Ni mwaka wa 3 sijaangalia TV! Wageni wanashangaa kutokuta TV nyumbani kwangu!

wengine wajasiria mali wa maporini miezi mtu uko porini unasaka mahela mererani au kwenye mbaazi na ufuta huko ukirudi home umekaa sana siku 2.na tv za sikuhizi hazikamiliki mpaka uwe na king'amuzi kinyume cha hapo itakywa kama pazia tu waste of resource bora kununua music system hifi kuliko tv kama huna muda wa kuweka tako home
Hata mimi ni mtu wa field sana mkuu, lakini hili halikuwa kikwazo kwangu. Hivi vitu haviozi mkuu.
 
maisha yamerahisishwa sana, simu yatosha kupata habari na kuangalia Tv utakazo duniani kote, kama una bando hata huangaiki. Ila shida ni kwa hao "pasua kichwa" utakuwa umewaweka kwenye giza la kihabari na maarifa
 
Hata mimi ni mtu wa field sana mkuu, lakini hili halikuwa kikwazo kwangu. Hivi vitu haviozi mkuu.
tunajadili in general terms tu kwamba sio muhimu kivile hapa home nina kila taka taka hadi vingamuzi viwili lakini baada ya taarifa ya habari na mpira sina kipindi labda ikitokea tena stand up comedy ya wanasiasa wetu live especially yule mwanasiasa mkuu wa Tz hapo ndio nakuwa glued on telly ila most of shits naziangalia u tube !
 
Mi naangalia isindigo tu,kwani tumetoka nao mbali,
taarifa sijui itv,cloud,Tbc naona ni upotevu wa mda tu bora nisome zangu novel kwenye simu,
CNN nao washanichosha kila siku majungu ya trump collusion with russia etc,
 
Jamani, mie ni kitambo sana nimeshaacha kuangalia TV. Yani kuona TV labda niwe bar au kwa jirani.
Sasa wageni wengi wakija kwangu wanashangaa kutokuta TV. Kwani kuna shida kutokuwa na TV?

Sasa kama huoni umuhimu wa kuwa na TV hizo za huko baa au kwa jirani wazitazamia nini!!!

Uswahili tu utakuwa umekujaa...
 
Hata mimi sijaona umuhimu wa kuangalia tv, ila madogo lazima wazingue wakikosa tv home, huchelewi kuwakuta wapo jirani
 
Same applied kwangu,

Mwaka wa tatu sina TV,

Kuna watu wakinitembelea huwa huwanielewi kabisa,

Nipo mwenyewe by the way,

Huwa sijishughulishi kabisa na kuangalia TV,

May be sometimes movies naangalia kwa laptop
 
Si ubinafsi mkuu,

Kila ukirudi unakuta kuna kitu kimeharibika, Mara kimoja wapo kimeungua, ukiangalia unowaacha home ni watu wazima na ndevu zao, Mara rimoti imepotea

Nikaona kuongea sana isiwe tabu nitaambiwa nna gubu bure,

Kingine hawataki kufanya kazi kukicha kwenye TV hadi SAA 8 usiku

Sasa hivi wanasoma namba, na hakuna anayeshinda hme,
Mkuu malalamiko hayo kama ya mzee wangu kipindi niko home
 
tunajadili in general terms tu kwamba sio muhimu kivile hapa home nina kila taka taka hadi vingamuzi viwili lakini baada ya taarifa ya habari na mpira sina kipindi labda ikitokea tena stand up comedy ya wanasiasa wetu live especially yule mwanasiasa mkuu wa Tz hapo ndio nakuwa glued on telly ila most of shits naziangalia u tube !
Poa mkuu, ndio hivyo. Hata mimi hapo awali ilikuwa hivyo mi nilikuwa naangalia mpira tu.
 
Wewe binafsi ni sawa, ila nunua TV itakua na manufaa kwa watoto au wageni. Kweli mda haupo kwangu kuangalia TV, nikiwa sebuleni nipo bussy na JF, mambo yote ni JF
 
Jamani, mie ni kitambo sana nimeshaacha kuangalia TV. Yani kuona TV labda niwe bar au kwa jirani.
Sasa wageni wengi wakija kwangu wanashangaa kutokuta TV. Kwani kuna shida kutokuwa na TV?
Hao wageni watakuwa kizazi cha .com, enzi za chama kushika hatamu hatukuwa na TV
 
Labda kama unaishi peke yako bila familia
WAKATI MWINGINE TV BADALA YA KUJENGA MAHUSIANO NA MAONGEZI NA FAMILIA INABOMOA.KUNA KIPINDI HATA MIMI SIKUTAKA MTOTO AZOEE TV AKIWA MDOGO NILITAKA APENDE KUSOMA VITABU ZAIDI KWAHIYO SIKUWEKA TV MPAKA AKAWA NA MIAKA 5 NA MUDA WOTE NILIKUWA NAMUWEKA BIZE NA VITABU BAADAYE AKAANZA KWENDA KWA MAJIRANI KUANGALIA VITU VINGINE AMABAVYO SINA UWEZO WA KUZUIA KUANGALIA KAMA MIELEKA, VITA NK NIKAAMUA KUNUNUA TV ILA BADO HAJAKUWA ADDICTED KAMA WENGINE WANAOANGALIA TV KUANZIA ASUBUHI MPAKA UMEME UKATWE NA WAKIJA WATOTO WENZAKE ANAWAAMBIA HUU SIO MUDA WA TV NI KUSOMA NA WAKIWEKA CHANELS ZA OVYO PIA ANAWAKATAZA.KWAHIYO KUNA WAKATI TV SI KITU MUHIMU SANA
 
Jamani, mie ni kitambo sana nimeshaacha kuangalia TV. Yani kuona TV labda niwe bar au kwa jirani.
Sasa wageni wengi wakija kwangu wanashangaa kutokuta TV. Kwani kuna shida kutokuwa na TV?
Aisee we utakuwa ka ndugu yangu flani ana pesa ndefu lakini kwake hakuna TV.
Ana bonge na mansion hatari furniture zake najenga nyumba complete lakini hana TV.
Simwelewagi yani yeye habari gazetini
 
Kama huna pesa ya kununua sawa ila kinyume na hapo wewe ni lofa na mpumbavu...
 
Jamani, mie ni kitambo sana nimeshaacha kuangalia TV. Yani kuona TV labda niwe bar au kwa jirani.
Sasa wageni wengi wakija kwangu wanashangaa kutokuta TV. Kwani kuna shida kutokuwa na TV?
Ukiniondolea TV ndani ya nyumba umenikomesha! Nyumba ikiwa na godoro na tv tu naweza kuishi bila shida yoyote.
 
Mkuu tupo wengi. Mara ya mwisho kwangu waliangalia TV ilikuwa May 2016. Antena ya king'amuzi nilishampa mtu, decoder yenyewe watoto wanaiburuza kama gari, TV nimewawekea madogo chumbani kwao wanaangalia Movie na Video za kusoma siku maalum. Huwa nafungia DVD player chumbani kwangu. Nimewawekea Computer chumbani kwao nimewajazia movie za watoto za kawaida na za kujifunza.

Mimi na wife tunarudi usiku na hatuna mpango na taarifa ya habari. Nafuatilia habari mitandaoni hapa JF na habari za nje mitandao mingine.

Hii imesaidia kuwadhibiti watoto wasione makorokocho. House girls wengi ni watata wanaweka channel za mambo ya ovyo na wanakodi au kuazima DVD za mambo mabaya hadi ngono.
 
Back
Top Bottom