Bandari inaanzia mlingotini mpaka zinga. Haya maeneo ndiyo ya kuwahi kuwekeza nyumba za kupanga na lodge kwa ajili ya wageni na wafanya kazi wa bandari. Changamkieni fursa mapema
Acha wahuni waendelee kubwabwaja humu mitandaoni wengine wanawekeza ama kuangalia maeneo potential kwa uwekezaji.
 
Tokea upate ufahamu ulishawahi kuonyeshwa mikataba hadharani ama unajisemea tu…Jiwe aliamua kuwa muwazi period… maana hili swala la Tanzania kufanywa kichwa cha mwendawazimu kilimkera sana, mara kwa mara alikuwa anasema tumechezewa sana…imetosha

sasa km wewe ni tomaso subiria nchi iuzwe hii uchakae…ukafikiria ni watu wote wako kwa ajili ya maslahi yako…
Jamaa yako alisemaga eti gase imeuzwa,, nduguzanguni wakristo tuache roho za kwanini,, akifanya muislamu sawa akifanya mkirsto iwe sawa. Roho za kwanini hazijengi,, SSH angeweza kusitisha ununuzi wa ndege, kwani ni mradi wa jpm, au angesitisha bwawa la nyerere richa ya kuwa ni uwekezaji ambao hauna garantii ya hali ya hewa, lakini hana roho ya kwanini. Eti mradi ukikamilika atasifiwa jpm na si yeye,,
Tuacheni roho za kwanini na ubinafsi,, kwani mradi wa gase na huu wa bandari ya bagamoyo itatoa nafuu sana kwa kuchumi,
Waliodai eti gase kauziwa mchina , wataumbuka tu with time,
TOTAL kwa kuanzia ni kampuni ya UK kama sikosei
 
Unasema kikwete kuweka Jiwe la msingi inamaanisha kulikuwa na Mkataba alafu huweki huo mkataba!

Wewe ni sukuma gang tu! Hamna ushahidi kazi kupoteza muda humu kushambulia miradi anayofanya Mama Samia
Mi mjumbe tu
Kama mkataba haukusainiwa, lile jiwe la Msingi ni la nini?
 
dah nilitaka kuuziwa kiwanja hapo ukuni kikubwa kweli kwa bei yakutupa nikadharau... dah leo bei zitakuwa balaa......

Tuache siasa, hatuwawezi hawa wanasiasa wetu washatushinda na sisi ni majibwa koko tu....sisi tutafute fursa zilizopo na sisi tufanye yetu..
Mkuu njoo PM kama bado unahitaji.
 
Tokea upate ufahamu ulishawahi kuonyeshwa mikataba hadharani ama unajisemea tu…Jiwe aliamua kuwa muwazi period… maana hili swala la Tanzania kufanywa kichwa cha mwendawazimu kilimkera sana, mara kwa mara alikuwa anasema tumechezewa sana…imetosha

sasa km wewe ni tomaso subiria nchi iuzwe hii uchakae…ukafikiria ni watu wote wako kwa ajili ya maslahi yako…
Kama jamaa yako alikuwa na mapenzi ya dhati na nchi hii alitakiwa kuweka wazi mkataba mzima ili tuone mapungufu na faida.
Nijuavyo maana ya mkataba kuna utakachopata na ambacho utapoteza.
Magufuli aliorodhesha hasara lakini hakutaja faida hata moja.
Haiwezekani mkataba mzima ulikuwa wa kupoteza kila kitu.

Hata hivyo hilo halishangazi sana ,maana Magufuli alikuwa na ubinafsi mwingi.
Hivi ni uzalendo gani aliotumia kujenga uwanja wa ndege Chato badala ya Geita.
Geita ni karibu na Sengerema, Kahama, Ushirombo, Katoro, Mbogwe nk, lakini kwa kuwa alikuwa mbinafsi hakuona hasara ya kwenda kuteketeza hela za walipa kodi kijijini kwao Chato.
 
Nimeona wengi wakimshutumu Mwambe, lakini inawezekana Mwambe akawa yupo sawa Ila kikwete ndio aliongopa.
Tarehe 17/10/2015 ilifanyika hafla ambapo raisi mstaafu J Kikwete alizindua jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya bagamoyo.
Hadi kufikia hatua ya kuweka jiwe la Msingi tafsiri rahisi ni kuwa mmeshakubaliana (mkataba) kuanza ujenzi.
Sasa hivi Mwambe anasema hakuna mkataba uliosainiwa bali ilikua muhtasari tu wa vikao, sasa Cha kujiuliza lile jiwe walilozindua raisi kikwete pamoja na wale wachina ilikua geresha?
Au inawezekana pia raisi kikwete alituongopea, lile jiwe la Msingi halikua kwa ajili ya bandari ya bagamoyo.
Ni nani mkweli Kati ya kikwete na Mwambe?
Chini nimeweka clip ya you tube kikwete alizindua hilo jiwe la msingi

View attachment 2016527

Heshima mkuu kwa uwasilishaji wa mada wenye mantiki.

Ni wazi kuna uongo mwingi sana unaotembezwa kwenye mradi huu. Lazima kuna sababu za uwepo wa mkanganyiko mkubwa kiasi hiki. Hii ni dalili za juhudi za kuficha madudu yanayoambatana na mradi huu.
Hizi sio dalili nzuri hata kidogo.
 
dah nilitaka kuuziwa kiwanja hapo ukuni kikubwa kweli kwa bei yakutupa nikadharau... dah leo bei zitakuwa balaa......

Tuache siasa, hatuwawezi hawa wanasiasa wetu washatushinda na sisi ni majibwa koko tu....sisi tutafute fursa zilizopo na sisi tufanye yetu..
Unawasaliti waTanzania wenzako wasiokuwa na mianya ya kufanya hayo unayotarajia kuyafanya wewe. Upo tayari kuwauza, kama wanavyouzwa na hawa wanasiasa unaosema tuachane nao.
Wewe na wanasiasa hamtofautiani chochote, ni maadui wakubwa wa wananchi wa Tanzania.
 
Mama Samia na watu wake wanatafuta gea zote za kuhalalisha hii Bandari. Kumbe Magufuli alikumbuka na hii kadhia ndiyo maana akawa anasema ni mkataba wa kipumbavu.
Tumkumbuke sana huyu mwamba,miaka 99 inakuwaje mkataba huo.
Tumerudi kulekule twendeni tu.
 
Sasa tulitegemea serikali ya Samia Suluhu ije na kauli kuwa, imeamua kufufua ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambao mkataba wake ulizuiwa kutekelezwa na Magufuli.
Na Samia akiondoka akaja mzalendo kama Magufuli kuna uhakika gani kuwa hayo makubaliano ya huo ujenzi yatasalimika?
Waweke wazi huo mkataba wananchi wauone !
 
Nimeona wengi wakimshutumu Mwambe, lakini inawezekana Mwambe akawa yupo sawa Ila kikwete ndio aliongopa. Tarehe 17/10/2015 ilifanyika hafla ambapo raisi mstaafu J Kikwete alizindua jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo...
Wote wanaweza kuwa waongo. Kwani lazima wanasiasa ndiyo wafikiri kwa niaba ya wananchi kana kwamba wananchi hawana akili na wanasiasa ndiyo wenye akili tu.
 
Kama jamaa yako alikuwa na mapenzi ya dhati na nchi hii alitakiwa kuweka wazi mkataba mzima ili tuone mapungufu na faida.
Nijuavyo maana ya mkataba kuna utakachopata na ambacho utapoteza.
Magufuli aliorodhesha hasara lakini hakutaja faida hata moja.
Haiwezekani mkataba mzima ulikuwa wa kupoteza kila kitu.

Hata hivyo hilo halishangazi sana ,maana Magufuli alikuwa na ubinafsi mwingi.
Hivi ni uzalendo gani aliotumia kujenga uwanja wa ndege Chato badala ya Geita.
Geita ni karibu na Sengerema, Kahama, Ushirombo, Katoro, Mbogwe nk, lakini kwa kuwa alikuwa mbinafsi hakuona hasara ya kwenda kuteketeza hela za walipa kodi kijijini kwao Chato.

Naamini madini yanathamani kubwa sana ulimwenguni… sasa katika sekta ya madini mikataba haikuwa wazi…umefaidika nini na huo uwekezaji…

Jamaa kajitoa muhanga kusema ukweli mnaanza kuquestion…shida zimetuzunguka kila kona huna umeme, huna maji, huna hela, tozo zimekuzunguka, madarasa hatuna, dawa hospitalini huna bado mnakimbilia wawekezaji ambao tokea waanze kuja hakuna mabadiliko yoyote kwa maisha ya mtanzania shida ni zilezile…unabaki kuquestion mikataba ambayo mmeshaonyeshwa wazi jinsi tunavyochezewa…faida unazozitaka zipi wakati kashakwambia TRA hawataruhusiwa kusimamia mapato au za mama ntilie na vibarua kupata ajira…

Hv tumelogwa!
 
Mkuu haya yote ni sera mbovu za maraisi wa ccm na viongozi wengine huku bunge letu nalo nikiwa dhaifu na hovyo kabisa.
 
Unasema kikwete kuweka Jiwe la msingi inamaanisha kulikuwa na Mkataba alafu huweki huo mkataba!

Wewe ni sukuma gang tu! Hamna ushahidi kazi kupoteza muda humu kushambulia miradi anayofanya Mama Samia
Sio miradi ya Mama tu bali ni miradi ya TAIFA JUA HILO KWANZA
 
Back
Top Bottom