Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,855
2,000
Nimeona wengi wakimshutumu Mwambe, lakini inawezekana Mwambe akawa yupo sawa Ila kikwete ndio aliongopa. Tarehe 17/10/2015 ilifanyika hafla ambapo raisi mstaafu J Kikwete alizindua jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo...
Wote wanaweza kuwa waongo. Kwani lazima wanasiasa ndiyo wafikiri kwa niaba ya wananchi kana kwamba wananchi hawana akili na wanasiasa ndiyo wenye akili tu.
 
Micho

JF-Expert Member
Apr 12, 2009
544
500
Kama jamaa yako alikuwa na mapenzi ya dhati na nchi hii alitakiwa kuweka wazi mkataba mzima ili tuone mapungufu na faida.
Nijuavyo maana ya mkataba kuna utakachopata na ambacho utapoteza.
Magufuli aliorodhesha hasara lakini hakutaja faida hata moja.
Haiwezekani mkataba mzima ulikuwa wa kupoteza kila kitu.

Hata hivyo hilo halishangazi sana ,maana Magufuli alikuwa na ubinafsi mwingi.
Hivi ni uzalendo gani aliotumia kujenga uwanja wa ndege Chato badala ya Geita.
Geita ni karibu na Sengerema, Kahama, Ushirombo, Katoro, Mbogwe nk, lakini kwa kuwa alikuwa mbinafsi hakuona hasara ya kwenda kuteketeza hela za walipa kodi kijijini kwao Chato.

Naamini madini yanathamani kubwa sana ulimwenguni… sasa katika sekta ya madini mikataba haikuwa wazi…umefaidika nini na huo uwekezaji…

Jamaa kajitoa muhanga kusema ukweli mnaanza kuquestion…shida zimetuzunguka kila kona huna umeme, huna maji, huna hela, tozo zimekuzunguka, madarasa hatuna, dawa hospitalini huna bado mnakimbilia wawekezaji ambao tokea waanze kuja hakuna mabadiliko yoyote kwa maisha ya mtanzania shida ni zilezile…unabaki kuquestion mikataba ambayo mmeshaonyeshwa wazi jinsi tunavyochezewa…faida unazozitaka zipi wakati kashakwambia TRA hawataruhusiwa kusimamia mapato au za mama ntilie na vibarua kupata ajira…

Hv tumelogwa!
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
13,329

Mkuu haya yote ni sera mbovu za maraisi wa ccm na viongozi wengine huku bunge letu nalo nikiwa dhaifu na hovyo kabisa.
 
All TRUTH

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
5,173
2,000
Unasema kikwete kuweka Jiwe la msingi inamaanisha kulikuwa na Mkataba alafu huweki huo mkataba!

Wewe ni sukuma gang tu! Hamna ushahidi kazi kupoteza muda humu kushambulia miradi anayofanya Mama Samia
Sio miradi ya Mama tu bali ni miradi ya TAIFA JUA HILO KWANZA
 
Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
1,221
2,000
Si kuna watu wa mjini walilipwa fidia? Sasa ilikuwaje watu wakalipwa fidia bila mkataba? Mbona tunadanganyana?
 
Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
3,120
2,000
Kikwete akiwa rais wa Tanzania aliweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Hiyo ina maana kuwa majadiliano yalishafanyika, mkataba ulishasainiwa, bajeti ya pesa ilishatengwa, utekelezaji wake ulishaanza!

Alipoingia Magufuli akasema amesitisha ujenzi (utelekezaji) wa bandari ya Bagamoyo kwa sababu mkataba ule ulikuwa haina maslahi kwa Tanzania.

Sasa tulitegemea serikali ya Samia Suluhu ije na kauli kuwa, imeamua kufufua ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambao mkataba wake ulizuiwa kutekelezwa na Magufuli.
Ulikuwa unamuamini kweli mtu yule?
 
Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
3,120
2,000
Si kuna watu wa mjini walilipwa fidia? Sasa ilikuwaje watu wakalipwa fidia bila mkataba? Mbona tunadanganyana?
Watu mbona mnachanganya mambo, sasa watu kulipwa fidia kea eneo kutaka kutwaliwa ndio kunahitaji mkataba wa ujenzi wa Bandari? Hiyo inaweza kuwa sehemu ya roadmap ya utekelezaji tu haina connection na mkataba wa ujenzi wa Bandari. Tafadhali msichangaye mambo.
 
Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
1,890

Na jiwe la Msingi mlilozindua? Napo mkataba ulikua bado? Acheni uongo bana
Huwezi kuweka na kuzindua jiwe la Msingi ikiwa hamjakubaliana
Yanaanza makubaliano(mkataba) ndio inafata kuweka jiwe la Msingi, alafu ujenzi ndio unaanza.
Yaani kabisa uanze kufyeka na kuweka mipaka ya shamba kabla ya kulinunua?
 
Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
3,521
2,000
Mkuu hata una uandishi mbaya kiasi hiki? Hauzijui Nomino?

Ona huyu nae,hizo nomino ndiyo zimefuta mantiki ya hoja zake? Nilidhani unasoma hoja zake kumbe umeng’ang’ana na nomino kama mwalimu wa kiswahili darasa la nne.
 
residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,727
2,000
Mwambe hajawahi kugombea ubunge aliteuliwa na Magufuli kuwa mbunge kisha waziri kwa hiyo ana ushamba fulani wa madaraka.
Kibunda alichohongwa kimemzuzua kweli kweli
Mwambe ni CDM!!??
CCM hakuna kiongozi.
CCM na ufisadi ni binadamu na damu.
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
6,107
2,000
Kama JPM alikuwa anasema yaliyokweli kwann na yeye huo mkataba wa bandari ya bagamoyo hakuuweka wazi. Mbona na yeye alikuwa anaingua mikata ya Siri Hadi leo wananchi hatuijui? Kizazi kilekule cha Panya ila ndio viongozi tofauti hamna jipya
Huwa nawadharau sana watu walikuwa wanamuamini Magufuli, hili lazima niliweke wazi. Magufuli aliponda mikataba ya Bandari ya Bagamoyo na Gesi ya Mtwara bila kuiweka wazi. Lakini MAGUFULI huyo huyo akatumia Matrilioni ya fedha za walipa Kodi wa Tanzania kujenga miundombinu mikubwa na isiyo na tija wilayani Chato bila idhini ya Bunge.

UKIWA na AKILI huwezi kufanya reference kwa kauli za MAGUFULI. He was jealous and a diasaster. Nafuu ALIKUFA mapema kabla jajatupeleka pabaya sana
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,159

Mradi gani uliojengwa kwa matrillion chato? Tafadhali naomba unitajie
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
6,107
2,000
Mradi gani uliojengwa kwa matrillion chato? Tafadhali naomba unitajie
Jumlisha gharama za kujenga Chato Airport, CHato Referral Hospital, Chato Burigi National Park, VETA Chato, Chato Stadium, Chato Port etc
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,159
2,000
Jumlisha gharama za kujenga Chato Airport, CHato Referral Hospital, Chato Burigi National Park, VETA Chato, Chato Stadium, Chato Port etc
Unaijua trillion? Burigi national park?national park toka lini ikajengwa?
Chato stadium? Hizi story huwa mnazitoa wapi?
Chato port? Hata huko chato.unapajua kweli?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom