Ni mwanasiasa gani anaekuvutia katika siasa zake?

KOSAM

Member
May 25, 2013
43
5
Habarin wanabodi.... Kumekuwepo na wanasiasa wengi katika vyama mbali mbali wamekuwa wakitumia nguvu nyingi ikibidi na pesa kuwavutia wananchi kujiunga na vyama vyao vya siasa pasipo ya wao kujua siasa zao zinawavutia wananchi? Sasa nawaomba tujue je ni wanasiasa/mwanasiasa gani mwenye mvuto kwa sasa na anatoka chama gani?:: haya sasa wanabodi kazi kwenu... Tupieni jina na chama chake
 
Mwigulu Nchemba, CCM. Jamaa ana akili sana mpaka katengeneza movie ya njama za mauaji. Chezea CCM wewe?
 
Mwigulu chembaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Rev.Christopher Mtikila, huyu jamaa anaweza kutamka hisia zake bila ya kujali hisia za wengine, tafuteni Mtanzania ya jana tareh 9 june, 2013. Anaelezea jinsi anavounga mkono watu wa kusini kujitenga tena anataka mpaka uwe Reli ya Kati,anakosoa unafik w Watanzania kiasi cha kufikia ukitaka usimame kidete uwatetee sharti uwahonge ili wakuunge mkono. Baadhi ya misimamo yake siikubali ila napenda alivyo muwazi kiasi cha kufanya aeleweke siasa zake badala ya kuwa vugu vugu kama walivyo wasnii wetu wa kisiasa!
 
Anne Makinda kwa kulifanya bunge kama NGO yake
Madelu Nchemba na Lusinde kwa kuibomoa CCM
Nape kwa kuropoka
 
Navutiwa sana na utendaji wa Tundu Lissu,ana msimamo kwa jambo analoliamini,IQ yake iko juu,ni msafi na kwa namna anavowasumbua CCM angekuwa na tuhuma yoyote hakika angekoma! Amwombe sana mwenyezi Mungu awe ndiye mlinzi wake nami namwombe maisha marefu! Nadhani huyu bwana ndiye MUSA wetu
 
Back
Top Bottom