Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
1,876
2,000
Nimeona wengi wakimshutumu Mwambe, lakini inawezekana Mwambe akawa yupo sawa Ila kikwete ndio aliongopa. Tarehe 17/10/2015 ilifanyika hafla ambapo raisi mstaafu J Kikwete alizindua jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Hadi kufikia hatua ya kuweka jiwe la Msingi tafsiri rahisi ni kuwa mmeshakubaliana (mkataba) kuanza ujenzi. Sasa hivi Mwambe anasema hakuna mkataba uliosainiwa bali ilikua muhtasari tu wa vikao, sasa Cha kujiuliza lile jiwe walilozindua raisi kikwete pamoja na wale wachina ilikua geresha?

Au inawezekana pia raisi kikwete alituongopea, lile jiwe la Msingi halikua kwa ajili ya bandari ya bagamoyo.

Ni nani mkweli Kati ya kikwete na Mwambe?

Chini nimeweka clip ya you tube kikwete alizindua hilo jiwe la msingiScreenshot_20211119-181127_1.jpg
 

Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,140
2,000
Mtoa Mada ungeweka na Mifano pamoja na tafsiri kuwa kuweka jiwe la msingi ni sehemu ya mkataba. Mbio za mwenge au waziri fulani huwa wanaweka mawe ya msingi kwa ujenzi fulani na inakuwa kwenye michoro tu, badaye ndiyo hutafuta pesa au mwekezaji, wakikubaliana na mwekezaji ndiyo mkataba husainiwa.

Je, unafahamu kuwa michiro ya bandari ya bagamoyo imechorwa na serikali ya Tanzania au China,ukilifahamu Hilo ndiyo utajua nini maana ya jiwe la msingi.
 

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,503
2,000
Kama JPM alikuwa anasema yaliyokweli kwann na yeye huo mkataba wa bandari ya bagamoyo hakuuweka wazi. Mbona na yeye alikuwa anaingua mikata ya Siri Hadi leo wananchi hatuijui? Kizazi kilekule cha Panya ila ndio viongozi tofauti hamna jipya
Ungejua kama huo mkataba ni wa kipumbavu kama angefanya siri?
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,055
2,000
dah nilitaka kuuziwa kiwanja hapo ukuni kikubwa kweli kwa bei yakutupa nikadharau... dah leo bei zitakuwa balaa......

Tuache siasa, hatuwawezi hawa wanasiasa wetu washatushinda na sisi ni majibwa koko tu....sisi tutafute fursa zilizopo na sisi tufanye yetu..
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,705
2,000
Kikwete akiwa rais wa Tanzania aliweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Hiyo ina maana kuwa majadiliano yalishafanyika, mkataba ulishasainiwa, bajeti ya pesa ilishatengwa, utekelezaji wake ulishaanza!

Alipoingia Magufuli akasema amesitisha ujenzi (utelekezaji) wa bandari ya Bagamoyo kwa sababu mkataba ule ulikuwa haina maslahi kwa Tanzania.

Sasa tulitegemea serikali ya Samia Suluhu ije na kauli kuwa, imeamua kufufua ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambao mkataba wake ulizuiwa kutekelezwa na Magufuli.
 

Donkey

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
1,140
2,000
dah nilitaka kuuziwa kiwanja hapo ukuni kikubwa kweli kwa bei yakutupa nikadharau... dah leo bei zitakuwa balaa......

Tuache siasa, hatuwawezi hawa wanasiasa wetu washatushinda na sisi ni majibwa koko tu....sisi tutafute fursa zilizopo na sisi tufanye yetu..
Bandari inaanzia mlingotini mpaka zinga. Haya maeneo ndiyo ya kuwahi kuwekeza nyumba za kupanga na lodge kwa ajili ya wageni na wafanya kazi wa bandari. Changamkieni fursa mapema
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom