Ni mwaka wa ufukara na kudaiwa, hakika Tanzania ya viwanda sijaona

mkara mshamba

Member
Jan 15, 2020
16
45
Kuna nyimbo hadi matangazo yalikuwa yanatolewa na serikali yetu tukufu ya Tanzania ya viwanda. Binafisi nilfarijika sana nikiamini kuwa uchumi wa nchi na watu utakuwa na tunakwenda kuishi maisha ya kati kama tulivyo aminishwa. Lakini cha kusikitisha na kuuzunisha siku hizi hayo matangazo siyasikii, hata kuona viongizi wangu wakifungua viwanda pia sioni. Hatima yake naona bado uchumi wa watu unashuka hadi kufirisika, ajira zikiendelea kuwa mwiba na maisha ya Watanzania yakiwa magumu tofauti na yale ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

Wataalamu na wachumi, naomba kusaidiwa, HIVI TUMEFELI WAPI? Mheshimiwa alituambia kuwa nchi hii ni tajiri sana na inauwezo wa kujiendesha hadi kukopesha. Lakini kwenye lipoti ya CAG naona kama vile deni la taifa limeongezeka, sijajua ni kwanini. Sitaki matusi katika kuchangia naomba hoja, ni kwanini watu wanaendelea kufilisika na maisha ya Watanzania yakiendelea kuwa magumu mno? Tatizo liko wapi?

Nakumbuka moja ya hotuba za baba wataifa kuwa ili tuendelee tunaitaji vitu vinne (1) Watu (2) Aridhi (3) Uongozi bora na (4) Siasa safi. Hivi kwa hapa kwetu Tanzania tumekoswa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
May 11, 2014
2,078
2,000
"Tanzania ya viwanda inakuja ipo kitonga kuelekea Moro ikitokea mbeya. Kipindi kimoja hakitoshi tumuongezee kamuda kidogo" alisikika kada mmoja
 
Top Bottom