Ni mwaka wa maamuzi magumu kibovu,haramu na kichafu hakitapita.

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani. Ni mwaka wa maamuzi. Ni mwaka wa kuleta mabadiliko chanya ya kisiasa kupitia sanduku la kura.
Ni mwaka wa pekee ambao haujawahi kuwa na watz wenye mwamko mkubwa ktk kuleta mabadiliko ya kisiasa ktk nchi yao. Watz wamejiandaa vya kutosha. Kwa heri na kwa shari.
Na niwambie tu kuwa,mwaka huu kibovu na kichafu hakitapita. Kuna watu wamezoea kusafiria nyota mbovu na chafu kama ufisadi na rushwa. Mwaka huu mwisho. Chochote kilicho haramu,kibovu na kichafu hakitapita.
Ni kipindi cha kuonesha kuwa wakati wa kupitisha haramu,vibovu na vichafu umepita. Vilipata upendeleo vikaona kuwa ni haki,sasa imetosha.
Mmeishi kwa uchafu,unafiki na ubovu kwa sababu ya ujinga na upumbavu wa watu wachache mkijua kuwa ni haki.
Navipinga haramu na vibofu kwa nguvu zote. Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.
 
Kufanya maamuzi magumu yasiyo na tija wala weredi ni sawa sawa na sifuri! Kwanza lazima ujue tunakosea wapi na wapi na kurekebisha!
 
Soma uelewe,kwani Lowasa wanaposema ni mtu mwenye maamuzi magumu wanamaanisha kuwa ni maamuzi magumu yasiyo na tija?

Nimekuelewa sana, kauli ya maamuzi magumu kwa Wabongo ni wimbo ambao wengi wao hawajui maana yake, ndo maana nasema unaweza ukafanya maamuzi magumu, lakini still hayana faida kwako. Chamsingi fanya maamuzi magumu yenye mustakabali wa tija na weredi na yenye matokeo chanya kwako.
 
Noted BigBro!!

Back
Top Bottom