-Jumapili.

Pia kuna mama anaitwa Asumpta Nalitolela, nae anaandika katika Mwananchi-Jumapili; uwa anaandika makala nzuri juu ya maisha kiujumla.
 
Asante sana.. kwa kweli majina mengi ndio yanasikia leo.. unajua kuna watu wanasema "avumaye baharini papa..."
 
kuna Mwandishi anajiita Mabala wa Mabalaa, ana page yake Gazeti la Raia Mwema(kila wiki J5) inaitwa Aya za Ayah Binti Hidaya. sina uhakika kama ni yule Richard Mabala. But ni kind ya hadithi flani hivi za kufikirika za maisha ya kila siku zinasisimua kusoma.

Mkuu uko right huyo ndo yule richard mabala, mzee wa yale mashindano ya drama. Ni Mtanzania mzungu, mwenyewe anajiita msukuma
 
Jamani nataka tuweze kuwatambua dada zetu na hasa wanaondika kuhusu maisha yetu. Hata kama yuko nje ya Tanzania lakini ni Mtanzania.. Yawezekana kuwa labda ni kuwa kina dada zetu hawapati nafasi zaidi? Au labda niulize pia labda kuna dada ambaye anapenda sauti yake isikike katika mambo kama haya na hajapata nafasi?
..hapa JF yupo AshaDii. Ni Mwandishi, ila anajiita Mstaafu.
Amewahi ku-publish kazi yake mwenyewe, ingawa sijafanikiwa kuiona. Labda akija hapa atafafanua zaidi
 
sasa nimmmepata mwangaza, nampenda Ndyoko, Bujibuji na Rev. Masanilo

kweli kama huu ndio mwangaza ni kazi.. imebidi nifafanue zaidi maana hivi hivi inaweza kuzunguka kweli. Angalia sehemu ya "c" hapo juu ili kufuata maelekezo kwa kina.
 
Inawezekana kwamba hatuna waandishi wanaovutia au dada zetu wao wanasoma hadithi tu lakini siyo vitu vya makini na vya kina?
 
Jamani nataka tuweze kuwatambua dada zetu na hasa wanaondika kuhusu maisha yetu. Hata kama yuko nje ya Tanzania lakini ni Mtanzania.. Yawezekana kuwa labda ni kuwa kina dada zetu hawapati nafasi zaidi? Au labda niulize pia labda kuna dada ambaye anapenda sauti yake isikike katika mambo kama haya na hajapata nafasi?

Mimi hapa....can you help???
 
Back
Top Bottom