Ni Mwakyembe au Magufuli kupewa wizara ya Maliasili na utalii

Kwani hadi Kagasheki kutungiwa zengwe ni nini?? Ni baada ya kukamata meno ya tembo ya wakubwa Dar, bado kafuata mengine Zanzibar ambako hawana hata mbuga ya swala, hebu kwa mwenye kufuatilia atuambie hapa, wale Wachina waliokamatwa na meno ya tembo Dar wako wapi? Au wale ws Zanzibar wako wapi? Means Kagasheki aliingilia seal za wakubwa.
Kumtoa Dr Harison uchukuzi itaharibu utaratibu mzima wa kufufua reli, na huenda ikafanyika maksudi ili malori ya wakubwa yafanye deal. Magufuli can go anywhere, huyu ni kiherehere hana lolote.
 
Source Jambo Leo

Imesemekana kuwa kwa kuwa Jk karudi yoka USA kuchunguzwa afya sasa wapambe wake wanasema inawezekana wizara ngumu iliyomwondoa Kaghasheki kuna hati hati kupewa Dr. Maghufuli au Dr. Mwakyembe kutokana na utendendaji wao au ikishindikana atarudishwa bwana Maige
Ili kumaliza ugonjwa,mmoja wao angepewa uwaziri mkuu kabisa hapo ndo nigesema kutapatikana suluhisho.
Hili la kuwaamisha toka wizara moja kwenda nyingine ni sawa na kuchimba shimo ili uzibe shimo,angalia mfano mzuri ni Magufuri alihamishwa kutoka mifugo na uvuvi,sasa miongoni mwa waliowajibishwa ni pamoja na walioshika nafasi yake.
Kama hatutapata waziri mkuu wa kuwasimamia mawaziri waliochini yake kiufasaha,tutaendelea kucheza ngoma isiyokuwa na mwisho.
 
So baraza la mawaziri zima linavunjwa au zinafanyiwa replacement tu sehemu zilizo wazi.
 
JK ndo mwamuzi wa mwisho. CCM ina majembe mengi ambayo hayajatumika ipasavyo
Dr. wa ukweli alimwambia Kinana ndani ya CCM haoni waziri asiye mzigo kasoro wawili tu,

labda alikuwa anamaanisha hayo matairi mawili mnayoyazungusha kila wizara ambayo nayo yameanza kuota upara.
 
HIYO WIZARA ITAZIDI KUWAHARIBIA CV MAWAZIRI WA WIZARA HIYO HATA KAMA ATAWEKWA NANI, KWA SABABU WANAOIHARIBU WIZARA NI WALE MAKADA WATIIFU WA CHAMA CHA MAPINDUZI.Hakuna waziri atakayebaki salama atakayepewa hii wizara.
Hiyo ni kweli kabisa!
 
Kuna msemo usemao mchawi mkabidhi mwanao. Hivyo basi wizara ya maliasili na utalii likabidhiwe jembe Kinana!

Hii ni kali Mkuu! ni kweli mchawi mpe mwanao amlee,mana akiummwa malaria kidogo tu atafanya juhudi atibiwe,mana akifa ataambiwa karoga,hivyo basi Jangili kinana apewe ubunge viti maalumu,then apewe wizara anayotuhumiwa kuua tembo!
 
Back
Top Bottom