Ni mwaka 2020, mwaka wa uchaguzi, mwaka wa neema na machungu mwaka ambao waganga wa jadi wana thamani kuliko uhai

Masinki

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
694
451
Zingatia kichwa cha habari, hatimaye inaelekea kutimia, bado miezi michache sana kufanyike uchaguzi mkuu wa viongozi katika ngazi za urais, ubunge na udiwani.

Ndio ni mwaka ambao ni furaha sana kwa wanasiasa, wananchi na wapambe wa wagombea.

Lakini pia ni mchungu kwa baadhi ya wanasiasa na makundi yao(ndugu,jamaa,na marafiki bila kuwasahau wapambe)
Ni mwaka ambao wakina Mshana Jr na waganga wengine watachuma fedha haswa kutoka kwa ndugu zetu wanasiasa lengo ni kusaidiwa washinde kwenye nyadhifa waombazo.

Wagombea wameanza kujitokeza kwa kificho (kuna vyama vimezuia kampeni)wanaenda kwa wajumbe, viongozi wa ngazi za wilaya ili kujitambulisha ama kuelezea Nia mfano Jimbo nililopo kwa sasa kuna mtifuano mkali kati Mwl. Chacha Ryoba (Mbunge wa Sasa), Dr.Kebwe S.Kebwe, (Mbunge wa zamani), Marwa Chandi (x mnec,mfanyabiashara), Nkiri itabe (Mtendaji Kijiji Lobanda) na wengineo.

Sawa ni haki ya Kila mmoja kugombea nafasi za uongozi lakini kama taifa lazima tuangalie watu wa kuwapatia nafasi za kuongoza,kwenye urais sina shaka sana maana Dr Magufuli kwa upande wangu anafaa, kwa upinzani niseme kweli sijaona mtu mwenye leadership quality, hawajaandaliwa kuwa viongozi wa nchi labda wa vyama ambapo na kwenyewe wanafeli, rejea kauli ya Baba wa Taifa kwamba mpinzani wa kweli atatoka CCM.

Nitoe Rai kwa Benard K Membe, ni vema akarudi kwa Dr Magufuli aombe msamaha no matter what, hawezi kuwa Rais wa nchi iwe kwa amani ama kwa shari, he can't be there, so sululuhisho ni kuomba msamaha walau aje azikwe kwa heshima kama walivyofanya wenzake Lowassa & Sumaye.

Aidha rafiki zangu wapinzani ni wakati wa nyinyi kujitafakali upya nilishangaa Sana Chadema kumpa Tena Mbowe Freeman uenyekiti wa Taifa,mnapaje mtu aliyefeli hata jimboni kwake? Hivi hamuoni yule DC HAI alivyomzidi akili?

Anyway endeleeni, lakini sure nawaambieni hamna jipya na wala hamsutui kwenye ubunge mkipata walau watatu (3), udiwani(15) mshukuru sana Mungu. Maana itakuwa ajabu kama shule ya kata Machochwe wanafunzi wake kupata division One darasa zima.
 
Nauona ni mwaka wa vijana kama hakutakuwa na kubebana na kujuana sijui huyu nilikuwa naye chuo, sijui wizarani, sijui alinipa zawadi, sijui ni mwenzetu. Hawa wazee wastaafu wanatakiwa wapumzike. Utakuta rais ana miaka 60, katibu mkuu ccm miaka 50+, lakini utakuta mgombea ambaye amestaafu utumishi wa umma ana miaka zaidi ya 65 anataka kuwatumikia wananchi. Ubunge/udiwani sio pensheni bali ni mzigo wa kuwatumikia wananchi. Sasa mtu ana miaka 65-75 amechoka kichwani hadi kufikia kustaafishwa et leo hii anarudi kuwatumikia wananchi wenye changamoto lukuki. Walikuwa wapi wakati bado wana nguvu. Au walitaka wapate pensheni ya kutolea rushwa? Huu ni wakati wenu vijana, vyama tambueni hilo. Huwezi kumkamua maziwa ya kutosha ng'ombe mzee aliyejichokea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Nitoe Rai kwa Benard K Membe, ni vema akarudi kwa Dr Magufuli aombe msamaha no matter what, hawezi kuwa Rais wa nchi iwe kwa amani ama kwa shari, he can't be there, so sululuhisho ni kuomba msamaha walau aje azikwe kwa heshima kama walivyofanya wenzake Lowassa & Sumaye."

Hii aya ndio imenichefua zaidi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi wa kijinga kabisa!sasa kati ya jiwe na membe nani kiongozi hapo?HIVI KIONGOZI ANAWEZA KUWAAMBIA WANANCHI KUWA HAJALETA TETEMEKO????ANAWEZA PAKIA TWIGA APELEKE KWAO???ANAWEZA MZUNGUMZIA MWENZAKE VIBAYA MBELE ZA WATU?ANAWEZA ONGOZWA NA KISASI???muwe mnaacha ujinga!!!ADMINI PIGENI BAN HUYU MWIMBA PAMBIO!!!!
 
Ni mwaka ambao wakina Mshana Jr na waganga wengine watachuma fedha haswa kutoka kwa ndugu zetu wanasiasa lengo ni kusaidiwa washinde kwenye nyadhifa waombazo.

Jr
 
"Nitoe Rai kwa Benard K Membe, ni vema akarudi kwa Dr Magufuli aombe msamaha no matter what, hawezi kuwa Rais wa nchi iwe kwa amani ama kwa shari, he can't be there, so sululuhisho ni kuomba msamaha walau aje azikwe kwa heshima kama walivyofanya wenzake Lowassa & Sumaye."

Hii aya ndio imenichefua zaidi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Usiseme hivo siasa ni upepo na hakuna ajuaye kesho yake,hata aliyopo akutegemea kuwa alivo
 
Uzi wa kijinga kabisa!sasa kati ya jiwe na membe nani kiongozi hapo?HIVI KIONGOZI ANAWEZA KUWAAMBIA WANANCHI KUWA HAJALETA TETEMEKO????ANAWEZA PAKIA TWIGA APELEKE KWAO???ANAWEZA MZUNGUMZIA MWENZAKE VIBAYA MBELE ZA WATU?ANAWEZA ONGOZWA NA KISASI???muwe mnaacha ujinga!!!ADMINI PIGENI BAN HUYU MWIMBA PAMBIO!!!!
Ipo tofauti ya mtawala na kiongozi
 
Back
Top Bottom